Chama cha Upinzani NPP Chapinga Matokeo ya Urais Ghana Mahakamani

Chama Kikuu cha Upinzani nchini Ghana, New Patriotic Party (NPP), kimeyapinga matokeo ya hivi karibuni ya Uchaguzi wa Rais, kikidai uchaguzi huo ulighubikwa na vitendo vya udanganyifu. Kikigoma kuyakubali matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi, chama hicho kimeamua kulipeleka suala hilo katika vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa blogu yaGhana Decides:

chama hicho kikuu cha upinzani NPP kimeyapinga matokeo ya uchaguzi wa rais mwaka 2012, kikiituhumu Tume ya uchaguzi kutumiwa na chama kilichoko madarakani, National Democratic Congress (NDC) kuiba kura.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Dr. Kwadwo Afari Gyan, amekanusha madai hayo akisema kwamba chama cha NPP wanayo haki ya kupinga matokeo hayo katika mahakama za Ghana kwa mujibu wa sheria za uchaguzi za nchi hiyo.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Dr. Kwadwo Afari Gyan, alimtangaza Rais Mahama kuwa mshindi kwa kujipatia asimilia 50.7 ya kura, akimshinda mpinzani wake wa karibu Nana Akufo-Addo wa chama cha NPP aliyepata asimilia 47.7 ya kura.

Ubashiri wa matokeo uliofanywa na chama cha NPP. Picha: Ukurasa wa Facebook wa Nana Ado (Mgombea Urais wa NPP).

Ubashiri wa NPP katika ukurasa wao wa Facebook ulioneysha kwamba wameshinda uchaguzi huo kwa mujibu wa matokeo waliyoyapokea kutoka kwa mawakala wao wa uchaguzi.
Blogu ya Ghana Decides inaripoti:

Chama cha NPP kinasisitiza kwamba matokeo yaliyokuwa kwenye “nakala za karatasi za bluu”, ambayo yalipokewa katika vituo vyote vya kupigia kura na vile vya kuhesabia kura kote nchini, yalibadilishwa kidogo kumpendelea Mahama wa chama cha NDC.

Vigogo wa chama hicho cha NPP wamekuwa wakiendelea na mkutano kujadili suala hilo na kuangalia ikiwa kuna ulazima wa kuchua hatua za kwenda mahakamani.

Blogu ya Ghana Decides inaripoti:

Kufuatia hayo, chama cha NPP kimeamua kulipeleka suala hili mahakamani na wameapa kutumia njia zote zinazowezekana kutafuta haki. Wakati huo huo, wafuasi wengi wa chama hicho walijitokeza katika mitaa ya Circle, wakiwa na kiu ya kuwasikiliza viongozi wa chama chao ambao walikuwa wamejikusanya karibu na mtaa wa Kwame Nkrumah Circle kuwahutubia wananchi.

Watazamaji na waangalizi wa uchaguzi huo, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Afrika na CODEO wameyaunga mkono matokeo hayo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi na wametoa wito wa amani.

Haya ni baddhi ya maoni ya wa-Ghana kwenye mtandao wa Twita:

@nosivid: Nana Addo anazunguka akirudia madai yale yale ya wizi wa kura akidai ana ushahidi na ametaka MAELEZO #GhanaDecides

@kwasireports: “Nitaenda mahakamani”-Nana Akuffo-Addo amethibitisha wakati chama cha NPP kikiandaa ushahidi kuyapa nguvu madai yao ya wizi wa kura uliofanywa na chama cha NDC #GhanaDecides #amaniee

@nfaoforiatta: Ni wazi wamepoteza uchaguzi. Wa-Ghana wausimamie ukweli utakapowekwa bayana. Huu ni mustakabali wetu wa kulindwa. #GhanaDecides

@Kwabena: Ah, sawa, nilidhani wasingefungua kesi. Mahakama Kuu iamue sasa. #GhanaDecides

@sam_btw: Chama cha Upinzani cha NPP kimegndua tofauti ya asilimia 10 ya kura katika uchaguzi wa rais 2012. Udanganyifu? Ni juu ya Mahakama Kuu kuamua #GhanaDecides

Wanasheria wanaokiwakilisha chama cha NPP hapo awali walifungua kesi katika Mahakama Kuu tarehe 28 Desemba, 2012. Chama cha NPP kina siku 21 pekee kupinga matokeo hayo ya uchaguzi kisheria vinginevyo rais aliyechaguliwa ataapishwa tarehe 7 Januari, 2013.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.