Afrika: Kusherehekea Siku ya Ukombozi wa Afrika kwenye Mtandao wa Twita


Siku ya Ukombozi wa Afrika
ni maadhimisho ya kila mwaka kukumbuka tarehe 25 Mei 1963 siku ambayo Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ulianzishwa. Siku ya Ukombozi wa Afrika 2012, ambayo awali iliiitwa Siku ya Uhuru Afrika, iliadhimisha miaka 49 ya Siku ya Afrika na miaka 10 tangu kuundwa kwa Umoja wa Afrika (AU).

Siku hiyo nzima, waafrika na marafiki wa Afrika wamekuwa wakituma ujumbe kupitia mtandao wa twita kuhusiana na maadhimisho hayo.

@Chrisfordshind1: Ni siku ya uhuru wa Afrika. Lakini ninachokijua huwezi kuwa mjinga na bado ukawa huru kwa wakati huo huo, lakini kwa kuujua ukweli ni mwanzo wa uhuru

@Luyanda_Peter alipokea fulana ya kusherehekea Siku ya Afrika mwaka 2010. Picha ya mtumiaji wa twita @Luyanda_Peter

@Thagman_Hits: Si suala la kusherehekea tu “uhuru wa Afrika”. Ni kujiuliza swali “je ni kweli watu wanauona uhuru wa kweli?”

@laokov: Heri ya siku ya uhuru wa Afrika, lakini je ni kweli Afrika i huru?

@NikiMapoma: Habari za asubuhi ndugu zangu! Leo ni siku a Uhuru wa Afrika. Nimesoma mahali kwamba Zambia ni nchi pekee ambayo imeifanya siku hii kuwa ya mapumziko ya kitaifa kuwapa fursa raia wake kuadhimisha siku hiyo. Utaitumiaje?

@Thato_wally: Haiwezi kuwa furaha ya Afrika kama watu wetu bado wanaishi katika njozi za uhuru, kama ufisadi unaonekana kama desturi na jambo la kawaida…

@Pepuzani: Siku ya uhuru wa Afrika, nadhani kuna aina fulani ya uhuru wa kusherehekea. Uhuru wa kutumia Facebook.

@champoj: Msifanye makosa yale yale ambayo baba zenu walifanya. Jifunzeni kwao myafanye maisha yenu kuwa bora zaidi hata kama tunasherekea siku ya uhuru Afrika!

@Mutakala88: Ninasherekea Siku ya Uhuru Afrika kwa kusoma Rasimu ya Katiba ya Zambia #ZambianPride #fb

@khadijapatel: RT @khayadlanga: Kwa kuwa ni siku ya Afrika, hapa kuna hotuba kuu ya Thabo Mbeki “Mimi ni Mwafrika”. Jikumbushe tena kwa kutazama video hii http://bit.ly/LxspGq

@lead_sa: RT @williamwealth: @702JohnRobbie @lead_sa Je, u mwafrika awezaye au asiyeweza? Ninaamini tunaweza! Furahia siku ya Afrika!

@stwala20: Heri ya siku ya AFrika. Jamani tufurahie kuwa waafrika kwa kutunza utamaduni wetu. Endeleza uhuru wa kiuchumi ili bara la Afrika liendelee.

Kenyan Poet anadhimisha siku hii kwa ushairi:

Ilianza kama maono ya mtu mmoja,
Ndoto ya mwana mmoja,
Mwana wa Ghana, Nkurumah aliyeimba wimbo
Ambao maneno yake yameandikwa kwa damu ya ndugu zetu
Waliosafirishwa kwenda mashambani kama watumwa wa mabwana weupe
Wimbo ambao wizani na ala zilipigiliwa misumari
Na vilio vya watu wake
Miguu ikichechemea, mikono ikitetemeka, midomo ikilalama

Hatuwajui!
Hatuwajui wapigania uhuru
Wizani ya mijeledi migogoni mwao
Milio ya risasi ikitawala katika siku zichoshazo lakini zenye jua kali,
Usiku wa giza, lakini wenye mbalamwezi,
Sauti zimekuwa nyimbo za maombelezo katika masikio yao
Maafa, Maafa

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.