Shirika la Friedrich Ebert Lachapisha Ripoti ya Matumizi ya Mitandao ya Kijamii Nchini Cameroon

Shirika la Friedrich Ebert limechapisha ripoti ya utafiti kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Cameroon:

Kwa kiwango kipi, kwa malengo yapi na kwa akina nani basi mitandao ya kijamii kama Twita, Facebook, Blogu, Linkedin, nk. inatumika nchini humo? Kujua majibu ya maswali hayo, Shirika la Friedrich Ebert limetoa taarifa ya matumuzi ya mitandao ya kijamii nchini Cameroon…

Kwa upande wa umaarufu wa mitandao ya kijamii, kama ilivyo kwingineko, Facebook ndiyo zana maarufu zaidi nchini Cameroon. Baadhi ya makundi ya Ki-Camerron yana hadi wafuasi 20.000 na zaidi. Na kwa hali ya kushangaza ni umaarufu wa mtandao wa Linkedin. Karibu watumiaji wanne kati ya watano wa mtandao wa intaneti nchini Cameroon wamejiunga na huduma hiyo, ikilinganishwa na asilimia tatu tu kwenye nchi jirani ya Naijeria. Utafutaji wa kazi na fursa za ajira inaweza kuwa sehemu ya majibu ya hali hii. Mtandao mwingine unaopata umaarufu nchini humo ni Twita. Cameroon kwa sasa ni kati ya nchi kumi maarufu za kiafrika zenye ujazo mkubwa wa twiti, ingawa twiti nyingi zinatokea kwenye miji ya Douala na Yaoundé. Kwa kulinganisha, bado kuna uchanga wa kublogu, kwa kuangalia mahitaji makubwa ya muda na maudhui. Hata hivyo, ingawa wanablogu wa Cameroon ni wachache kwa idadi, wana uwezo mkubwa kimaudhui na viwango. Baadhi ya blogu maarufu zaidi barani Afrika zinatoka Cameroon, baadhi zikiwa zinaratibiwa na na muungano wa wanablogu uitwao “Collectif des Blogueurs Camerounais.” Kwa nyongeza, tayari jitihada za kiubunifu zimefanyika na haina shaka kuwa jitahada hizo zitaongeza kuenea kwa mitandao ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi ambayo kwa sasa inasaidia kukuza shughuli za kiuchumi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.