Yaliyojiri Wiki Hii Global Voices: Yeyote ni Kipaumbele?

Katika toleo hili, mhariri wa Habari wa global Voices, Lauren Finch pamoja na mimi — mhariri Mtendaji wa Global Voices– tunakupeleka hadi China, Mexico, Jamaica, Macedonia na Uganda.

Nchini China, tunakupasha habari kuhusu wakosoaji nchini china waliojawa na hofu kufuatia mtandao wa Twita kumuajiri mwanajeshi mstaafu wa China ili awasaidie kuandaa mpango wa biashara nchini China. Habari hii ilisimuliwa kwa kina na Oiwan Lam.

Pia, tunaelekea nchini Mexico ambapo tutapata habari iliyotayarishwa na mshirika wetu, Sin Embargo, ambapo Mkandarasi wa kutumainiwa wa serikali ya Mexico anaihamisha jamii ya raia wazawa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa barabara kuu. Baadae, tutaangaza huko Jamaica, ambapo mwandishi wetu, Emma Lewis aliandika habari kuhusu wanafunzi katika mgahawa wa Kahawa, Deaf Can! wanaojifunza namna ya kuandaa kahawa na pia kujifunza mambo anuai kuhusu biashara hii. Huko Macedonia, ambapo mitaa yake imefunikwa na waandamanaji wanaodai haki, mshirika wetu Goran Rizaof alitupasha kuhusu habari hii.

Mwisho tunakupeleka nchini Uganda, ambapo raia wakasirishwa na  vipaombele vya serikali yao. mshine pekee ya kutibu kansa kwa kutumia mionzi ya nchini humo iliharibika hivi karibuni. Ilikuwa ikihudumia zaidi ya watu elfu 27 kwa mwaka, lakini kwa sasa, imeshindikana hata kuifanyia matengenezo. mshirika wetu Prudence Nyamishana aungana nasi kutupasha zaidi ni kwa nini Raia wa Uganda wamekasirishwa na kwa nini kifaa cha kiasherati kinavyohusika.

Katika toleo la wiki hii la Global Voices, tulizungumzia muziki iliyo chini ya hati miliki ya Creative Commons kutoka kwenye hifadhi huru ya muziki, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully by Jahzzar; Twitterpated by Floating Spirits; Gladiator by Tommy Tornado; Good Riddance by Ars Sonor; Highway 101 by Josh Spacek; and Sex and Lucia by Gary Lucas.

Shukrani nyingi kwa waandishi wetu, watafsiri, na wahariri wetu waliofanikisha kutoka kwa toleo hili. Tusikilize tena baada ya wiki mbili zijazo panapo majaliwa.

Image in Soundcloud thumbnail: Picha ya Mashine ya kutibu kansa kwa mionzi kwa hisani ya Prof Seegensmiedt. Imetolewa kwa idhini ya Creative Commons.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.