Tofauti na nchi nyingine katika eneo lake, Sudani mara nyingi huwa haipati nafasi katika vyombo vikuu vya habari, na hili lilikuwa wazi zaidi wakati wa maandamano yaliyofanyika Ijumaa na Jumamosi. Sababu ni kwamba serikali ya Sudani imevibana mno vyombo vya ndani vya habari na kuwazuia waandishi kuripoti habari zinazohusu masuala ya haki za binadamu na ufisadi.
Hali hii, hata hivyo haihalalishi tabia dhahiri ya vyombo vya habari vya nje ya kutotilia maanani [maandamano hayo]. Al Jazeera, kwa mfano, ilifanya wajibu wake kwa namna ya pekee katika kuripoti maandamano yaliyotokea katika nchi kadhaa za ki-Arabu, lakini watumiaji wa mtandao wanasema shirika hilo linaonekana kupuuza matukio yanayoendelea nchini Sudani.
Habari za maandamano ya hivi karibuni nchini Sudani zilizopata nafasi kwenye vyombo vikuu vya habari, zilionekana tu kwenye makala zilizochapishwa kwenye mtandao wa Al Arabiya na Al Jazeera, kwa kujumuisha dondoo chache kwenye Idhaa ya Kiingereza ya Al Jazeera. Mashirika mengine ya habari yaliyoripoti maandamano hayo ni CNN, The Star shirika la habari la ki-Malaysia, New York Times, Yahoo News, ABC News, na Chicago Tribune. Hata hivyo, habari hizi hazijafanya watu kujua vizuri kile kinachoendelea nchini humo, kwa kuwa, kwa mujibu wa watumiaji wa mitandao, vyombo hivi vya habari havina hadhira kubwa katika eneo hili.
Maandamano yalianza baada ya swala ya Ijumaa katika msikiti wa mtaa wa Wad Nubawi huko Omdurman. Wito wa maandamano ulitolewa kupitia alama habari ya #SandstormFriday siku moja kabla. Maandamano yaliratibiwa ili kupinga mfumuko wa bei na mpango wa serikali kubana matumizi ambao ulitangazwa na rais wa Sudan Omar Al-Bashir na kuanza kutekelezwa juma lililopita. Wale waliosikia habari za maandamano hayo walijitokeza kwenye eneo la tukio. Hamid alikuwa mmoja wao, na hapa alitwiti tweeted [ar]:
Baada ya swala, watu walikusanyika mbele ya msikiti na kuandamana kupitia barabara za mitaa ya Wad Nubawi wakiimba kauli mbiu za kupinga utawala wa nchi hiyo. Maandamano yalimalizika saa chache kabla ya polisi kuwatawanya waandamanaji kwa kutumia mabomu ya machozi na polisi waliokuwa wamevaa kiraia walijipenyeza kwenye makundi ya waandamanaji.
Baada ya waandamanaji kutawanywa, Yousif Al Mahdi alikuwa kwenye eneo la tukio na
kutwiti :
في الطريق إلى مسجد السيد عبدالرحمن بودنوباوي #جمع_الكتاحة”.
Maandamano yamerudi safari hii kwenye wilaya ya Wad Nubawi wakipambana, magari ya polisi yameegeshwa pembeni mwa barabara yanarusha mabomu ya machozi
Wakati huo huo, maandamano kama hayo yalianza kwenye mitaa ya Burri jijini Khartoum, na baadae kule Al-Daim. Maandamano ya Burri yalidhibitiwa haraka sana na wanausalama wakishirikiana na polisi. Yale ya Al-Daim hata hivyo yalikuwa makubwa mno kwa polisi kuweza kuyadhibiti. Ammar Mahdi alitwiti :
Maandamano ya Al-Daim yaliendelea mpaka usiku huku magari kadhaa ya polisi yakiteketezwa kwa moto na wanaandamanaji. Haitham Makkawi alikuwa kwenye eneo la tukio na alidai kwamba wakaazi wa Al-Daim wamejaza eneo hilo:Masaa machache yaliyopita kutoka #AlDaim watu wanatupa alama za polisi na wanapanda juu ya alama hizo
Wakazi wa Al-Daim wamejazana eneo hili! Picha za kuteketea kwa magari ya polisi zimetawanyika kwenye mtandao wa twita kuonyesha athari ziliozletwa na waandamanaji.
Baadae usiku huo, maandamano mengine yalianza kwenye mtaa wa Siteen, barabara kuu mjini Khartoum, karibu na mtaa wa Riyad;Picha hii inaonyesha wanaandamanaji wakikusanyika kuzunguka tairi linaloungua moto katikati ya barabara.
Girifna, wanaharakati wa vuguvugu la amani, walitumia zana za habari za kiraia kama Facebook na Twita ili kutawanya habari kuhusu mahali walipo waandamanaji katika mji huo mkuu wenye majimbo matatu. Katika twiti hii, Girifna anaelekeza watu eneo la maandamano huko Omdurman:
Jitihada za Girifna ni mfano dhahiri wa uandishi wa habari za kiraia katika nchi ambapo uhuru wa kujieleza na kuripoti habari umebinywa.
Jamii ya wa-Sudani mtandaoni ilifurahishwa mno na matukio yanayoendelea katika mji mkuu wa Khartoum; Hamid Murtada, ambaye alikuwa kwenye maandamano hayo, alitwiti:
Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa twita wa-Sudani walifurahishwa na matukio yanayotokea mjini Khartoum na yale yanayotokea kwenye nchi nyingine za eneo hilo na kuonyesha mshikamano na wale wanaohangaika kujikwamua na tawala za ki-dikteta duniani kote. Khalid Ewais, mwandishi wa habari wa Al Arabiya, alitwiti:
Raia wa Sudani wanaoishi nje ya nchi hiyo walikuwa tayari kwa wale waliohitaji msaada walioko eneo la tukio kwa kuwapa maelekezo ya namna ya kutangaza maandamano hayo na matumizi ya zana za uandishi wa kiraia ikitokea mtandao wa intaneti umekatwa. Nada, m-Sudani anayeishi Misri, alishauri namna ya kutangaza vyema yanayoendelea kwenye maandamano:
Kama unatumia simu aina ya IPHONE na ni miongoni mwa waandamanaji nchini Sudani, shusha (download) programu ya USTREAM kupitia kitendea kazi kiitwacho world#SudanRevolts.
Jamii ya mtandaoni ya wa-Sudani ina matumaini na mwelekeo wa mapinduzi ya Sudani, ambapo wengi wanajiapiza kwamba tarehe 30, Juni 2012 itakuwa siku ya mwisho ya chama kinachotawala nchi hiyo cha NCP (National Congress Party) kuadhimisha kuwapo kwake madarakani.
1 maoni