Inaonekana,kwa kiasi fulani, nchi ya Japan ina mapenzi na kapibara, wanyama wakubwa wenye sura kama ya panya buku wanaopenda kuogolea kwenye maji ya moto.
Kwa mfano, chaneli ya YouTube “ukurasa wa wapenzi wa kapibara” ina wafuatiliaji wapatao 6,000 na imetazamwa mara milioni sita. Chaneli hiyo ya YouTube ina lenga nini? “Kupata picha nzuri zaidi za video za kapibara kadri inavyowezekana.”
Video ya “namna ya kuwasugua kapibara” imetazamwa mara milioni 1.2:
Kadhalika, kuna tovuti ya Ninawapenda Kapibara (カピバラ大好き), maalum kwa ajili ya wanyama hao. Kuna blogu, chaneli ya YouTube na Akaunti ya Twita, lakini mabandiko mengi hufanyika kwenye ukurasa wa Facebook wenye wafuasi 33,000 na huwekwa habari mpya mara kwa mara.
Kivutio kikuu cha tovuti hiyo ni “ramani ya kapibara” inaonesha wapi unaweza kumpata mnyama huyo mwenye sura kama panya buku kote nchini Japani.
Akaunti ya ukurasa wa Twita ina picha nyingine:
レオマリゾートのカピバラ達(3頭)も会って来ました。今から飛行機に乗って帰ります。ちゃんとブログに訪問記書きます〜少しブログさぼってたからね。 pic.twitter.com/1hr44JGIPt
— 渡辺克仁◎カピバラ写真家 (@capybarahp) April 27, 2016
Nilikwenda kuwaona kapibara pale kwenye Mgahawa wa Reoma (eneo la Kagawa kwenye kisiwa cha Shikoku), na nitasafiri kwa ndege kurudi nyumbani leo. Nitawapa habari zaidi kwenye blogu yangu.
Video maarufu kwenye chaneli ya YouTube inamwonesha kapibara akirukia kwenye bwawa la kuogelea:
Kapibara wana asili ya Marekani ya Kusini, wanafahamika sana nchini Japani shauri ya katuni mmoja maarufu aitwaye Kapibara-san.
【TRYWORKSより】
カピバラさんが大人気ゲーム「LINEポコパン」とコラボしました!
カピバラさんたちが召喚動物や友だちランキングに登場したり
内容もりだくさん♪
詳細はこちらhttps://t.co/MSX5rqFzkY pic.twitter.com/lJKJqCJ6kt— カピバラさん by TRYWORKS (@FROM_TRYWORKS) May 27, 2016
Kutoka tovuti ya TRYWORKS: Kapibara-san anashirikana na LINE Pokopan katika mchezo mpya mkali! Kapibara-san ni mkali kwa wanyama wote na ni rafiki mwenye mengi ya kuvutia. Habari zaidi hapa: https://t.co/MSX5rqFzkY pic.twitter.com/lJKJqCJ6kt
Mapenzi ya kapibara hayapo Japani pekee.
Umami Dearest, mwanachama wa jumuiya ya mtandaoni ya MetaFilter, ametengeneza mwongozo wa kwenda kwenye migahawa ya wanyama nchini Japani, na tovuti yake ina maelezo ya wapi unaweza kumwona kapibara nchini humo.
Kapibara ni wakubwa kwenye maeneo ya kufugia wanyama #capybara #gianthamster #wetcapybara http://t.co/8Re8C0LM49 pic.twitter.com/1lNZpHtFVC
— Animal Cafes (@AnimalCafes) August 7, 2015
Kapibara ni wakubwa kwenye maeneo ya kufugia wanyama
Kwa wale wanaopenda, Umami Dearest amechapisha baadhi ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu mikahawa ya wanyama nchini Japani.