Kwa kura tano za kukubali dhidi ya kura tatu za kukataa, majaji wa Mahakama ya Kikatiba ya Ecuador wametambua haki ya mtoto mwenye wazazi wote wa jinsia moja ambapo nchini humo inajulikana kama kesi ya Satya.
Satya ni mtoto wa Nicola Rothon na Helen Bicknell, wanawake wawili wa Uingereza wanaoishi nchini Ecuador wanaoishi kinyumba na walimpata mtoto wao kwa njia ya upandikizaji.
Hata hivyo, kuzaliwa kwa Satya hapo 2012 kulikuja na msuguano wa kisheria. Nchini Ecuador, kama ilivyo nchi nyingine zenye uhasili wa Kihispania, ni utamaduni mtu kuwa na majina mawili ya ubini na kwa wazazi wenye mahusiano ya kawaida (mwanaume na mwanamke), jina moja hutoka upande wa baba na jingine hutoka upande wa mama.
Lakini wakati Rothon na Bicknell walipojaribu kumsajili mtoto wao kwa ubini wa pande zote mbili, Msajili wa Umma wa Ecuador alikataa.
Miaka sita baadaye, baada la malalamiko ya kisheria, midahalo na majadiliano kadhaa baina ya wananchi na vyombo vya habari, mwanzoni mwa Juni 2018 mahakama iliamua kuwa lazima Msajili wa Umma lazima amsajili Satya kwa majina ya mama zake.
Uamuzi huouliamsha hisia nyingi tofauti mitandaoni. Katika tovuti kama vile Medium, kwa mfano waangalizi waliamini kuwa shauri la Satya litaleta mwangi katika historia ya haki za kiraia nchini Ecuador.
Mtaalamu wa Haki za Binadamu Benalcázar Alarcón alionyesha kuwa mwitikio wa wafanyakazi wa Usajili wa Umma unaakisi jinsi kesi hii ilivyoamsha changamoto katika misingi ya suala la ubini toka pande mbili ambapo limekubalika kama la “asili” katika historia ya nchi:
La Corte Constitucional al resolver la acción extraordinaria de protección, da un paso trascendente y transformador frente a las estructuras culturales, jurídicas, ideológicas y políticas que sostuvieron un régimen de discriminación […] por su parte, Satya, Helen y Nicola a través de su sueño de vivir la simple y tierna felicidad de una familia, rompen materialmente siglos de exclusión y plantean a la sociedad la legítima presencia de la diversa condición humana.
Mahakama ya Kikatiba imefanya kitendo cha kipekee kabisa cha ulinzi na ni hatua muhimu na ya mabadiliko katika utamaduni, sheria, mitazamo na mifumo ya kisiasa ambayo huunga mkono unyanyapaa. Na kwa Satya, Nicole na Helen katika ndoto yao ya kuwa na familia yenye furaha na amani, wamevuka vikwazo vya kutengwa na kuweka msingi wa utambulisho wa uwepo wa utofauti katika hali za ubinadamu
Kesi moja kati ya nyingi
Familia za wazazi wa jinsia moja zipo Ecuador, lakini kutokuonekana kwao kisheria husababisha matatizo ya mara kwa mara. Kama, kwa mfano mmoja wa wazazi akifariki na mtoto hana jina la ubini wa mzazi aliyesalia, mzazi huyo hupoteza haki zote za malezi kwa mtoto kwa sababu hawajasajiliwa kisheria kama mzazi na mwanae. Na hili husababisha serikali kumuweka mtoto katika orodha ya kuasiliwa.
Madhara ya kutengana kwa wazazi humaanisha kupoteza haki ya uzazi na matunzo, kumtembelea mtoto na mengi yanaweza kuzuiwa kutokana na haki za urithi na utambulisho kisheria.
Kwa ujumla, kutokuwa na uhakika huko ni matokeo ya wazazi wa jinsia moja kutokuwa na haki sawa mbele ya sheria. Hivyo, kutoka kwa mhariri wa tovuti Andes, maamuzi ya mahakama ni muhimu:
Es, además, una forma de reconocer una situación social que se da de hecho y cuyo desconocimiento oficial no hace sino llevar a niños, niñas y adolescentes que se crían en familias no convencionales a no gozar de la protección que deben proveer el Estado, la sociedad y la familia para lograr su desarrollo integral.
Hii ni zaidi ya njia ya kutambua hali ya kijamii ambazo hakika hutokea ambapo maafisa wasiojua hawafanyi chochote lakini huwachukuwa wasichana na wavulana na matineja ambao hukulia katika nyumba zisizo za kawaida ambapo hawapati ulinzi ambao wangeupata kutoka kwa serikali, jamii au familia ili kuwa na ukuaji mzuri.
Wachambuzi wengine waliopitia shauri la Satya walisema kuwa umuhimu wa shauri hili bado haujaonekana:
El #casoSatya tiene una importancia que aún no logramos dimensionar. Acá lo ponemos en #Contexto. https://t.co/rb0DTaIjaH
— GK (@GKcityec) June 12, 2018
Shauri la Satya lina umuhimu ambao hatujaweza kuupima bado. Hapa tunaliweka katika mazingira halisi
Ni mwanzo tu
Inaonekana kwamba uamuzi wa mahakama utakuwa ni kwa shauri hili pekee na Bunge litakuwa na mwaka mmoja wa kutengeneza sheria mpya kuziba mwanya huu. Kwa sasa, Msajili wa Umma atautaka Umma radhi kama ilivyotarajiwa na pia kuchukuliwa hatua kwa watumishi waliokataa kumsajili Satya. Wote wanaoifuatilia kesi hii wanatarajia bunge kutumia maamuzi ya shauri hili kama muongozo wa kuweka taratibu mpya zitakazotambuliwa na katiba ya nchi, haki ya utambulisho, usawa mbele ya sheria na hatua kuu kwa maslahi ya shauri yawe: haki za watoto ambao ni sehemu ya familia za wazazi wa jinsia moja.
