Maandamano na Tuhuma za Udanganyifu Vyafuatia Uchaguzi wa Rais wa Ecuador

Bandera del Ecuador. Foto de Yamil Salinas Martínez en Flickr. Usada bajo licencia CC 2.0

bendera ya Ecuador. Picha na Yamil Salinas Martínez kutoka Flickr. Imetumika kulingana na leseni ya CC 2.0.

Daniela Gallardo aliandika makala hii kwa lugha ya Kihispania. Tafsiri ya lugha ya Kiswahili hapa chini imesahihishwa na kuboreshwa.

Kufuatia kampeni za nguvu za wagombea Guillermo Lasso na Lenin Moreno, ndiye aliyetangazwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho cha urais nchini Ecuador hapo Aprili 2 mwaka huu. Hata hivyo, upinzani na wafuasi wa Lasso wanalalamikia udanganyifu katika matokeo na wanaitisha maandamano ya kutaka kura kuhesabiwa tena.

Hesabu iliyotolewa kiofisi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilikuwa ni 51.16% kwa Moreno na 48.84% kwa Lasso.

Siku zilizofuata baada ya uchaguzi limeonekana wimbi kubwa la maandamano, yakiwa na hashtagi za #Megafraude (Udanganyifu-mkuu) na #LicenciadoMoreno (“Muhitimu” Moreno, jina la kawaida analoitwa mtu mwenye shahada au digrii) kuchorea mstari ukweli kwamba watu hawataki kumuita “Rais Mteule”:

Baadhi ya wananchi wa Ecuador wameingia mitaani kuandamana ili sauti zao zisikike

Kampeni hizi zimeibua mgawanyiko mkubwa baina ya wapiga kura, kati ya wale wanaomuona mgombea wa chama Tawala Lenin Moreno kama muendelezo wa ajenda ya siasa za ujamaa ambazo hadi karibuni zilikuwa zinaongozwa na Rais Rafael Correa, na hao wanaoona mgombea wa chama cha CREO Guillermo Lasso kama muwakilishi wa mikakati bora ya mabadiliko yakiambatana na uchumi wa kihafidhina.

Lisette Arévalo Gross na Sol Borja, mchambuzi kutoka katika vyombo vya habari vya Ecuador; GkillCity, ameelezea jinsi kila mgombea anavyotoshea katika muktadha wa majibizano ya kisiasa na pia hofu waliyonayo wa-Ecuador wengi kuhusu uhuru wa kujieleza na kudumisha demokrasia. Kuhusu hao waliompigia kura Lasso, Arévalo Gross alisema:

Hay mucha gente que está de acuerdo con Guillermo Lasso de que al Ecuador hay que salvarlo. Esa es la razón por la que van a votar por él, lo apoyan y siguen. Incluso hay quienes no lo apoyan, ni lo siguen, pero votaron por él en primera vuelta por la simple y sencilla razón de que Guillermo Lasso era el más opcionado para llegar —como en efecto llegó— a una segunda vuelta con Lenín Moreno, el candidato que corre por Alianza País, el partido de gobierno.

Watu wengi wanakubaliana na Lasso kuwa Ecuador inahitaji kuokolewa. Ndiyo maana wanaenda kumpigia kura, kumfuata na kumuunga mkono. Pamoja na hao wasio muunga mkono au kumfuata, lakini walimpigia kura katika mzunguko wa kwanza kwa mtazamo wa kuwa Guillermo Lasso ni rahisi kumfikia – hakika kama ilivyokuwa katika mzunguko wa pili na Lenin Moreno anayegombea kupitia chama cha serikali, Alianza País.

Na kuhusu Lenin Moreno, Borja alidokeza:

[Lenin Moreno] Ha sido presentado como la cara buena de un fenómeno político liderado por un personaje de carácter explosivo, intolerante e impulsivo […] La idea de que Moreno es un patriota es repetida por sus seguidores y pulida por su equipo de campaña. Hay un cerco estricto que hace muy difícil llegar a él y verlo fuera de la imagen heroica que presentan sus asesores.

