Habari kutoka 30 Disemba 2012
Kitabu-pepe Kipya cha GV: Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko
"Sauti ya Kiafrika ya Matumaini na Mabadiliko", kinakupa mtazamano wa kipekee kuhusu watu na habari za eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kupitia posti zetu zilizo bora zilizoandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa mwaka 2012. Hii ni zawadi sahihi kabisa ya kuukaribisha mwaka mpya.
Kenya: Kufundisha Uvumilivu wa Kikabila Kupitia Hadithi za Sayansi
Watoto wa Kenya wanafundishwa uvumilivu wa kikabila kupitia hadithi za sayansi: “Kushambuliwa kwa akina Shida:Bunduki za AKA Zaokoa Sayari” ni hadithi inayozungumzia maisha ya jamii tatu zilizoishi katika jangwa katika...
Video ya Kuomba Ujenzi wa Vyoo vya Umma huko Jharkhand, India
Amit Topno, mwakilishi wa jumuiya ya hiari “inayopiga picha za video” aliripoti kwamba wakati wa kijiji cha Nichitpur katika Jimbo la Jharkhand hawana choo chochote cha umma kinachotumika. Wanavijiji wanaziomba...
Chama cha Upinzani NPP Chapinga Matokeo ya Urais Ghana Mahakamani
Chama Kikuu cha Upinzani nchini Ghana, NPP, kimegoma kuyakubali matokeo ya uchaguzi wa Rais. Mnamo tarehe 9 Desemba 2012, Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Rais Mahama kuwa mshindi kwa asilimia 50.70 ya kura, akimshinda mshindani wake wa maribu Nana Akufo-Addo wa NPP. Chama cha NPP hapo awali kilifungua mashitaka katika Mahakama Kuu tarehe 28 Desemba, 2012.