Kiasi cha watu 70,000 walihudhuria matembezi ya fahari ya mashoga na wasagaji nchini Taiwani mnamo Oktoba 25 katika kusherehekea tofauti za hisia za kimapenzi na utambulisho wa kijinsia na kuuhamasisha umma kuiga mfano huo.
Idadi ya washiriki ilikuwa kubwa kabisa kuwahi kuonekana tangu matembezi ya kwanza yafanyike mwaka 2003. Katika miaka hii ya karibuni, matembezi haya yamekuwa makubwa kabisa katika bara la Asia na yamevutia hisia za wahudhuriaji wengi kutoka nje ya nchi.
Maudhui ya matembezi ya mwaka 2014 yalikuwa ‘Tembea kwa Kutumia Viatu ya (Unaowaona) Hawako kawaida,’ yakiakisi sauti za jamii za watu wa mapenzi ya jinsia moja, mashoga, wanaotengwa kama walemavu, watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na makahaba.
Washiriki wengi katika maandamano hayo walipaza sauti zao kuunga mkono hatua kuhalalisha kisheria ndoa za jinsia moja. Muswada wa usawa wa haki ya ndoa ulipelekwa bungeni na Taasisi ya Umoja wa Kukuza Haki za Ushiriki wa Kiraia nchini Taiwan mwaka 2012. Bunge liliupitia muswada huo baada ya kuusoma kwa mara ya kwanza Oktoba 23, 2013, lakini mchakato wa kisheria ulisimamishwa baada ya wapinzani wa sheria hiyo kupinga vikali ndoa za jinsia moja.
Wanaharakati wa haki za Mashoga walianza kuwashinikiza wabunge waurudie mswada huo mwezi Oktoba mwaka huu na usomaji wa wazi wa muswada huo ulifanyika Oktoba 16. Wapenzi wengi katika jamii ya mashoga walitumia fursa ya maandamano ya mwaka huu kusimuliza hali na matumaini yao kwa wengine.
Hapa chini unaweza kuona picha zilizopigwa kwenye maandamano hayo.