Kipi Kinajiri Maekelawi? Simulizi ya Ukatili wa Kituo cha Kushikilia Watuhumiwa cha Ethiopia Kinachotarajiwa Kufungwa

Wanachama wote wa Zone9 wakiwa Addis Ababa, 2012. Kutoka kushoto kwenda kulia: Natnael, Abel, Befeqadu, Mahlet, Zelalem na Atnaf. Picha kwa hisani ya Endalk Chala.

Wiki hii, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Desalegn alitangaza kuwa Maekelawi, ambacho ni moja ya vituo maarufu vya kushikilia watuhumiwa wa makosa mbalimbali, hivi karibuni kitaweza kufungwa.

Hatua hii imeibua hisia mbalimbali miongoni mwa raia wengi wa Ethiopia walioshuhudia vitendo vya mahojiano yanayoambatana na mateso makali walivyovishuhudia walipokuwepo Maekelawi. Miongoni mwao ni mwandishi wa Global Voices na mwanablogu wa haki za binadamu Befeqadu Hailu.

Mwaka 2014, Befeqadu alikamatwa sambamba na waandishi na wanablogu wenzake kwa sababu ya ushiriki wao wa pamoja wa kuendesha blogu inayofahamika kama Zone9, jukwaa walilolitumia kuandika maoni yao kuhusu wajibu wa serikali kwenye haki za binadamu na utawala wa sheria.

Waandishi hawa tisa walishikiliwa huko Maekelawi bila ya kufunguliwa mashitaka yoyote kwa takribani wiki 12 mwaka 2014, kabla ya kushitakiwa kwa sheria ya nchi ya kukabiliana na Ugaidi.

Baadae Befeqadu aliandika alitoa maelezo yake mwenyewe ya uzoefu wa kushikiliwa kwenye kituo hiki, maelezo tunayoyaweka hapa kama namna ya kutupia jicho hali ya ukweli wa mateso ya Maekelewi, kituo kinachoendeshwa na serikali ya sasa ya Ethiopia.

Mapema mwezi Agosti 2014 barua iliyowasilishwa Global Voices na wanasheria wa mwanablogu huyu, Befeqadu aliandika:

Wazo la kutia mguu kwenye eneo la mateso makali la Kituo cha Ushikiliaji cha Maekelewi kinaweza kusababisha homa ya baridi kali kwa yeyote anayefahamu historia yake. Hata hivyo, imani yangu thabiti na ukweli kuwa mateso makali na udhalilishaji wa utu wa watu ilikuwa ni kumbukumbu ya muda mrefu iliyonisaidia kutokuogopa pale nilipokuwa nikisindikizwa katika viunga vya Maekelawi. Hali ilikuwa vivyohivyo hata kwa marafiki zangu, bila shaka. Kingine ni kuwa, hatukuwa na cha kuogopa, kwa kuwa hatukuwa mashushushu wala wanajeshi. Tulikuwa waandishi tu.

Hata hivyo, mara tu baada ya kuwasili Maekelawi, watu wengine walioshikiliwa walinitaarifu kuwa nimepangwa kwenye moja ya vitengo vyenye utatili mbaya sana wa kituo hiki, kitengo kinachojulikana kama “Siberia”. Kwa kipindi cha chini ya wiki moja, nilijisikia kuwa nilikuwa ninayaishi sawia mambo yaliyoelezwa kwenye Ripoti ya Human Rights Watch iliyokuwa na kichwa cha habari, “Wanahitaji Kukiri”.

“Wanahitaji Kukiri” inaelezea matukio mabaya ana ya uvunjifu wa haki za binadamu, mbinu sisizo za kisheria za mahojiano, pamoja na mazingira mabaya ya kituo cha kushikilia wahalifu cha Maekelawi kilichopo jijini Adis Ababa, matukio yaliyopatikana kwa kufanya mahojiano na watu waliokuwa wameshikiliwa Maekelawi pamoja na ndugu wa familia zao. dWaliokuwa wanashikiliwa Maekelawi ni pamoja na wanasiasa wa upinzani, waandishi wa habari, waratibu wa maandamano na wale wanaodhaniwa kuwa ni watu wanaounga mkono vitendo vya ugaidi.

Befeqadu alielezea njia za mahojiano huko Maekelawi ni zaidi ya”kutawaliwa na kujishusha kuliko kujiamini na ubunifu.”

“Kama watashindwa kupata taarifa kutoka kwako kulingana na matarajio yako, wanalazimisha mtu akiri kwa kupigwa ngumi, kuchapwa, kumpatia mtu mazoezi ya muda mrefu sana, anaandika. “Niliongea pia na baadhi ya watu waliokuwa wameshikiliwa na ambao walikabiliana na mambo mabaya sana ambayo dhahiri yalikiuka uhuru wao wa faragha. Baadhi ya washikiliwa walilazimishwa kuvua nguo zote na kuamrishwa kusimama au kusimama na kuchuchumaa hadi kulipokucha.”

