Miezi Michache Baada ya Kupotea kwa MH370, Kuanguka kwa Ndege Nchini Ukraine Kwawashitua Raia wa Malasia

A relative of those on board flight MH17 getting emotional while being interviewed by media. Photo by Hon Keong Soo. Copyright @Demotix (7/18/2014)

Ndugu wa baadhi ya watu waliokuwa wakisafiri kwa ndege aina ya MH17 akionesha uso wa huzuni pale alipohojiwa na vyombo vya habari. Picha na Keong Soo. Haki miliki na @Demotix (7/18/2014)

Kutokana na tukio la kuanguka kwa ndege aina ya MH17 ya shirika la ndege la Malaysia, huko mashariki mwa Ukraine, salamu za rambirambi zimekuwa zikitumwa kwa familia za abiria 298 pamoja na wafanyakazi waliokuwemo kwenye ndege hiyo. 

MH17 ilitunguliwa kwa kombora la BUK ikitokea Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur. Taarifa mbalimbali zinawahusisha waasi walio na uhusiano wa karibu na serikali ya Urusi ambao kwa bahati mbaya waliishambulia ndege ya abiria, hata hivyo, kiongozi wa waasi hao amekanusha taarifa hizi. 

Hili ni tukio la pili kuzikumba ndege za Malaysia katika kipindi cha miezi kadhaa. Ndege aina ya MH370 Malaysia iliyokuwa na watu 239 pamoja na wahudumu mnamo Machi 8 ilitoweka na haijulikani ilipo mpaka sasa.

Wakishtushwa na matukio hay mawili, raia wa mtandaoni wa Malaysia wanatumia kiungo habari cha Twita #PrayForMH17 kujadili kuhusiana na tukio hili la kuanguka kwa ndege.  

Mhudumu wa ndege ya shirika la ndege la Malaysia alijadili kwa uchache kuhusiana na idadi kubwa ya watu kupoteza maisha kwenye ndege hiyo aina ya MH17 pamoja na ile yaMH370, kwa kuweka picha katika ukurasa wa Twita na Instagram: 

Kwa kipindi cha miezi 4 nimepoteza marafiki wanaofikia 30…. inasikitisha lakini ukweli ni kuwa tunaishi katika ulimwengu uligubikwa na uadui

Image shared from a Malaysia Airlines flight attendant's Instagram

Picha iliyowekwa na mhudumu wa shirika la ndege la Malaysia Instagram

Wanasiasa wengi walitumia kurasa zao za Twita wakionesha namna walivyoguswa na tukio hili na pia kutoa maoni yao kuhusiana na kipi kifanyike kufuatia tukio hili.

Waziri mkuu, Najib Razak alitoa pole kwa familia za wafiwa:

Ninawaombea abiria na wahudumu wote wa MH17, pamoja na familia za wafiwa. Huu ni wakati mgumu sana kwetu sote.

Hishammuddin Hussein, ambaye ni waziri wa ulinzi wa Malaysia alitwiti kuhusiana na mikakati ya serikali ya Malasia: 

Mikakati yetu ya sasa ni kutaka kujua- 1) Ndege ile ilingushwa? na kama ndivyo, 2) Iliangushwaje? 3) Na nani? Vikosi vyetu vyote vya usalama wa taifa tayari vimeanza kazi.

Waziri wa Malaysia wa wizara ya Vijana na Michezo, Khairy Jamaluddin, alisisitiza kuwa lawama zisielekezwe kwa ndege za Malaysia kupita katika anga la ukanda ulio na mgogoro:  

Tunapaswa kupinga maelezo ya kulalamikia uchaguzi wa uelekeo. UHALISIA: Ndege nyingine nyingi zimepita pia katika anga hilo. UHALISIA: ICAO ilihakiki uelekeo huo.

Raia kadhaa maarufu wa Malaysia walitoa salamu salamu zao za pole na kuonesha namna walivyoguswa na tukio hili kupitia kurasa zao za Twita. Miongoni mwao ni mchezaji wa mchezo wa mpira wa vinyoya wa Malasia, Lee Chong Wei: 

Moyo wangu unasononeka sana ninaposhuhudia ndugu na wapendwa wetu waliokuwa wakisafiri na #MH17 waliopoteza maisha katika tukio hili baya na la kusikitisha.

Mtangazaji wa Televisheni na Redio, Xandria Ooi alidokeza kuwa lawama hazitasaidia kujua chanzo: 

Kusikiliza kupitia kwenye kompyuta ilisikitisha sana. Wengi wanafahamu kuwa ndege hii iliruka katika uelekeo ilipopatia ajali kwa makosa. Hili ni janga. Lawama hazisaidii.

Pang Khee Teik, mratibu wa Seksualiti Merdeka (Tamasha la usawa wa jinsia la Malasia), alituma salamu zake za pole:

Katika ulimwengu wa kusadikika, matukio ya kusadikika yanaweza kuwa na maana. Katika ulimwengu wa kusadikika, upendo wa kusadikika ndio wokovu wangu wa pekee. Ninawapenda nyote.

Kumekuwa na njama zinazosambaa mitandaoni kuhusiana na kuanguka huku kwa ndege, lakini kwa jamii kubwa ya watu wa Malasia, huu ni wakati wa kuomboleza vifo vya watu wasio na hatia na kuwafariji wale wote waliofiwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.