Maandamano ya Nicaragua Yachochea Kufungwa kwa Vyombo vya Habari, Shambulizi la DDos na Mauaji ya Mwandishi wa Habari Angel Gahona

Waandamanaji wakiwa katika viunga vya Managua, mji mkuu wa Nicaragua, mapema Aprili 2018. Picha kwa hisani ya Sauti ya Amerika, imetolewa kwenye jamii kupitia Wikimedia Commons.

Ripoti ya Utetezi wa Raia wa mtandaoni inakuletea mkusanyiko wa changamoto, mafanikio na mwenendo wa matukio yanayojitokeza kuhusiana na haki za matumizi ya mtandao wa intaneti ulimwenguni kote.

Kwa mujibu wa kituo cha Haki za Binadamu cha Nicaragua, watu zaidi ya 34, akiwemo mwanahabari mmoja wameshapoteza maisha hadi sasa wakiwa kwenye maandamano nchini Nicaragua kwa kipindi cha siku kadhaa zilizopita.

Maandamano yaliyoanza kwa ajili ya kupinga mabadiliko ya bima za jamii yalichukua sura mpya hadi kuwa kilio kikuu cha wananchidhidi ya uongozi wa Rais Daniel Ortega, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 11 lakini akiwa ameshashika nyadhifa mbalimbali za kisiasa tangu mageuzi ya Sandinista ya mwaka 1979. Kwa sasa baadhi ya raia wanamtaka kuondoka mdarakani.

Vituo kadhaa vya runinga vimekuwa havipatikani hewani au vimezuiwa kurusha matangazo ya maandamano ikiwa ni pamoja na kituo kimoja cha Redio . Tovuti huru za habari za wazawa La Prensana Confidencialzilikabiliwa na kile kinachodhaniwa kuwa ni kuzuiwa kutoa huduma kufuatia Shambulizi la Kuzuia Tovuti Kutoa Huduma (DDoS). Tovuti zote zilikuwa zikiripoti kwa wakati halisi matukio yote yaliyokuwa yanatokea wakati wa maandamano.
Touti ya Confidencial ilishambuliwa na kutopatikana kwa masaa saba mnamo Aprii 23. Kupitia ujumbe wa Twiter, mhariri Carlos Chamorro alithibitisha shambulio hili kwa kuandika:

KWA WASOMAJI WETU. Kwa kipindi cha masaa matatu yaliyopita, tovuti ya Confidential haikuwa inapatikana. Tumegundua kuwa kilichosababisha ni shambulio la makusudi kutoka kwa maadui wasiopenda uhuru wa vyombo vya habari. Mafundi wetu wanashughulikia tatizo hili ili kurejesha mawasiliano. Tutaendelea kuwapa yanayojiri kupitia mitandao ya kijamii.

Tovuti ya Inter-American Press Association ililaani mashambulizi haya.

Katika jiji la Bluefields, kwenye pwani ya Caribean ya Kusini mwa Nicaragua, mwanahabari aliyebobea kwenye video Angel Gahona aliuwawa kwa kupigwa risasi akiwa anachukua picha za video na kutangaza moja kwa moja kupitia Facebook makabiliano kati ya waandamanaji na polisi. Gahona alikuwa akiishi na familia yake na pia akisimamia kituo chake kidogo cha habari kinachojulikana kama El Meridiano. Mashududa kadhaa wanasema kuwa polisi ndio waliokuwa na silaha nzito ambazo zingeweza kumpiga mtu na kumuua. Hadi sasa polisi bado hawajatoa taarifa kufuatia kifo cha Gahona.
Gahona hakupoteza maisha hapohapo, hali iliyomruhusu angalau kuchukua video za baadhi ya matukio mara baada ya kupigwa risasi, ambayo hadi sasa yamekuwa yakitazamwa ulimwenguni kote kupitia You Tube na vyombo mbalimbali vya habari. Kwenye mahojiano na Univisión,dada yake alisema: “Sikuweza kuamini ikiwa alichukua video ya kifo chake mwenyewe.”

Taasisi ya Mataifa ya Amerika na Tume ya Mataifa ya Amerika ya Hali za Binadamu kwa pamoja zimelaani vitendo vya kufungia vyombo vya habari na mauaji ya Angel Gahona. Watu wa familia yake wanaomba msaada wa mazishi ya ndugu yao pamoja na fedha za kuendeshea maisha yao kupitia anwani ya GoFundMe.

Mwanaharakati wa Kihispaniola alikamatwa kwa kosa la kukashifu serikali ya Kifalme kupitia ukurasa wa Facebook

Roberto Mesa, mwanaharakati wa mtandaoni katika kisiwa cha Kihispaniola cha Tenerife alikamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake mapema Aprili 18 mara baada ya kuchapisha ujumbe kwenye Facebook akisema kuwa familia ya Kifalme yapaswa kwenda kwa “mshauri nasaha”. Kwa Kihispaniola, ujumbe huu unasomeka: “Los Borbones, a los tiburones.” Wanaomuunga mkono wanaona kuwa mwanaharakati huyu atahukumiwa kwasheria ya nchi ya usalama ya Hispania, ambayo mara nyingi hufahamika kama sharia kabaji (“Ley Mordaza”), inayoweka makataa mbalimbali ya maandamano ya wazi na ya mtandaoni.

