Siku ya Jumamosi ya Machi 8, mashirika ya habari duniani kote yaliripoti kuwa ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyokuwa angani kuelekea China imepotea. Ndege hiyo MH370 ilikuwa ikitokea Kuala Lumpur kwenda Beijing ilipoteza mawasiliano na waongoza ndege, ambapo shirika la ndege pamoja na mamlaka zinazohusika zikishindwa kufahamu kwa hakika iliko ndege hiyo. Ilikuwa na abiria 227 na wafanyakazi 12 wa ndege
Kwa mujibu wa gazeti la The Guardian, ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na kifaa cha kuongozea ndege ikiwa kwenye anga la Vietnam.
Shirika la ndege hiyo limekuwa likiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kutoa habari kuhusu mwenendo wa mambo, ikiwa ni pamoja na tamko lililotolewa na Mkurugenzi wake Mkuu Ahmad Jauhari Yahya:
Tunasikitika sana kuwa tumepoteza mawasiliano yote na ndege namba MH370 iliruka kutoka Kuala Lumpur saa 6.41 usiku wa manane ikielekea Beijing.
Ndege hiyo ilikuwa itue kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing saa 12.30 asubuhi kwa saa za Beijing.
Kituo cha Kuongozea ndege cha Subang kilitoa taarifa kuwa kimepoteza mawasiliano saa 8.40 usiku (kwa saa za Malaysia) leo.
Ndege MH370 ilikuwa aina ya Boeing B777-200.
Ndege hiyo ilikuwa imebeba jumla ya watu 239 na wafanyakazi -hiyo ikiwa ni abiria 227 (watoto 2), na wafanyakazi 12. Abiria walikuwa wa mataifa 13 tofauti.
Shirika la Ndege la Malaysia kwa sasa linafanya kazi kwa karibu na mamlaka ambao wanaendelea na zoezi la utafutaji na uokoaji kujaribu kujua ndege hiyo iko wapi.
Timu yetu kwa sasa inawapigia simu warithi wa abiria na wafanyakazi.
Taarifa nyingine kwa vyombo vya habari iliyotolewa na shirika hilo la ndege limemtambua rubani wa ndege hiyo kuwa ni Captain Zaharie Ahmad Shah, ambaye ana masaa 18,365 ya kurusha ndege kwenye mkanda wake.
Kwenye mtandao wa Twita, watu wengi wameonyesha wasiwasi na hofu:
Flown Malaysia Airlines @MAS many times, including one of their 777-200s from KL to Shanghai. Thoughts with all at this hard time.
— Peter McGinley (@PeterMcGinley) March 8, 2014
There are reports that Malaysia plane has crashed but no official confirmation. http://t.co/tE3HWmeNBt #BreakingNews — Christl Dabu (@ChristlJZDabu) March 8, 2014
Kuna taarifa kuwa ndege ya Malaysia imeanguka lakini hakuna taarifa rasmi za kuthibitisha hilo
The Malaysia Airlines’ flight that disappeared is exactly why I'm terrified of flying — Jonathan Woelk (@jonathanwoelk) March 8, 2014
Ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea ndicho hasa kinachonifanya niogope kusafiri kwa ndege
Fingers crossed the Malaysia Airlines plane did not crash and the 239 people aboard are safe and sound — C0ll0R. (@F_ckOhioSt) March 8, 2014
Naweza kujiapiza kuwa ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia haijaanguka na watu 239 walio kwenye ndege hiyo wako salama na wanaendelea vizuri
Very shocking news for aviation industry and those onboard! BBC News – Malaysia Airlines loses contact with plane flying to Beijing — Stephen Chimalo (@SChimalo) March 8, 2014
Habari za kusikitisha kuhusiana na tasnia ya usafiri wa anga na wale waliokuwepo kwenye ndege hiyo! Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC), Shirika la Ndege la Malaysia limepoteza mawasiliano na ndege yao iliyokuwa ikisafiri kuelekea Beijing
Tukio hilo limemfanya Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib Razak kujibu kupitia mtandao wa Twita:
My thoughts and prayers are with the family members of flight #MH370. I've asked all measures possible to be taken.
— Mohd Najib Tun Razak (@NajibRazak) March 8, 2014
Mawazo na maombi yangu yako na familia za wanaosafiri na ndege #MH370. Tumeagiza hatua zote zinazowezekana zichukuliwe
Shirika la Habari la Reuters sasa limeripoti kuwa ndege hiyo ilianguka kwneye Bahari za China Kusini, hata hivyo, hakuna tangazo rasmi lililotolewa wakati wa kuandikwa kwa makala haya.
1 maoni