Mzazi wa Kisyria Auomba Ubalozi wa Uingereza Kumwunganisha na Mwanae

Syrian father Wael Zain claims his British son, Maudh, aged five, is stranded in Syria and that the British Foreign Office is not helping reunite them. Photograph shared on Twitter.

Mzazi wa Kisyria Wael Zain anadai mwanae wa kiume mwenye uraia wa Uingereza, mwenye miaka mitano, amekwama Syria na kwamba Ubalozi wa Uingereza haujamsaidia kukutana nae. Picha imewekwa kwenye mtandao wa Twita.

Wael Zain, Msyria anaishi na kufanya kazi jijini Londoa, ameingia kwenye mtandao wa Twita kutafuta kusikilizwa kufuatia tatizo la mwanae mwenye umri wa miaka mitano, Maudh, mwenye uraia wa Uingereza, ambaye amekwama na kubaki Syria kwa miaka mitatu.

Katika mfululizo wa twiti zake, Zain anaeleza kwamba mwanae huyo, anayedai kuwa alipigwa risasi, anaishi na mama yake kwenye kijiji fulani eneo la Deraa, na anahitaji matibabu kuokoa maisha yake. Anadai kwamba Ubalozi wa Uingereza umekuwa kiziwi kila alipofanya jitihada za kuwasilisha maombi yake.

Akiandika mwenyewe kutoka Deraa, Syria, Zain anatwiti:

Tafadhali msaidieni mwanangu wa miaka 5 (Mwingereza) aliyeko Syria aweze kuja nyumbani. Ubalozi wa Uingereza umemtelekeza

Anaeleza:

Kwa sasa yuko na mama yake kijijini karibu na eneo la Nawa huko Seraa. Amekuwa huko kwa miaka mitatu. Wiki mbili zilizopita alipigwa risasi. Anahitaji msaada

Katika twiti nyinginezo, alizozielekeza kwa Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ungereza William Hague, Zain anaomba:

Mhe Willian Hague mwanangu mwenye miaka mitano amekwama nchini Syria na ofisi yako imetelekeza.

Anaongeza:

Serikali ya Uingereza iliahidi kuwasaidia wakimbizi walio kwenye hatari nchini Syria hasa hasa wanawake na watoto lakini imegoma wamsaidia mtoto wa Kiingereza

Zain anasema hajamwona mwane kwa miaka mitatu na anaweka picha ya mara ya mwisho aliyonayo:

Hii ndiyo picha ya mwanangu akiwa Syria. Sijamwona kwa miaka mitatu. Anahitaji matibabu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.