Pamoja na Kutokupata medali hata moja, Nepali ina kila sababu ya kujivunia

The Olympic Village #Río2016. Image from Flickr by Mexican Olympic Committee. CC BY NC-ND-2.0

Kijiji cha Olympic #Río2016. Picha kutoka Flickr kwa hisani ya Kamati ya Mexico ya Mashindano ya Olympic. CC BY NC-ND-2.0


Wachezaji wa Nepal hadi sasa hawajapata medali hata moja kwenye mashindano ya Olimpiki ya Rio, lakini hata hivyo, raia wa Nepali hata hivyo, wana kila sababu ya kujivunia, shukrani kwa vyombo vya habari kwa kuupa nafasi wimbo wa Taifa pamoja na kumtambua mwogeleaji mdogo aliyeonesha umahiri mkubwa.

Mwanamichezo mdogo kuliko wote kwenye mashidnano ya Olimpiki ya Rio, Gaurika Singh, ni raia kutoka Nepal. Alikuwa na umri wa miaka 13 na siku 255 wakati aliposhindana kwenye mbio za mita 100 za kuogelea kimgongo mgongo kwenye mzunguko wa awali.

Pamoja na kuwa hakuweza kufika fainali na pia kuvunja rekodi ya kitaifa aliyokuwa ameipania — aliwashinda waogeleaji wengine wawili kwenye mzunguko wa awali alipokuwa akishindana nao.

Gaurika Singh at Women's 100m backstroke Heat. Image by Al Bello, Getty Images. Used with permission from the Brazilian Olympic Committee.

Gaurika Singh kwenye mbio za mita 100 za awali za kuogelea kinyumenyume. Picha na Al Bello, Picha za Getty. Ilitumiwa kwa ruhusa kutoka Kamati ya Olimpiki ya Brazili.

Kwa kuongeza furaha ya raia wa Nepal, ulikuwa ni uamuzi wa kituo cha utangazaji cha BBC wa kujumuisha wimbo wa Taifa la Nepal kwenye safu yake ya nyimbo za taifa bora kabisa kwenye mashindano ya Olimpiki ya mwaka huu.

Urusi ilikuwa ya kwanza, ikifuatiwa na Myanmar halafu Nepal.

Ukiwa umeandikwa na mshairi Pradeep Rai, aliyejulikana pia kama Byakul Maila, na kutungwa na hayati Amber Gurung, wimbo huu ulirasimishwa rasmi kama wimbo wa Taifa la Nepali mnamo Agosti 3, 2007.

Kama bado hujausikiliza, huu hapa ndio wimbo mzuri wa kujivunia umoja na uhuru wa Nepali.

Na hii ni tafsiri ya Kiingereza ya wimbo wa Taifa la Nepali iliyofanywa na Sushma Joshi.

Mamia ya mashada ya maua, sisi ni shada moja la raia wa Nepali.
Uhuru, umeenea kutoka Mechi hadi Mahakali.
Rasilimali zimeenea kila mahali, hazihesabiki
Damu za mashujaa zimetufanya kuwa huru, hawasahauliki.
Nchi ya maarifa, nchi ya amani— Tarai, Pahad, Himal
Isiyogawanyika, ipendwayo, nchi yetu ya asili Nepali.
Taifa tukufu la makabila mengi, lugha, Imani na tamaduni
Taifa letu endelevu, ishi maisha marefu, ishi maisha marefu nepali.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.