Walidanganya Mpaka Amefariki: Serikali ya Zambia Yakiri Ugonjwa wa Rais Mauti Yalipomkaribia

Zambia's Supreme Court reserves ruling in presidential petition case, February 17, 2009, photo by Harrison Tuntu. Lusaka, Zambia. Demotix.

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Zambia kwa Kesi ya Kulalamikia matokeo ya Urais wa Rais, Februari 17, 2009, picha na Harrison Tuntu. Lusaka, Zambia. Demotix.

Wakiwa gizani wasijue maradhi yanayomsibu kiongozi wao, wa-Zambia walipatwa na hasira na kushangazwa na habari zilizotolewa na serikali juma hili kwamba rais wa tano wa nchi hiyo, Michael Sata, anayefahamika kwa jina la King Cobra, alikuwa ameaga dunia jijini London mnamo Oktoba 28.

Serikali ilikiri hivi majuzi kwamba rais alikuwa mgonjwa, habari zilizotolewa Oktoba 20, siku nne kabla ya sherehe za Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia, ambapo Sata alikuwa amesafirishwa kwenda Uingereza kwa ajili ya matibabu ya dharura. Wakati huo, ikulu ya rais ilieleza kirahisi:

Mheshimiwa Michael Chilufya Sata, Rais wa Jamhuri ya Zambia, usiku wa jana aliondoka nchini kwa ajili ya kuchunguza afya yake ng'ambo […] mke wa rais Dk Christine Kaseba, baadhi ya wanafamilia na msaidizi wake wa hotuba wameongozana na Mkuu wa Nchi.

Hii haikuwa ziara ya kwanza ya Rais nje ya nchi kukutana na madaktari wa kigeni. lakini ilikuwa ni mara ya kwanza kwa maafisa wa serikali kukiri kwamba Rais alikuwa anapata matibabu. Awali, serikali ilikanusha tetesi zilizokuwa zikienezwa na baadhi ya mawaziri kuhusiana na kuzorota kwa afya yake, ikisema kwamba Sata alikuwa imara na akiendelea na kazi. Mapema mwaka hu, serikali iliwaambia waandishi wa habari kwamba Sata alikuwa kwenye mapumziko ya kikazi nchini Israel, ingawa vyombo vya habari vya Israeli baadae viliandika kwamba alikuwa kule kupata matibabu.

Kazi iliyokuwa ikifanywa na Idara ya Mahusiano ya umma ya serikali ya Zambia haikupita hivi hivi. Kwenye mtandao wa Facebook, B.M. Jermaine Sikombe alinukuu tamko lisiloeleweka lililotolewa na ikulu ya rais kutangaza kifo cha rais. Sikombe aligeuza geuza maneno, na kutoa wito kwa maafisa wa serikali kuwajibika kwa kuudanganya umma. 

KAMA MNAVYOFAHAMU, MHESHIMIWA MICHAEL CHILUFYA SATA, RAIS WA JAMHURI YA ZAMBIA AMEKUWA AKIPATA MATIBABU JIJINI LONDON, UINGEREZA

AMEONDOKA ZAMBIA AKIWA NA MKE WA RAIS NA WANAFAMILIA WENGINE MNAMO OKTOBA 20, 2014.

HATA HIVYO, NINA HUZUNI KUBWA KWA KUZUNGUMZA NANYI LEO, KULITAARIFU TAIFA KWAMBA RAIS WETU KIPENZI, MHESHIMIWA MICHAEL CHILUFYA SATA AMETUTOKA.

Sikombe anaandika:

Kisha mtu asiye na hisia yoyote na katika tamko lisilopangiliwa vizuri anaanza tamko ….hivi “KAMA MNAVYOFAHAMU, MHESHIMIWA RAIS MICHAEL CHILUFYA SATA,…..”.

tulijua nini na nani alituambia yuko London –jamani si tuache ujinga?

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Emmanuel Mwamba, msemaji wa zamani wa rais wa pili wa Zambia marehemu Frederick Chiluba, aliandika:

Wa-Zambia waliposumbuliwa na picha mbaya za Rais aliyeonekana wazi ni mdhoofu mwezi Aprili 2014, zilizoibua hisia za wasiwasi na mashaka, maafisa wa serikali hawakuonesha kujali.

Waziri wa Mambo ya Nje Harry Kalaba mara kwa mara alitoa matamko ya kijinga kwenye kituo cha Radio Phoenix kama vile “Viongozi wa upinzani wanaohoji afya ya rais Sata wanaongozwa na chuki”. “Sata atawashinda maadui zake wanaotamani apoteza maisha”, “Rais Sata anafurahia afya yake imara”.

Kilicholeta wasiwazi ni namna Rais Sata alivyozungushwa nchi mbali mbali, Afrika Kusini, India, Uingereza na Israeli kwa usiri mkubwa na hali ya dharura.

Hivi karibuni lilizizima pale rais sata alipofungua mkutano wa nne wa Bunge mnamo Septemba 19, 2014.Alionekana kuudhoofu sana.

Sata alitoweka hadharani mwezi Juni, baada ya kukutana na ujumbe wa maafisa wa China. Alionekana tena kidogo wakati wa kufungua mkutano wa bunge wa 2014-2015, ambapo alishindwa kusoma hotuba iliyoandaliwa. Baadae alisafiri kwenda New York kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, lakini alishindwa kuonekana wakati aliopangiwa kuhutubia ulipofika.

Matamko ya maafisa wa Zambia yalipotosha ukweli kuhusu afya ya Levy Mwanawasa, rais wa tatu wa nchi hiyo, alipoteza maisha akiwa madarakani kwa kiharusi mwaka 2008. Wakati Mwanawasa akiwa amelazwa hospitali, makamu wake Lupando Mwape, aliwaambia waandishi wa habari kwamba rais walikuwa anafanya mazoezi ya viungo jijini London.

Mwez Juni 2008, Rais Mwanawasa alianguka akiwa kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika nchini Misri. Aliwahishwa Ufaransa, ambako alifariki dunia majuma kadhaa baadae.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.