Ripoti ya Raia Mtandaoni: Sheria ya Uganda ya Kodi ya WhatsApp na Kadi za Simu Itafanya Iwe Vigumu Kuendelea kutumia Mtandao

Telco ad akiwa kwenye gari dogo Kampala, Uganda. Picha na futureatlas.com kupitia Flickr (CC BY 2.0)

Taarifa ya raia mtandaoni ya Advox inatoa picha ya haraka kimataifa juu ya changamoto, ushindi na mienendo inayoibuka katika haki za kimtandao duniani.

Serikali ya Uganda ilithibitisha kuwa sheria mpya ya kodi itahusu kiwango cha kodi ya huduma na bidhaa ikijumuisha akaunti ya fedha za simu na and huduma za mitandao ya jamii kama vile Facebook na WhatsApp.

Watunga sera walipopendekeza tu kile kinachoitwa “Kodi kwa ajili ya WhatsApp”, waungaji mkono wa pendekezo hilo– miongoni mwao alikuwa Rais Yoweri Mseven– alisema kwamba ingesaidia kupunguza “umbea” kwenye mitandao ya kijamii. Na lilipokelewa vizuri miongoni mwa watoa mawasiliano ya simu ambao hawafaidiki moja kwa moja na kutumia mitandao hiyo ya kigeni “mikuu” kama huduma za WhatsApp.

Katika mahojiano na mganda Pru Nyamishana ambaye mwanabloga na mwandishi wa Global Voices aliambia BuzzFeed kwamba :

Moja ya changamoto kubwa tunazokabiliana nazo ni upatikanaji wa mtandao. Kodi hii inafunga watu kuwa nje ya mtandao….tunaamini kuwa huu ni mpango wa makusudi kutaka kujua idadi ya waganda ambao ni watumiaji wa mtandao ili kunyamanzisha sauti za wapinzani.

Serikali ya Uganda ikitaja kutekwa na mauaji ya watu ya hivi karibuni imehitimisha kifungo cha miezi miwili cha ununuaji wa kadi za simu na kuamuru makambuni ya simu kuorodhesha watu wote wenye kadi mpya za simu kwenye kituo cha taarifa za kibayometriki cha taifa . Serikali pia imefunga mauzo ya kadi zinazokwanguliwa kwa ajili ya kuongeza salio kwenye simu.
Mamlaka zinasema kuwa wahalifu huwasiliana kwa kutumia kadi za simu ambazo hazijasajiliwa ili kupanga mikakati ya mashambulio bila kufatiliwa.

Wakati katazo juu ya kadi za simu limeondolewa, sasa sheria
mpya inawataka waganda wakati wananuna kadi hizo kutoa kadi za utambulisho wa taifa kwa wachuuzi ili zithibitishwe kwenye kadi ya umeme inayosoma taarifa ya mnunuzi wa kadi za simu.
Kwa sheria hii mpya inayotarajia kuanza Julai mosi, wateja watatakiwa pia kutumia akaunti za fedha za simu zao kuongeza muda wa maongezi kwenye kadi za simu zao.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na chama cha kulinda walaji cha Uganda kilisema kuwa hatua za kudhibiti kadi za simu zisingepunguza kiwango cha uhalifu. Akiandika kuhusu sheria ya kodi mpya, Juliet Nanfuka wa ushirikiano wa sera ya kimataifa ya TEHAMA kusini mwa Afrika(CIPESA) aliiita sheria hiyo kuwa “ni kitendo kipya katika mfululizo wa matendo ya serikali ambayo yanatishia upatikanaji wa mtandao kwa wananchi.”

Sera hizi mpya zikitelezwa kwa pamoja ni gharama kubwa kwa waganda – na hasa wale wanaoishi katika umaskini– kila siku kuwasiliana na kufanya shughuli nyingine mtandaoni kwa kutumia simu zao za mkononi.

Mtandao katika jimbo la tamil Nadu India wafungwa kufuatia mauaji ya waandamanaji

Baada ya askari polisi kufyatua risasi na kuua raia 13 katika maandamano ya umma kusini mwa jimbo la Tamil Nadu India vifaa vya mawasiliano na simu za mononi zilizounganishwa kwenye mtandao vilifungwa katika wilaya tatu kwa amri ya mamlaka ya serikali za mtaa. Waandamanaji walikuwa wanapinga upanuzi wa machimbo ya shaba ambao walisema unahalibu hewa na maji katika wilaya yao na kufanya afya zao kuwa katika hatari. Picha za video za askari wakiwatendea ukatili waandamanaji zimekuwa zikisambazwa katika mitandao ya kijamii ambazo ziliwaacha wengi na wasiwasi juu ya nia ya serikali ya kuondoa upatikanaji wa mtandao.