Tovuti ya Habari na Mijadala ya Nchini Tanzania Yapata Shambulizi la Kuzuiwa Kutoa Huduma (DDoS)

Jukwaa la habari na mijadala la nchini Tanzania Jamii Forums kwa kiasi fulani halikuwa linapatikana wiki hii kutokana na shambulizi la matandaoni la kuzuiwa kutoa huduma (DDoS). Likifahamika kwa mijadala mizito ya kisiasa na uwekaji bayana wa matendo ya rushwa kupitia maoni na mijadala kwenye nyuzi mbalimbali, kama ilivyo kwa Reddit, Jamii Forums ni moja ya tovuti maarufu sana kwa ukanda wa Afrika Mashariki. Mwanzilishi mwenza na mmiliki wa Jukwaa la Jamii Forums, Maxence Melo kwa sasa anakabiliwa na kesi chini ya sheria ya Tanzania ya makosa ya mtandaoni kwa kukataa ombi la polisi la kumataka kutoa taarifa za watumiaji wa jukwaa lake.

Maudhui ya Haki za Wasagaji, Mashoga, na Mabasha (LGBT) Yasitishwa Kukaguliwa Nchini China, Shukrani kwa Shinikizo kutoka kwa Wananchi

Kampeni ya kupitia mitandao ya kijamii ya #IamLGBT ilikilazimisha Chombo cha Usimamizi wa Mawasiliano cha China kupunguza ufuatiliaji wa maudhui ya LGBT kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, mara baada ya Weibo kutangaza kuwa michezo ya mtandaoni, habari mbalimbali na maudhui ya LGBT yatakuwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi mitatu, kiungoishara cha #IamLGBT kilitumiwa mara 500,000 na kilikuwa na watazamaji milioni 500. Ndani ya siku chache, gazeti la Chama cha Kijamaa (Chinese Communist Party)-People’s Daily lilichapisha hati inayosema kuwa maudhui ya LGBT hayapaswi kufananishwa na maudhui ya hovyo, kidhalimu au ya kingono, na pia Weibo ilitangaza kuwa uhamasishaji wake wa miezi mitatu hautahusisha tena maudhui ya LGBT.

Je,Ni kweli kuwa Kundi la Urusi la Propaganda za Mtandaoni Linaanzisha Chombo cha habari?

Kundi la Urusi la propaganda za mtandaoni lililo na uhusiano wa karibu na Taasisi ya Utafiti wa Intaneti ya Saint Petersburg ilitangaza azma yake ya kuzindua mradi mpya wenye jina “USA Really” mapema mwezi ujao. Mradi huu, ambao hapo awali uliripotiwa na tovuti ya EU vs Disinfo, unasimamia kidete kupambana na Magharibi, kuchukizwa na kisa cha kiliberali cha juhududi zilizopita za Wakala wa Utafiti wa Mtandao wa Intaneti, ambayo iliteka vichwa vya habari vya kimataifa mnamo mwaka 2016, kabla na baada ya chaguzi za Urais nchini Marekani. “Asasi ya Habari” inayojipambanua yenyewe ya RIA FAN ilitangaza:

Taarifa zinazosambaa kutoka Marekani na kwa washirika wake, na ambazo zinalenga kushushia hadhi Shirikisho la Kirusi, halipaswi kunyamaziwa na vyombo vya habari vya Urusi.… Federal News Agency (FAN) haitafumbia macho ubabe wa mamlaka za Marekani katika tasnia ya uhabarishaji.

YouTube Yaondoa Mamilioni ya Video, Nyingi Zikiwa za Taswira za Machafuko na Udhalilishaji

YouTube iliondoa zaidi ya video milioni 8.2 kati ya Oktoba na Disemba 2017, ambapo video milioni 6.68 zilitambuliwa moja kwa moja kwa kutumia mifumo iliyobuniwa mahususi kwa ajili ya kutambua video za udhalilishaji wa kijinsia pamoja na picha za ukatili uliokithiri. Youtube ilitoa taarifa hii katika Ripoti ya uwazi ya hivi karibuni, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa kampuni mama ya Silicon Valley kuweka taarifa ya kina ya namna hii kuhusu maudhui yaliyoondolewa kwenye tovuti yao. Ni nani atakayefuata?

Facebook Yatoa Miongozo Ya Ofisi Kuhusu Udhibiti wa Maudhui

Facebook ilifanya uamuzi wa kufanya mchakato wa kudhibiti maudhui kuwa wa wazi zaidi kwa kuweka hadharani taratibu karibu zote za kiofisi ambazo hutumiwa na wadhibiti wake kama namna ya kuimarisha uaminifu wake kwenye jamii. Kampuni [ya Facebook] haikuweka wazi taarifa kuhusu mambo kama vile ya ugaidi ili kutoruhusu watumiaji kutumia taratibu hizo kujinufaisha.
Pia, Kampuni hii ilitangaza mipango ya kuruhusu watumiaji kukata rufaa kuondolewa kwa picha, video au andiko sambamba na kuondolewa kwa akaunti au ukurasa kwa kundi fulani la maudhui. Katika siku za mbeleni, Facebook yaweka wazi kuwa itawapa watu nafasi ya kuongeza maudhui pamoja na kuruhusu watumiaji kukata rufaa ya maudhui yaliyotolewa taarifa na kutozingatiwa.

Tafiti Mpya

 

Jisajili na Netizen Riport

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.