Aliendelea kuelezea namna yeye na wenzake walivyolazimishwa kukiri[makosa]:

Kwenye shauri letu, hatimaye tulilazimishwa kukiri makosa yetu. Tulikiri kutokana na nguvu kali iliyotumiwa. Hatukuweza kuvumilia ukatili na kuathiriwa vikali kisaikolojia. Tuliishia kuwaeleza kile walichohitaji kukisikia kutoka kwetu. Kwa faida yao, tuliongeza maneno ya kuonesha makosa yetu kwa kadiri ya ilivyowezekana. Hata hivyo, misemo kama vile “ndio, tulitaka kuhamasisha machafuko”, haikuwabariki kabisa. Kwa hiyo waliandika upya maelezo yetu ili yaendane na matakwa yao. Baadhi yetu tulijaribu kutoa maelezo na wengine walijaribu kuvumilia vipigo. Hatimaye, tulisaliti amri(isipokuwa Abel ambaye kwa wakati huo aligoma kabisa) na kuweka saini kurasa za maelezo zilizoandaliwa kwa umahiri mkubwa. Alivumilia mateso yote tangu awali, na maelezo yake ambayo hatimaye aliyoyatoa, hayakuwa na ukweli wowote wa kuthibitisha lolote kuhusu sisi.

Kwa sasa tunafahamu kuwa mateso ni sehemu ya sherehe ya Maekelawi inayotumiwa kufichua “ukweli” wa makosa aliyotuhumiwa nayo mtu. Kwa kipindi kirefu nilikuwa nikifahamu kuwa mahojiano ya kipolisi ni mchakato mrefu unaohusisha weledi, maarifa na mbinu za kisaikolojia katika kubaini ukweli. Kwa sasa nimeelwa kuwa mahojino ya polisi huko Maekelawi hayapo hivi. Kwanza, polisi wa Maekelawi wapo kawaida kabisa. Wao ni kama mashine zinazowajengea makosa watu watuhumiwa.

Kwa Maekelawi, msingi mkuu wa mahojiano ya kipolisi ni kuwa una makosa hadi pale itakapothibitishwa vinginevyo. Unataka kuonesha kuwa huna hatia – au kuomba kutoa ufafanuzi – hakuna anayekusikiliza hasilani.

Befeqadu na wenzake walishikiliwa gerezani kwa miezi 18 kwenye magereza nchini Ethiopia kabla ya kuachiwa huru mapema mwezi Oktoba 2015. Yeye pamoja na wenzake walionekana hawakuwa na hatia bila hata ya kupelekwa mahakamani.

Wanablogu wa Zone9 wakifurahia mara baada ya kuachiwa kwa Befeqadu Hailu (wa pili kutoka kushoto aliyevaa skafu) mapema mwezi Oktoba 2015. Picha ilichapishwa Twitter na Zelalem Kiberet.

Pia Befeqadu alielezea maelezo aliyoyasikia kutoka kwa wafungwa wenzake, ambao waliletwa Maekelawi ambao walipitia mateso mengine makali walipokuwa kwenye vituo vingine vya kushikilia watuhumiwa nchini Ethiopia. “Wahikiliwa hawa walikabiliana na vitendo vibaya sana na vya kidhalimu kama vile kung'olewa kucha, kupigwa, na kufunikwa vichwa,” aliandika.

Taarifa zilizopatikana kwa watu wanaoshikiliwa kutoka kwenye vituo vya kushikilia visivyofahamika huhakikiwa kwa kukabiliana na mahojiano zaidi kwenye kituo cha kushikilia cha awali cha Kusikiliza maishauri. watu waliokuwa wanashikiliwa hawakuwa wanafahamu wapi wanapelekwa kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kikatili wa namna hii kwa kuwa wakati wote nyuso zao zilikuwa zinafunikwa. Vituo vya kushikiliwa watu visivyofahamika ni kama vile mashimo meusi.

Akirejelea uvunjwaji wa haki za binadamu chini ya Serikali ya Kijeshi, ambayo serikali ya Ethiopia kwa sasa inajitahidi kuepukana nayo, Befeqadu alifananisha uzoefu huu na kipindi kilichopita.

“Imefahamika kwamba hofu ya wafungwa nchini Ethiopia, kitu ambacho kilishakaribia kufutika kwenye kumbukumbu za watu, kumbe ni nkumbukumbu iliyokaribu kabisa” anasema.

Akitolea ufafanuzi kuhusu habari ya wiki hii, Befeqadu aliandika kwenye Twitter:

Befeqadu na wenzake wawili Atnaf na Natnael hawapo huru moja kwa moja. Pamoja na kuwa makosa yao ya ugaidi yalifutwa, bado wanasubiria maamuzi kwenye mashtaka yao mengine, ambayo yote yalitokana ukosoaji wao wa serikali kwa njia ya amani

Soma zaidi:

  • Maelezo halisi ya Befeqadu kuhusu mambo aliyokabiliana nayo alipokuwa ameshikiliwa Maekelawi

  • Ufuatiliaji wa Kina wa Global Voices kuhusu kesi ya wanablogu wa Zone9

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.