Kutokana na kituo huru cha sheria cha habari nyororo za mtandao cha New Delhi, kumekuwa na kuzimwa kwa mtandao katika kanda 55 nchini India hadi mwaka 2018.

Papua New Guinea yatoa katazo la mwezi mmoja kutotumia Facebook likitaja kuwepo kwa ‘watumiaji bandia’

Maafisa kusini mwa jimbo la kisiwa cha Pacific cha Papua New Guinea wataweka katazo la mwezi mmoja kutotumia facebook , kwa kile wanachosema ni jitihada za kuelewa jukwaa hilo vizuri zaidi ambalo limechochea kusambaa kwa taarifa za uongo mtandaoni.

Katika mahojiano na gazeti la Gardian , msomi wa vyombo vya habari vya kidigitali na mwandishi wa Global Voices, Aim Sinpeng alieleza kuhusu katazo hilo, lakini pia alibainisha kwamba kule kuna athari kidogo kuliko sehemu nyingine yoyote ulimwenguni kutokana na uwiano mdogo wa watumiaji wa mtandao. Papua New Guinea ina idadi ya watu ambao wanazidi kidogo milioni nane na kiasi kinachoingia kwenye mtandao ni asilimia 12 tu.

Wakili wa haki za binadamu wa UAE akabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela kwa sababu ya harakati katika mitandao ya kijamii

Wakili wa haki za binadamu wa Emirati Ahmed Mansoor alihukumiwa miaka kumi jela na mahakama ya rufaa kwa kusambaza habari za “chuki na kubagua” na kuchapisha “habari za uongo” kwenye mitandao ya kijamii. Pia alipigwa faini ya kulipa milioni moja ya Abu Dhabi (ni sawa na dola za Kimarekani 272,000) kwa “kutukana hadhi na heshima ya UAE.”

Mansoor aliwekwa kizuini tangu Machi 2017, ni miongoni mwa mawakili wachache wanaotetea haki za binadamu katika nchi ya Guba ambaye alipewa tuzo ya watetezi wa haki za binadamu ya Martin Ennals mwaka 2015 . Pia, aliwahi kufungwa mwaka 2011 baada ya kufanya kampeni ya mabadiliko ya kidemokrasia katika UAE na alisaini ombi la waraka wa demokrasia nchini humo. Kuanzia muda huo hadi anakamatwa hivi karibuni, amekumbwa na unyanyasaji na ufuatiliaji wa karibu mno mtandaoni na nje ya mtandao.

Kampuni ya Amazon. Com inatumia habari nyororo kusaidia serikali kufuatilia wakazi wa Marekani.

Amazon. com wameanzisha kitambuzi cha kielektroniki chakutambua uso kinachojulikana kama Rekognition, ambacho kampuni inasema ni zao ambalo linaweza “kutambua sura katika sura milioni kumi na kuchunguza sura hadi 100 katika picha nyngi.”

Sheria ya uhuru wa habari inamtaka mwanasheria mkuu wa Umoja wa uhuru wa raia Marekani kupata na kutoa barua pepe kuthibitisha kuwa amazon imekuwa ikiuza kitambuzi hicho serikali za mtaa katika majimbo ya Arizona, California na Oregon na kampuni hiyo imewapa mafunzo na ushauri wa kitaalam maafisa wa serikali katika mkataba wa siri.

Pia Umoja huo ulimwandikia barua ya pamoja Mtendajii mkuu Jeff Bezos wa Amozon, iliyodai kwamba Amazon “iache kuimarisha miundombinu ya serikalini ya ufuatiliaji ambayo inatishia sana wateja na jamii nchini kote.” Baraza la mahusianao ya kiislamu Marekani, Umoja wa kujitolea wa kielektronik na waangalizi wa haki za binadamu walikuwa ni miongoni mwa watia saini barua hiyo.

Tafiti Mpya

 

 

Jiunge na taarifa za raia mtandaoni

 

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.