Nyumba ya Kiongozi wa Upinzani Nchini Zimbabwe, Tendai Biti Yalipuliwa Mara ya Pili

Zimbabwe's former finance minister Tendai Biti.

Waziri wa zamani wa Fedha wa Zimbabwe Tendai Biti. Picha imetolewa chini ya leseni ya Creative Commons na Chatham House.

Nyumba ya Waziri wa zamani wa Fedha wa Zimbabwe Tendai Biti ilidaiwa kulipuliwa alfajiri ya Februari 25, 2014, watumiaji wa Twita na vyombo vingine vya habari vilitangaza. [Biti] ni mmoja wa wanachama tegemeo wa chama cha Upinzani cha MDC [Movement for Democratic Change] na mkosoaji mkubwa wa Rais Robert Mugabe.

Biti ni katibu mkuu wa MDC, kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Morgan Tsvangirai. Nyumba yake ililipuliwa mwaka 2011. Hakuna watuhumiwa walikamatwa mpaka sasa.

Nyumba ya Biti iliyoko Harare imelipuliwa kwa petroli

Inahuzunisha vibaya na ni ukichaa, vyote kwa pamoja. Sina upande wa kutetea. Bob [rais Robert Mugabe] anakula bata na kufanya utani kuhusu ghasia hizi za kisiasa

Wanaweza kukuta mabaki ya keki maarufu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa [rais Mugabe alisherehekea siku yake ya kuzaliwa Februari 21, 2014] kwenye chupa za vikopo vilivyotumika kutenengeneza mabomu

Vyama vyetu vya upinzani haviwezi kukwepa lawama kwa kuwa na vikundi vya wahuni, lakini mabomu ya petroli hayawezi kutoka kwingine kokote isipokuwa kwneye vyombo vya usalama vya dola.

Inagwa watu wengi wanaonekana kuitilia mashaka serikali, mtumiaji mmoja wa mtandao wa Twita, tinashe chirape, alipendekeza kuwa [huenda] ilikuwa ni kazi ya chama cha upinzani cha MDC chenyewe:

Hivi ghasia ndio zimeanza ndani ya MDC [chama cha upinzania cha Movement for Democratic Change]? Tsvangirai [Kiongozi wa MDC] tuliza hali ya mambo kwneye chama chako

Another user said the news of the bombing is fake:

Uongo! Ni chupa tu imetupiwa getini na mtoto wa mtaani aliyekuwa anapita

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.