Bango la kuonyesha heshima kwa Nelson Mandela limechukua umaarufu usiojulikana wa kiongozi wa Afrika Kusini nchini Brazil kwa kuwaita wale ambao wanaenzi urithi wake kusaidia haki za binadamu. Ujumbe huo ulienezwa na shirika lisilokuwa la kiserikali Conectas Human Rights katika Siku ya Haki za Binadamu, Desemba 10, 2013.
“Tenda zaidi ya kuongozwa” ni mwito wa shirika katika nchi ambapo kihafidhina na maono hasi kuhusu haki za binadamu inaonekana kuongezeka. Kama baadhi kura za maoni ya hivi karibuni zinaonyesha, 90% ya Wa-Brazil wanaunga kupunguza umri wa miaka kwa jukumu la jinai, na 61% wanaamini kwamba uhalifu unasababishwa na tabia mbaya za watu.