Jiandikishe Sasa kwa Mkutano Mkuu wa Global Voices 2017: Desemba 2-3 Jijini Colombo, Sri Lanka!

Colombo, Sri Lanka. PICHA: Amila Tennakoon (CC BY 2.0)

Mkutano Mkuu wa Global Voices 2017 uko wazi kwa ajili ya kujiandikisha!

Tutakuwa tukikutana mwaka huu jijini Colombo, Sri Lanka mnamo Desemba 2-3 kujadili mabadiliko ya hali ya mtandao huru, harakati huru za kiraia mtandao na haki za binadamu katika zama za kidijitali. Katika vipindi, majopo, na midahalo, tutaangazia masuala kama upotoshwaji wa taarifa, kudhibitiwa kwa mtandao, matishio ya kisheria dhidi ya wanablogu na wanaharakati -changamoto hizi zinazochangia kuharibu au kujenga mustakabali wa mtandao wa intaneti.

Watakaoungana nasi watakuwa ni wanajamii na mashirika yanayohusika kwa karibu na historia na mustakabali wa mtandao huru wa intaneti, duniani kote au kwa maeneo husika, ikiwa ni pamoja na Creative Commons, Mozilla, Wikipedia, Web Foundation, Association of Progressive Communications, IFEX, MIT Media Lab, Digital Asia Hub, yote hayo yakitanguliwa na utamaduni wa intaneti nchini Sri Lanka, pamoja na wengi wengineo.

Mkutano utafanyikia TRACE Expert City, kituo cha teknolojia kilichopo kwenye wilaya ya Maradana jijini Colombo.

Tembelea ukurasa wetu wa kujiandikisha ili kujiwekea nafasi kwenye ratiba ya Mkutano Mkuu wa Global Voices 2017, na endelea kuchungulia tovuti ya Mkutano kwa majuma machache yajayo kadri tunavyoendelea kuweka ratiba kamili ya Mkutano na habari, sauti na mahojiano.

Tutaonana nawe Desemba!

Mkutano Mkuu wa Uandishi wa Kiraia wa Global Voices 2017 umewezeshwa na Ford Foundation, MozillaMacArthur Foundation na Groundviews/Centre for Policy Alternatives.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.