GV Face: ‘Tupige Kura au Tusipige'? Sauti za Raia wa Tunisia Katika Uchaguzi Unaokaribia

Uchaguzi Mkuu huu ni wa kwanza tangu Tunisia ipate katiba mpya na ni wa pili tangu yafanyike maandamano ya 2011 yaliyomng'oa madarakani Rais wa zamani wa nchi hiyo Ben Ali.

Tunisia ndiko kulianzia cheche za Mapinduzi ya Kiarabu zilizoenea katika eneo lote la Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati mwaka 2011. Mapinduzi hayo katika nchi hizo yalisababisha mashindano ya kisiasa, mapinduzi ya kijeshi au ghasia zisizokwisha, lakini mambo yamekuwa tofauti nchini Tunisia.

Zaidi ya wagombea 9,000 kutoka vyama zaidi ya 100 wanagombea kwenye uchaguzi huu, na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, wa-Tunisia hawawezi kubashiri chama gani kitashinda.

Baadhi ya wananchi wa Tunisia wameamua kufanya maamuzi ya makusudi ya kutokupiga kura, wakati wengine wakiamua kuelekeza kura zao kwa vyama vichache vyenye nguvu za kisiasa ambao wanaonekana kuzoa kura nyingi.

Mhariri wetu wa Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati Amira anazungumza na mwandishi wetu wa GV Ahmed Medien na mwangalizi wa uchaguzi Emir Sfaxi.

Tunazungumza nao kuhusu matumaini na matarajio yao, zoezi la uchaguzi na mabadiliko ambayo uchaguzi huo unaweza kuyaleta katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Fuatilia uchaguzi huo kwenye mtandao wa Twita: #TnElec2014 | #tnelec

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.