Kwa kuanzia na marekebisho ya katiba ya mwaka 2008,mfumo wa kisheria kwa ajili ya wanachama wa chama cha wapenzi wa jinsia moja nchini Ecuador umepanuka kwa miaka kadhaa iliyopita. Marekebisho hayo ya katiba yalitambua utofauti wa familia katika wigo mpana, utofauti baina ya utambulisho na njia za kujamiiana na ndoa za jinsia moja, kati ya mambo mengine.
Baada ya muongo mmoja tukiwa na katiba mpya ya Ecuador, bado miiko ya kijamii yenye kuwanyanyapaa wapenzi wa jinsia moja ipo na ikiwazuia kupata haki zao na kuwafanya si kitu.
Makala fupi yenye jina la “Satya: Shauri la Helen na Nicola” lilitoa mwanga juu ya ugumu uliopo katika mdahalo huo. Wanaharakati wa haki za wapenzi wa jinsia moja, watetezi wa haki za binadamu na wawakilishi wa vikundi vinavyopinga kumtambua Satya kama msichana mwenye mama wawili vilishiriki katika kutengeneza filamu hiyo.
Vikundi hivyo vinasema kuwa sababu ya pingamizi hilo sio kwa sababu za dini, lakini ni “kwa sababu za kijamii”: wanatafuta kulinda ” heshima ya utaratibu wa asili” na ” usawa” unaoletwa na elimu ambayo hutolewa kwa familia zinazoundwa na mwanaume na mwanamke.
Kwa upande mwingine wapigania haki za binadamu wameongelea umuhimu wa kuangalia mashauri mengine ya zamani kama vile haki za wanawake kupiga kura ambapo lilikuwa jambo lisilowezekana kwa karibu karne moja iliyopita …..na maendeleo ya jamii kwa pamoja.
Wanatamani Ecuador kujiunga na mwenendo wa ulimwengu ambapo usawa unakuwa desturi kwa kutambua rasmi haki za watu wote hasa zile zisizotambuliwa na jamii zenye mfumo dume au desturi zote mbili, na ambao haki zao zinaweza kudhulumiwa na sheria.
Danilo Marzano, mwanachama wa chama cha wapenzi wa jinsia moja ambaye alifanya mahojiano kwa ajili ya makala fupi wakati wa moja ya mihadhara ya kumuunga mkono Satya, Nicola na Helen alisema:
“En realidad hoy más que un deseo personal es un deseo colectivo. […] Necesitamos estar incluidos dentro de los beneficios constitucionales como ciudadanos de primera categoría. No es solamente el caso de Satya […Es] importante reconocer constitucionalmente el derecho de las familias homoparentales; que tanto hombres como mujeres de las poblaciones del LGBTI podamos tener derecho a conformar nuestras propias familias […] derecho al desarrollo de la libre personalidad de amar [más aún al estar bajo la protección de una constitución] supuestamente tan de avanzada […] tan progresista [Algo que, sin embargo] no ha sido cierto.
Katika uhalisia, [utambuzi wa familia za wapenzi wa jinsia moja] ni matamanio ya wengi na sio kwa mtu mmoja. Tunahitaji kujumuishwa katika maslahi ya katiba hiyo hiyo moja [kama watu wengine na] kama raia wa daraja la kwanza. Sio shauri la Satya pekee [ni….] . muhimu kuzitambua kisheria familia zenye wazazi wa jinsia moja, ambapo wanaume na wanawake wa jumuia ya wapenzi wa jinsia moja wangeweza kuwa na haki ya kuunda familia zao wenyewe, haki binafsi ya uhuru wa kupenda [hata zaidi, chini ya ulinzi wa katiba] ambayo [ni] imeboreshwa na ni endelevu. [Kitu chochote kinachobeza hili,] hakijawa na ukweli.
Kupigania haki hizi inapata umuhimu zaidi baada ya ugunduzi wa Chuo cha Takwimu na Sensa cha Taifa (NISC), ambapo ilifichua viwango vya kutisha vya unyanyapaa na vurugu: “kati ya wanachama wa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja waliohojiwa, asilimia 70.9% waliripoti kuwa walishawahi kukumbwa na unyanyapaa katika mazingira ya nyumbani mwao.”
Na kwa asilmia 72.% walishawahi kudhibitiwa, 74.1 walishawahi kukutana na aina aina za mashambulizi, 65.9% walishakumbana na kukataliwa na 62.4 walishawahi kufanyiwa vurugu.”
Makala hii imeandikwa kwa msaada wa waandishi wenza kutoka Global Voices Daniela Gallardo, ambaye amekuwa akifuatilia shauri la Satya kwa ajili ya Global Voices kuanzia mwanzo wake mwaka 2012 kupitia muendelezo wake mwaka 2014.