[Lenin Moreno] Amekuwa akioneshwa kwa uso wa kisiasa wenye urafiki unaoongozwa kwa utata, kutokuvumiliana na tabia zisizovumilika. Kauli kwamba Moreno ni mzalendo zinaelezwa na wafuasi wake na kupendezeshwa na timu yake ya kampeni. Kuna ukuta usiopenyeka unaofanya iwe vigumu kumtoa nje ya picha ya kishujaa inayotengenezwa na washauri wake.

Wengine wanamuona Lasso kama Muhafidhina sana kiasi cha kutokuweza kupenya hadi kwenye kitovu cha siasa na kupata kura, ambazo zingebadilisha matokeo.

Lasso hakutaka kumfurahisha yeyote… Kama jamii tusingekuwa wazito dhidi ya serikali ya wala rushwa katika historia…

Siku ya kupiga kura kulikuwa na vikwazo vingi. Malalamiko juu ya vituo vya kupigia kura yalizunguka katika mitandao ya kijamii na mashirika kama vile Usuarios Digitales (Watumiaji wa kidigitali), ambayo yalifuata mwenendo wa wananchi mtandaoni, walilaumiwa kwa kucheza mchezo mchafu kwa kutoa taarifa ambazo hazikuwa nzuri kwa wagombea ambao walikuwa karibu na serikali.

#KiashiriochaKidigitaliEC: Tovuti kwa ajili ya kufuatilia uchaguzi kutoka chama cha siasa cha CREO kwa sasa imezimwa. Huenda kuna shambulio la DDoS

Kuna mlinganisho uliofanywa kwa hali za kisiasa za maeneo mengine ya ukanda wa Ulatini ya Amerika. Kwa wengi, kuibuka kwa Moreno ni muendelezo wa ajenda sawa na mikakati ya kisiasa na uchumi ilivyoonekana huko Venezuela, ambayo imekuwa katikati ya malumbano makali kutokana na mgogoro wake wa kisiasa na kiuchumi.

Ninatumaini kuwa kilichotokea Venezuela ni mfano kwa Ecuador, kwamba kura itakuwa ni mrudio wa HAPANA kwa Ujamaa wa Kidikteta katika karne ya 21 #EcuadorImechagua2017

Vilevile, madai haya ya udanganyifu yalirudisha mashitaka yaliyofanywa wakati wa Venezuela's 2013 uchaguzi baina ya Nicolás Maduro, Rais wa sasa wa Venezuela na Henrique Capriles, mpinzani wake muhimu:

Kitu kile kile kilichotokea Venezuela Aprili 2013 ndicho kinachotokea Ecuador kwa sasa. Capriles alishinda lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikatangaza kuwa Maduro aliongoza kwa asilimia 1 %. Udanganyifu

Hapa Ecuador wanachofanya kwa #GuillermoLasso ni kama alivyofanyiwa Capriles huko #Venezuela. Hapana kwa UDANGINYIFU! #LassoRais

Lasso alitangaza kuwa ataitisha kura zihesabiwe upya na atakubaliana na matokeo hata kama atakuwa ameshindwa “kwa kura moja”.

Katika kuangalia mgawanyiko wa nchi pasi na makosa, wengine walihitimisha hivi:

Kugawanya nchi katika pande mbili zisizopatana kwa 50% : Hayo ndiyo mafanikio makubwa ya Rafael Correa Delgado.

Hiki ndicho tulichokuwa tunahitaji katika mgogoro wa kisiasa na kiuchumi, Rais ambaye uhalali wa kuchaguliwa kwake una walakini. Shikilieni hapo hapo!

Zaidi ya malalamiko ya udanganyifu au msemo wa kuongezeka kwa mamlaka ya chama cha siasa, wasiwasi na mvutano juu ya rushwa vikwazo dhidi ya uhuru wa kujieleza vinaendelea.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.