Salamu, Brazil: Mashabiki wa Kiislam wa Kandanda na Kombe la Dunia la FIFA

futbol muslim

Picha imepigwa na Willard kwenye mtandao wa flickr. CC BY-NC-ND 2.0.

Raia wa Colombia aliye na makazi yake katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Marcelino Torrecilla anatuhabarisha [es] kuhusiana na upekee wa mashabiki wa kiislamu wa mpira wa miguu kwenye Kombe la Dunia la FIFA, 2014 :

Katika Kombe la dunia, waislamu 50,000 wamesili kutoka katika mataifa mbalimbali kama vile Irani, Naijeria, Aljeria, Marekani, Uingereza, Malaysia na wengine wengi wanaotarajiwa kutoka katika Ghuba hii. kwa hakika, wataweza kuijaza takribani misikiti 80 iliyo katika maeneo mbalimbali ya nchi hii kubwa kabisa;

Aliendelea kusema kuwa:

Nchi sita kati ya 32 zinazoshiriki shindano hili, hiki ni kiwango kikubwa cha ushiriki wa waislam. Miongoni mwa nchi hizi, tunazo, Bosnia-Herzegovina, Kameruni, Irani, Code Ivar na Naijeria.

Unaweza kumfuatilia Marcelino kwenye mtandao wa Twita.

Posti hii ni sehemu ya sita ya mpango wa #LunesDeBlogsGV [Jumatatu ya blogu kwenye GV] siku ya Juni 9, 2014.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.