Misri Yamhukumu Rais wa Zamani Morsi Miaka 20 Jela kwa “Utishaji na Matumizi ya Nguvu” Dhidi ya Waandamanaji

A banner which reads: "The revolution continues; Morsi will be back," seen in Giza this morning. Photograph shared on Twitter by @Ikhwanweb, the Twitter account of the Muslim Brotherhood in Egypt

Bango linasomeka: “Mapinduzi yanaendelea; Morsi atarudi,” lilionekana kwenye eneo la Giza asubuhi ya leo. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita na @Ikhwanweb, akaunti ya Twita ya Chama cha Muslim Brotherhood nchini Misri

Misri imemhukumu rais wake wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia Mohammed Morsi kifungo cha miaka 20 jela leo, kwa kukpatwa na “hatia ya utishaji na matumizi ya nguvu kupita kiasi” kwa waandamanaji mwaka 2012. Alihusishwa na mashitaka yanayohisishwa na kuwaua waandamanaji.

Morsi, ambaye ni mwanachama wa chama cha Muslim Brotherhood, alikuwa rais wa Misri kwa mwaka mmoja baada ya mapinduzi, aliyomng'oa Hosni Mubarak, aliyeitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30. Utawala wa Morsi ulikatishwa mwezi Julai 2013, kufuatia maandamano makubwa yaliyodai aondoke madarakani. Kisha, Jeshi la Misri lilitwaa madaraka, chini ya uongozi wa Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi nchini Misri na Waziri wa Ulinzi, Jenerali Abdul Fattah El Sisi, ambaye baadae alichaguliwa kuwa rais mpya wa Misri.

Mwandishi wa habari anayeishi Cairo Bel Trew alitwiti kilichokuwa kikiendelea mahakamani:

Viongozi wa [Muslim] Brotherhood Mohamed El-Beltagy, Essam El-Erian, Abdel-Arty wanatabasamu, wanapunga mikono, wakitoa salamu ya Rabaa wakiwa wamezungukwa na walinzi

Morsi hivi sasa amewekwa mbali kabisa na waandishi akiwa karibu na dawati la jaji, kuna mpiga picha anatafuta namna ya kupata picha yake akiwa amezingirwa na polisi

Viongozi wa [Muslim] Brotherhood waliofungwa na kutengwa na rais aliyepinduliwa wanamnong'oneza kupita ukuta unaozuia sauti kupenya

Anaongeza:

Morsi – na wenzake waliohusishwa na matukio ya mauaji – badala yake wamekutwa na hatia ya kutisha watu na matumizi ya nguvu kupita kiasi

Kwa ajili ya Farao Mkuu, imani ya Morsi lazima iwe somo kwa wale walio madarakani leo. Anaongeza:

Miaka miwili iliyopita, [Chama cha] Muslim Brotherhood kilikuwa kinatawala, kikituma wanajeshi kushambulia watu waliokuwa wakiandamana kwa kukaa. Kinachotokea hivi sasa lazima kiwe somo kwa wanaounga mkono ukovunjifu wa haki unaofanywa na utawala uliopo madarakani

Anaongeza:

Kila hukumu ya mahakama haina uhusiano na haki, ni mwendelezo wa visasi na vita kati ya makundi mawili

And continues:

Tamer El-Ghobashy alikuwa na wasiwasi na mfumo wa mahakama wa Misri. Anasema:

Mahakama za Misri zimefanya ukweli uonekane hauna maana. Haiwezekani kuona mashitaka yoyote yakiendeshwa kwa kitu kinachofanana na haki

Wasiwasi huo huo unaonekana kwa Tweet Palestine, anayesema:

Kwa hiyo, Mubarak anakuwa huru baada ya miaka 30 ya udikteta na Morsi anafungwa gerezani miaka 20. Ujinga wa namna gani katika mahakama za Misri zisizo na haki

Hata hivyo, inavyoonekana, hukumu hii si mwisho wa mambo kwa Morsi, kwa sababu shauri hilo linaendelea. Mwandishi wa habari Hafsa Halawa anatwiti:

Kumbuka mashitaka makubwa zaidi ya udukuzi na kuvunja mahakama bado yatafunguliwa

Jiandae kusikia mengi kadri mashitaka ya Morsi yanavyoendelea kwenye mahakama za Misri.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.