Tunisia: Mwaka 2011 katika Picha za Mitandao ya Kijamii

Makala hii ni sehemu ya habari zetu maalumu za Mapinduzi ya Tunisia 2011.

Mwaka 2011 haukuwa wa kawaida kwa nchi ya Tunisia – mwaka wa kihistoria ambao utaingia katika kumbukumbu za kila m-Tunisia. Kile kilichoanza kama kitendo cha mlipuko wa ubeuzi (kukata tama) kilichoanzia katika eneo lililosahauliwa na lililotengwa la Sidi Bouzid, kiligeuka kuwa maasi makubwa ambayo yangeikumba nchi hiyo, kuuangusha utawala wa miaka 23 wa Zeine el Abidine Ben Ali, na kubadili kabisa sura ya eneo hilo baada ya nchi za Kiarabu moja baada ya nyingine zikiambukizwa joto hilo la mapinduzi.

Mwaka ulianza kwa mauaji

Dead young Tunisian man in Tala (central-west of Tunisia), January 10, 2011. Photo from Nawaat.

Kijana wa ki-Tunisia aliyepoteza maisha yake mjini Tala (Magharibi ya Kati ya Tunisia), Januari 10, 2011. Picha kutoka Nawaat.

Mwaka ulianza kwa mauaji na vurugu. Tawala husika zilijibu madai ya waandamanaji ya “ajira, uhuru, na heshima ya taifa” kwa kutumia risasi za moto, mabomu ya machozi, mauaji ya zaidi ya waandamanaji 300 na kujeruhi wengine wengi zaidi.
Siku ambayo rais wa zamani alikimbilia Saudi Arabia

Photo by Talel Nacer, copyright Demotix (14/01/2011).

Picha kwa hisani ya Talel Nacer, haki miliki Demotix (14/01/2011)

Mnamo Januari 14, 2011, maelfu ya waandamanaji walikusanyika nje ya jengo la Wizara ya Mambo ya Ndani lililoko katika mji mkuu wa Tunis. Waandamanaji waliimba “Wizara ya Mambo ya Ndani ni Wizara ya Ugaidi”, na “Ben Ali Dégage” (Ben Ali Toka). Maandamano ambayo yalianza kwa amani, yaliisha kwa polisi kuwatawanya waandamanaji kwa nguvu. Baadae siku hiyo hiyo, Ben Ali alikimbilia Jeddah, Saudi Arabia.

Police use tear gas to disperse protesters outside the Interior Ministry on January 14. Photo by Wassim Ben Rhouma via Flickr (CC BY-NC-ND 2.0).

Polisi wakitumia gesi kuwatawanya waandamanaji nje ya Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 14 Januari. Picha ya Wassim Ben Rhouma kupitia mtandao wa Flickr (CC BY-NC-ND 2.0).

Dikteta ameondoka, lakini vipi kuhusu udikteta?

Protest against interim government presided by Mohamed Ghannouchi, a close ally of Ben Ali, on February 25. One day later, Ghannouchi resigned. Photo by Kahled Nciri.

Maandamano dhidi ya serikali ya mpito inayoongozwa na Mohamed Ghannouchi, mshirika wa karibu wa Ben Ali, tarehe 25. Siku moja baadae, Ghannouchi alijiuzulu. Picha kwa hisani ya Kahled Nciri.

Wa-Tunisia walikuwa makini kukata mifungamano yoyote na utawala ulioangushwa, vita kwa ajili ya demokrasia nchini Tunisia, haikumzuia Ben Ali kuikimbia nchi. . Kasbah square,lilipo jengo la Baraza la Mawaziri, likawa shabaha ya waandamanaji na wale wengine waliokuwa wamekaa, ambayo ilitafuta namna ya kukiangusha chama tawala cha kilichokuwa kimechukiwa sana (sasa kimesambaratishwa), RDC (yaani kwa vifupisho vya Kifaransa Le Rassemblement Constitutionnel Démocratique, kwa Kiswahili Mkutano wa Kikatiba na Kidemokrasia), ambacho kilihusishwa na ufisadi na unyanyasaji.

Uchaguzi wa kwanza wa Kidemokrasia

Voters lining up to vote. Photo by Erik (@kefteji).

Wapiga kura wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kupiga kura. Picha kwa hisani ya Erik (@kefteji).

Mnamo Oktoba 23, 2011, ndipo ilipowadia siku ya mageuzi kwa ajili ya Tunisia. Wapiga kura walisubiri kwa saa kadhaa ili kuwachagua wabunge, , katika uchaguzi wa kwanza ulio huru na haki kwa kile kinachoitwa Maasi ya Uarabuni.

Kuibuka kwa Waislamu wenye msimamo mkali

Banner reads: "Equality and justice for all Tunisians". November 21, 2011, in a protest outside the assembly. Photo by Soukaina W Ajbetni Rouhi via Facebook.

Bango linasomeka: “Usawa na haki kwa wa-Tunisia wote”. Mnamo Novemba 21, 2011, katika maandamano nje ya jengo la bunge. Picha kwa hisani ya Soukaina W Ajbetni Rouhi kupitia Facebook.

Chama chenye mrengo wa Kiislam Ennahdha kilishinda kwa asilimia 41 ya kura zilizopigwa, na kujinyakulia viti 89 kati ya viti 217 vya bunge la uwakilishi. Kwa waliberali, kuibuka kwa makundi ya Waislamu wenye msimamo mkali nchini Tunisia, ni tishio kwa tunu zisizo za kidini za nchi hiyo, na haki za wanawake wa ki-Tunisia, unaoaminika kuimarika zaidi katika eneo la Uarabuni.

Moncef Marzouki – Rais Mpya wa Jamhuri

Moncef Marzouki, new president of Tunisia. Image by Hamideddine Bouali, copyright Demotix (13/12/11)

rais mpya wa Tunisia. Picha kwa hisani ya Hamideddine Bouali, haki miliki Demotix (13/12/11)

Moncef Marzouki, Mnamo Desemba 12, bunge la taifa la kikatiba lilimchagua mwanaharakati wa haki za kibinadamu Moncef Marzouki, ambaye aliwahi kuwekwa jela, na kulazimishwa kuishi uhamishoni wakati wa utawala wa Ben Ali, kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Tunisia..

Wakati mwaka ukielekea kumalizika, waandamanaji na wale waliokuwa wakikaa mahali pamoja kushinikiza demokrasia, ajira, na heshima yanaendelea nchini Tunisia, kwa namna mijadala mikali ikifanyika kwenye bunge la nchi hii, na serikali ya mpito inayoongozwa na Hamadi Jebali (kutoka chama cha Kiislam cha Ennahdha) wakichukua majukumu yao.

Jiandae kwa habari zaidi kuhusu Tunisia kwa mwaka 2012.

Makala haya ni sehemu ya habari zetu maalumu za Mapinduzi ya Tunisia 2011.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.