Shirika la Umoja wa Mataifa linashughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO),Shirika la Ujerumani la Ushirikiano wa Kimataifa na Shirika la Kiingereza la Haki za Binadamu Ibara ya 19 wametengeneza video ya katuni iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube kuhusu Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu na raia.
Ikiwa jijini Arusha, Tanzania, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Raia ni mahakama ya bara zima iliyoanzishwa na nchi za Afrika kwa lengo la kulinda haki barani humo. Mahakama hiyo inafanya kazi bega kwa bega na Tume ya Afrika inayoshughulikia Haki za Binadamu na Raia. Wakati Tume ya Afrika ikiishia kutoa mapendekezo, Mahakama hiyo hufanya maamuzi.
Mahakama hiyo ilianzishwa chini ya Itifaki ya Makubaliano ya Afrika kwa Haki za Binadamu na Raia kuanzisha Mahakama ya Afrika kwa Haki za Binadamu na Raia. Kwa mujibu wa video hiyo, mpaka Septemba 2016, nchi 30 tu zimekubaliana na Makubaliano hayo.
Video hiyo inaonesha kuwa Mahakama hiyo tayari imefanya maamuzi makubwa mawili yanayohusiana na uhuru wa kujieleza barani Afrika. Mwaka 2014, Mahakama iliamua kuwa kufungwa kwa kosa la kumchafua mtu mwingine ni kinyume cha haki ya uhuru wa maoni. Mwaka huo huo, Mahakama iliagiza kufunguliwa upya kwa uchunguzi wa mauaji ya mwandishi wa habari za uchunguzi na mchapishaji raia wa Burkina Faso Norbert Zongo.
Msanii alitengeneza katuni hii ni m-Venezuela anayeitwa Juan Carlos Hernández Ramirez.