Tanzania/Malawi: Utafutaji Mafuta kwenye Ziwa Nyasa WachocheaMgogoro wa Umiliki

 

Habari kwamba Malawi inachunguza kuwepo kwa mafuta katika Ziwa Nyasa (pia linajulikana kama Ziwa Malawi, Ziwa Nyassa, Ziwa Niassa na Lago Niassa) kumeibua mjadala motomoto juu ya umiliki wa ziwa hilo. Wakati serikali ya Malawi inadai kulimiliki ziwa lote peke yake, Tanzania inatoa wito kwamba umiliki wa ziwa hilo uwe nusu kwa nusu, kwamba mpaka uko katikati ya ziwa.

Mgogoro huu unaanzia zama za ukoloni mwaka 1890, wakati Uingereza na Ujerumani kwa pamoja walipochora mipaka na maeneo ya nchi walizokuwa wakizimiliki. Wakati huo hakuna aliyefikiri kuhusu uwezekano wa kuwepo kwa mafuta chini ya ziwa hilo.

Kulingana na mwandishi wa habari na mwanablogu Mavuto Jobani, Oktoba mwaka jana 2011, Malawi ilisema ilikuwa imeipa leseni ya kutafuta mafuta kampuni ya Kiingereza Surestream Petrol.

A map showing two different borders between Tanzania and Malawi. Image courtesy of wavuti.com.

Ramani ikionyesha mipaka miwili tofauti kati ya Tanzania na Malawi. Picha kwa hisani ya wavuti.com

 

Akinukuu vyanzo rasmi vya Tanzania, Jubani anaandika:

 

“Malawi inadai kuwa ziwa lote ni mali ya nchi kulingana na mipaka ya kikoloni … Lakini msimamo wetu ni kwamba nusu ya ziwa ni mali ya Tanzania,” alisema Assah Mwambene, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.

Wakati baadhi ya wananchi wa Malawi wana hofu kuwa huenda kutazuka mapigano kati ya mataifa hayo mawili kwa ajili ya mzozo huo wa mpaka, serikali yao inasema mambo yanashughulikiwa vizuri na wamejipanga kushughulikia suala hilo ipasavyo.

Wanablogu kama Pearson Nkhoma wameepuka kutoa maoni yao juu ya maendeleo hayo mapya badala yake wamechagua kuwasilisha ukweli wa mambo. Kwa mfano Nkhoma anaandika:

 

Ziwa Malawi ni nmakazi ya aina zaidi ya 1000 za samaki. Idadi hii inakadiriwa kuwa ya juu mahali pamoja kulinganisha na maeneo mengine mbalimbali duniani. Ni la tatu kwa ukubwa barani Afrika, baada ya Ziwa Tanganyika lililopo Tanzania na Ziwa Victoria ambalo nalo sehemu yake kubwa inamilikiwa na Tanzania. Nchini Tanzania, Ziwa Malawi linaitwa Ziwa Nyasa, jina inayotokana na jina la Malawi wakati wa ukoloni, Nyasaland. Katika miaka ya mwanzo ya 1960, Dr Hastings Kamuzu Banda, aliyekuwa Rais wa Malawi, pia aliwahi kudai kwamba Mbeya — mkoa mmojawapo nchini Tanzania — ulikuwa sehemu ya Malawi.

Vyombo vya habari nchini Malawi na majukwaa ya kijamii vimejaa mjadala juu ya umiliki wa ziwa na uwezo wa mali kutokana na utafutaji mafuta. Wa-Malawi wengi wanadai umiliki kamili wa ziwa kubwa la tatu Afrika la maji baridi.

Ziwa Malawi/Nyasa kutokea upande wa Kisiwa cha Likoma. Picha iliyotolewa chini ya utaratibu wa Creative Commons (CC BY-SA 3.0) na mtumiaji wa Wikipedia Worldtraveller.

 

Serikali ya Tanzania mwaka 2007 iliagiza kwamba ramani zote zilizokuwa zikionyesha kwamba mpaka kati ya Malawi na Tanzania uko upande wa ndani ya Tanzania kwenye ufukwe wa ziwa zikamatwe na kutiwa moto, kwa sababu ya ‘kupotosha umma wa Tanzania na jumuiya ya kimataifa’ kuhusu uhalisi wa mpaka kati ya nchi hizo mbili.

Nchi hizo mbili zitakutana nchini Malawi tarehe 20 Agosti, 2012 ili kujadili suala hilo.

 

 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.