Katika wakati ambao karibu kila habari kuhusu Puerto Rico kwenye vyombo vikuu vya habari inahusiana zaidi na kudorora kwa uchumi na ukosefu wa fedha kisiwani humo, wingi vya vichwa hasi vya habari vinavyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaweza kumchosha mtu.
Ni dhahiri katika nyakati kama hizi, ndipo uandishi wa mizaha huchukua nafasi yake na kufanya wajibu muhimu wa kuwasaidia watu kuelewa habari, au badala yake, namna gani habari habari kutengenezwa.
The Juice Media, ukurasa wa Facebook ambao hujikita kwenye habari za mizaha, ulitengeneza video inayohusiana na kile wanachoamini ni mzizi wa matatizo na changamoto nyingi za Puerto Rico: Ukoloni wa Marekani.
Ikiwa imesambazwa mno kwenye mtandao wa Facebook, watengenezaji wake walitiwa moyo kutengeneza kipande baada ya mafanikio ya video kama hiyo kuhusu Hawai'i katika mfululizo wao wa “Matangazo ya Uaminifu Yatolewayo na Serikali”.
Video hiyo inatoa muhtasari wa baadhi ya njia ambazo serikali ya Marekani imekuwa ikizitumia kihistoria kuinyonya Puerto Rico, kuanzia kwenye kuituia nchi hiyo kama eneo la kujaribishia mabomu kwa miongo kadhaa, mpaka kuwafunga kizazi zaidi ya theluthi ya wanawake wa Puerto Rican bila wao kujua au kuwaomba ridhaa katikati ya karne ya kumi na mbili.
Mtangazaji wa kipande hicho mwenye bashasha anaanza kwa kusema:
Kwa bahati nzuri, hata hivyo, wachache wanafahamu Puerto Rico ya kwenye, koloni la Marekani tangu 1898 baada ya kuwanyang'anya wa-Hispania […] ambao nao waliliiba kutoka Taino […] na kuwafanya raia wa Puerto Rico kuwa raia wa Marekani —raia daraja la pili hata hivyo… [kwa sababu] pamoja na kupigana kila vita yetu bado hawawezi kuchagua Rais na hawana uwakilishi kwenye Baraza la Kongresi. Kwa maneno mengine, raia wa Marekani ambao wametufanyia kila ujinga wana kauli kuptia sheria ambazo Serikali ya Marekani inawatungia…
Video hii inaweza kutazamwa kikamilifu hapa chini: