#Mambo52KuhusuTanzania katika Kusherekea Miaka 52 ya Uhuru

Tanzania bara ilisherehekea miaka 50 ya uhuru wake kutoka kwa Waingereza tarehe 9 Desemba, 2013. Zamani ikiitwa Tanganyika, baayae iliungana na visiwa vya Zanzibar tarehe 26 April, 1964 kutengeneza nchi inayoitwa Tanzania.

Katika kusheherekea miaka 52 ya uhuru, watumiaji kadhaa wa mtandao wa Twita walitumia alama ishara ya #52ThingsAboutTanzania (yaani #Mambo 52KuhusuTanzania) kushirikishana takwimu na uhalisia kuhusu nchi yao:

Julius Nyerere “Baba wa Tanzania” alitafsiri kitabu cha Shakespeare kiitwacho “The Merchant of Venice; Julius Ceaser” kwa Kiswahili.

Mount Kilimanjaro,  the highest mountain in Africa, and the highest free-standing mountain in the world, in Moshi, Tanzania. Photo released by Muhammad Mahdi Karim (www.micro2macro.net) under GNU Free Documentation License.

Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu kuliko yote Afrika, na mrefu kuliko milima yote iliyosimama yenyewe bila kuwa kwenye safu za milima, ukiwa Moshi, Tanzania. Picha imewekwa na Muhammad Mahdi Karim (www.micro2macro.net) chini ya Leseni ya GNU Free Documentation.

Mlima mrefu kuliko yote duniani usio kwenye safu za milima ni Mlima Kilimanjaro

Tanzanite [vito vya thamani vinavyopatikana Tanzania] yameitwa kwa jina la nchi ya Afrika Mashariki iitwayo Tanzania mahali ambapo ndiko yanaykotoka. Jina hilo lilibuniwa na Tiffany.

Coconut crab,  the largest land-living terrestrial crab in the world, Photo released under Creative Commons by Flickr user Drew Avery.

Kaa aitwaye Coconut crab, kaa mkubw akuliko wote aishiye nchi kavu duniani kote,
Picha imewekwa mtandaoni kwa leseni ya Creative Commons na mtumiaji wa mtandao wa Flickr aitwaye Drew Avery.

Kiswahili kimeanzia Tanzania na hivi sasa kinazungumzwa na nchi kumi tofauti ikiwemo visiwa vya Comoro

Ngorongoro Crater,  a UNESCO World Heritage Site and one of the seven natural wonders of Africa, located in Arusha, Tanzania. Photo released by Thomas Huston under  GNU Free Documentation License,.

Hifadhi ya Ngorongoro, eneo ambalo kwa mujibu wa UNESCO ni Urithi wa Dunia na moja wapo ya maajabu saba ya asili ya dunia barani Afrika, lipo Arusha, Tanzania. Picha imewekwa mtandaoni na Photo Thomas Huston chini ya leseni ya GNU Free Documentation.

Bonde la Hifadhi ya Ngorongoro, nchini Tanzania, ni bonde kubwa kuliko yote duniani.

Tanzania inayo mlima wapili kwa ukubwa duniani (Kilimanjaro)

Sarafu ya Tanzania ni Shilingi ya Tanzania

Hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara, nchini Tanzania, ni makazi ya simba wakweao mitini wasiopatikana kwingineko kote duniani

Tree climbing lion in Tanzania. Photo released under Creative Commons by Flickr user Tracey Spencer.

Simba apandae miti nchini Tanzania. Picha iliwekwa kwa matumizi ya matandaoni chini ya leseni ya Creative Commons na mtumiaji wa mtandao wa Flickr Tracey Spencer.

Fuvu la kale zaidi duniani kuwahi kugundulika liligunduliwa kwenye Bonde la Olduvai nchini Tanzania

Mbuga ya Wanyama ya Amani (Mashariki mwa Tanzania) ni sehemu pekee duniani ambapo Maua yenye asili ya Afrika yaoteshwayo majumbani huota mwituni.

Mtu maarufu anayeheshimika sana duniani, Julius Nyerere (1922-1999) alikuwa mwanasiasa wa kanuni na mwenye kipaji cha akili nyingi

Mti wa Mpingo, wenye rangi nyeusi, unaopatikana sana Tanzania, ni moja wapo wa miti iliyo ghali zaidi duniani

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.