Kutana na Nabii Nchini Afrika Kusini Anayetumia Sumu ya Wadudu Kuponya

Image shared widely on social media. This one was shared by @Mission316Show.

Picha imesambazwa mno kwenye mitandao ya kijamii. Picha hii ilitumwa na @Mission316Show.

Mtu anayejitangaza kuwa nabii, Lethebo Rabalago, amewashtua wa-Afrika Kusini wengi baada ya habari kuenea kuwa anatumia sumu ya wadudu iitwayo Doom, kuponya. Anawanyunyuzia waumini wa kanisa lake sumu hiyo kwenye miili yao na hata kwenye nyuso zao.

Akitangaza nguvu za ‘uponyaji’ zilizoko kwenye sumu hiyo ya Doom, Rabalago aliandika kwenye ukurasa wa Facebook:

Kwa jina langu, mtayatoa mapepo.
Kwa jina nagu, mtashika nyoka. Kila mtakachokishika, kitapata kibali kwa sababu ya upako juu yenu. Sumu ya Doom ni jina tu, lakini unapoisemea maneno inageuka kuwa bidhaa ya kuponyesha. Watu wanaponywa na kufunguliwa kwa kutumia doom. Si kwa uweza wala nguvu, lakini kwa Roho Mtakatifu. Tunampa Mungu utukufu!!

Kampuni inayozalisha sumu hiyo ya wadudu imemshutumu Rabalago na inasema  iko kwenye mchakato wa kuwasiliana nae kumuonya kuhusu hatari ya kunyunyuzia sumu ya wadudu ya Doom kwenye nyuso za watu.

Mtandao wa intaneti umeitikia tukio hil kwa hasira, kutokuamini na hata kutengeneza ujumbe wa vichekesho kwa kutumia alama ishara ya #ProphetOfDoom [Nabii wa Doom].

Mtumiaji wa twita anayetumia jina ‘Sound Surgeon’ jalitania:

Habari Mpya: Bei ya Doom imepanda

Iloveza aliweka picha hii ikionesha makabati ya kuhifadhia Doom madukani:

Biashara [ya Doom] inakwenda vizuri

Mphuma alitaja vitendo vingine vya ajabu vinavyofanywa na manabii hawa wanaojitangaza kila siku nchini Afrika Kusini:

Pale unapofikiri umesikia vya kutosha, mara wachungaji wa [kunywesha] petroli, [kulisha] majani, nyoka na kadhalika…linatokea jingine jipya. Dunia inaisha.

Matendo ya ajabu ya “kinabii” yanayofanywa na wahubiri wa Afrika Kusini katika miaka ya hivi karibuni ni pamoja na kula majani, nyoka and kunywa petroli, ambayo inadaiwa hubadilika kuwa juisi ya nanasi baada ya maombi.

Kwa kuzingatia “muujiza” wa hivi karibuni zaidi, Ditjhaba alisema Afrika Kusini inahitaji likizi kidogo:

Nadhani tunahitaji likizo kama taifa. Hali imezidi kiwango na huyu nabii wa Doom amekomesha kabisa

@shandu009 alitwiti picha ya mtu anayejaribu kuongeza utajiri wake kwenye mashine ya ATM kwa kutumia ushauri wa mchungaji:

Mtumiaji mwingine wa Twita alisema:

Doom ni jibu mabibi na mabwana hebu tuinamishe vichwa tuombe

Vhoni alitania:

Nani anahitaji kwenda kufanya mazoezi wakati kuna Doom?

Mtu mmoja wa Zimbabwe aliweka picha ifuatayo akishauri kuwa rais wa Zimbabwe anahitaji “uponyaji maalumu wa Doom”:

Ninaachana na suala hili hapa…

Qamatha aliweka picha ya basi ndogo ikiwa na tangazo la Dom akidai linamilikiwa na kanisa hilo:

Nabii wa Doom amenunua kibasi kipya kwa ajili ya waumini wake

Video ifuatayo inamwonesha nabii akifanya vitu vyake:

Mjasiriamali wa mtandao nchini Afrika Kusini Peter Mansfield alishauri:

MFUNGENI, na wapelekeni waumini wake kwenye matibabu ya akili kujua kwa wamekuwa wajinga kiasi cha kumwamini

Mtumiaji mwingine wa mtandao wa Twita alinukuu kifungu cha biblia kwenye kitabu cha Yohana 3:16. Kifungu hiki kinasomeka: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanae wa pekee, ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” :

Hivi kuna mtu anaweza kuona siku ya mwisho ikikaribia au bado mnafikiri itakuja ghafla…

Celeste alifikiri kuwanyunyuzia watu dawa hatari ni kosa la kujaribu kuua:

Huyu nabii wa Doom akamatwe kwa kujaribu kukua. Doom inatumika kuua kwa hiyo wanaohusika wafunge washtaka

Kw akutumia picha ya uelimishaji wa mtandaoni nchini Ghana, Jake Amo, Barry Roux aliandika:

Mpendwa Nabii wa Dom, nisamehe kwa mwandiko mbaya, naandika kuuliza kama Doom inaweza kumponya TB Joshua

TB Joshua ni mhubiri wa ki-Naijeria anafahamika kwa kutoa matamshi ya kutabiri. Wakati wa uchaguzi wa Marekani alitabiri kuwa Hillary Clinton angeshinda uchaguzi huo.

Kalabash Media alitumia picha ifuatayo:

Umeishiwa mafuta?? Tumia Doom

Rabalago amedai kuwa kwa kutumia nguvu zake za kiroho anaweza kupiga simu bila kutumia kadi ya mawasiliano ya simu [sim card] au hata kuendesha gari bila mafuta.

Mwsiho, unahitaji chupa moja ya Doom ya uponyaji? :

Dawa ya uponyaji unauzwa, wasiliana na Nabii wa doom, Lethebo Rabalago wa Kanisa la Ufalme wa Doom kwa mawasiliano zaidi.

***Katika Kiingereza, Prophet of Doom inaanisha Nabii wa Uongo. Matumizi ya sumu ya Doom yanafanya nabii huyu afahamike kama Nabii wa ‘Doom’, ambayo inaleta maana ya Nabii wa Uongo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.