Jifunze Namna ya Kulinda Mawasiliano Yako ya Barua Pepe kwa Dakika Zisizozidi 30

#EmailSelfDefense infographic by Journalism++ for the Free Software Foundation (CC BY 4.0)

Picha ya maelezo ya #UlinziwaBaruaPepe iliyotengenezwa na Mfuko wa Zana za Uandishi wa Habari wa Bure (CC BY 4.0)

Ulinzi binafsi wa Barua pepe , ni mwongozo wa anayetaka kujifunza kulinda barua pepe zake kwa kutumia Mfuko wa Zana Huru (FSF), uliotolewa katika lugha sita mpya [kifaransakijerumanikijapanikirusikirenokituruki] mnamo Juni 30, 2014. Matoleo katika lugha nyinginezo yako mbioni kutoka.

Hata kama huna cha kuficha, kutumia zana hii kunalinda faragha ya watu unaowasiliana nao, na kufanya iwe vigumu kwa mifumo inayofuatilia mawasiliano ya watu kufanikiwa. Kama una kitu mihumu cha kuficha, basi umefika; hizi ni zana ambazo Edward Snowden alizitumia katika siri zake maarufu kuhusu sirika la ujasusi la Marekani NSA.

"Edward, a friendly email bot helps Email Self-Defense users test their new encryption systems."

Edward, kitufe kidogo rahisi, huwasaidia watumiaji wa zana ya Kujilinda Barua pepe zao katika mfumo mpya wa kutunza faragha.

Mwongozo huo wa FSF ulichapishwa awali kwa kuzinduliwa kama sehemu ya kampeni ya GV ya Reset The Net mnamo Juni 5, 2014 — siku ya dunia ya kuchukua hatua dhidi kufuatiliwa kwa mawasiliano ambayo ilisherehekea mwaka wa kwanza kwa kufunuliwa kwa siri za namna Shirika la Ujajusi la Marekani (NSA) linavyopeleleza mawasiliano ya watu kwa kutumia mashine, siri iliyotolewa hadharani na Edward Snowden.

Ulinzi binafsi wa barua pepe ni sehemu muhimu ya utatuzi wa tatizo la kufuatiliwa mawasiliano,” FSF linasema:

Wakati tunajifunza kutumia zana ya kulinda mawasiliano yetu, tunahitaji pia kufanya shinikizo la kisiasa dhidi ya ufuatiliaji, kujenga mtandao salama zaidi wa intaneti, na kulazimisha serikali na makampuni kupunguza kiasi cha data  wanazozitumia kutuhusu sisi kama hatua ya kwanza. Tunatumaini kuwa matoleo yaliyotafsiriwa ya Ulinzi Binafsi wa Barua pepe yanaweza kuwa mwanzo wa harakati zenye surra nyingi kwa watu wote duniani kote.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.