Habari kutoka 30 Aprili 2014
Kurekebisha Historia: Sauti ya Wahanga Waliolazimishwa Kuwa ‘Wagumba’ Nchini Peru
Likiwa na lengo la kukusanya saini 3,000, shirika la MujeresMundi limeanzisha madai ya mtandaoni kwenye jukwaa la Change.org likiitaka serikali ya Peru kujenga upya kumbukumbu ya kihistoria kwa sauti ya wahanga wa dawa za ugumba: […] kipindi cha pili cha serikali ya Alberto Fujimori; sera ya Taifa ya Afya ya...
Robert Antoni Ashinda Tuzo ya Boca 2014 ya Fasihi ya ‘Caribbean’
Mwanablogu wa Jamaika aishiye ughaibuni Geoffrey Philp anataarifu kuwa Robert Antoni, mwandishi wa kitabu cha “As Flies to Whatless Boys”, ameshinda Tuzo ya One Caribbean Media Bocas 2014 kwa Fasihi ya Nchi za ‘Caribbean’ wakati blogu ya ‘Repeating Islands’ ikichapisha pitio la kitabu riwaya yake hapa.
Mashabiki Jijini Skopje Wakusanyika Kubadilishana ‘Stika’ za Soka
Mamia ya watu walikusanyika mchana wa Jumapili kwenye eneo la wazi jijini Skopje kubadilishana ‘stika’ za mkusanyiko rasmi wa picha za Kombe la Dunia la FIFA tarehe 28 Aprili, 2014. Nchini Macedonia, kama ilivyo kwa nchi nyinginezo za Yugoslavia ya zamani, utamaduni wa kukusanya ‘stika’ una historia ndefu, inaanzia miaka...
Namna ya Kutafuta Chumba cha Kupanga Nchini China
Chengdu Living anawafundisha wasomaji wake namna ya kutafuta chumba cha kupanga nchini China bila kwenda kwa dalali kwa kutoa mwongozo wa hatua tano.
Mzazi wa Kisyria Auomba Ubalozi wa Uingereza Kumwunganisha na Mwanae
Wael Zain, raia wa Syria anayeishi Londona, ametumia mtandao wa Twita kutafuta kusikilizwa madai yake kuwa mwanae wa kiume mwenye uraia wa Uingereza ametelekezwa Syria kwa miaka mitatu sasa.
Ni “Udhaifu” wa Serikali, Yasema Ripoti ya Ajali ya Kivuko cha Korea Kusini
Zimetimu siku 14 tangu kivuko cha Sewol kizame na watu 205 wamethibitika kupoteza maisha. Wanasiasa wanatumia tukio hilo na habari zisizosahihi za vyombo vya habari kuchochea hasira miongoni mwa Wakorea Kusini.