Thailand: Utulivu Kabla ya Kimbunga?

Maandamano ya kuipinga serikali ya Machi 12 yalimalika salama huku kundi la Mashati Mekundu likiapa kurejea tena mitaani mwishoni maw juma hili ili kuendelea kushinikiza kuvunjwa kwa bunge na kuitisha uchaguzi mkuu.

Mashati mekundu wanapanga kufanya maandamano ya watu milioni moja mnamo Machi 14, Jumapili, ili kuipindua serikali iliyo madarakani.

Wengi katika kundi la mashati mekundu ni mashabiki wa Wazairi mkuu aliyetolewa Thaksin Shinawatra lakini siyo wote wanaomshabikia kiongozi huyo mtoro ambaye hivi karibuni mahakama iliamua kuwa ana hatia ya rushwa. Mashati mekundu wana mtazamo kwamba Waziri Mkuu wa sasa Abhisit Vejjajiva hana uhalali (wa kuwa madarakani) na si mwanademokrasia.

Maandamano ya Machi 12 mjini Bangkok na katika mikoa ya vijijini iliyo kaskazini yaliweka alama ya kuanza kwa mfululizo wa maandamano ya upinzani ambayo yamepangwa kutokea wikiendi hii. Serikali inakadiria kundi la watu 6,500 lakini waandalizi wa maandamano wanadai kuwa wamewandaa watu zaidi ya 30,000 mitaani.

Mashati mekundu wameahidi kutotumia vurugu katika maandamano hayo lakini video hii ya Youtube inaonyesha ugomvi baina ya mtu mwenye shati jekundu na dereva mmoja.

Video nyingine inaonyesha wanaodaiwa kuwa wanachama wa mashati mekundu katika kitendo cha kugawa pesa ili kukusanya waandamanaji.

Ni siku mbili tu kabla ya Siku ya Siku lakini wengi wa wakazi wa Bangkok wameamua kukaa mbali na maeneo makuu ya maandamano. Benki zilifungwa; dazeni za nchi zilitoa maonyo kwa wasafiri dhidi ya safari za kwenda Thailand wikiendi hii; na wakazi waliambiwa wasivae nguo za rangi nyekundu au za manjano “rangi ambazo zina ishara hai kisiasa” nchini Thailand. Mashati ya njano ni kundi linaloiunga mkono serikali.

Christopher Moore ameonyesha kuwa vyombo vya habari vya kisasa (uanahabari mpya) kuwa chanzo mbadala cha habari kuhusu hali ilivyo huko Bangkok

Katika Bangkok, wakati mwingi, ni vigumu kupata ishara mgando huru. Katika wakati mbaya zaidi, haiwezekani. Kuna kelele nyingi zinazoendelea katika mfumo. Televisheni na Redio bado viko chini ya udhibiti wa serikali na habari zinazotangazwa kwa kawaida huwa ni zile zinazoiunga mkono serikali. Lakini hakuna tena ukiritimba wa kutangaza habari. Intaneti, Twita, jumbe za maandishi kwenye simu za viganjani vimejaa moto kwa habari, uvumi, vitisho, maonyo na hofu. Mgongano wa jumbe hizo umepelekea kutokuwepo kwa uhakika na kuchanganyikiwa.

Tulichonacho hivi sasa ni hofu, hamu, hasira, chuki na kutoaminiana. Taarifa na ufahamu vinachujwa kupitia hisia hizi

Newley anaona kuwa hakukuwa na jambo la ajabu lililotokea tarehe 12 Machi mjini Bangkok.

Watu wengi hapa Bangkok walitarajia siku hiyo kuwa na vurugu. Biashara zilifungwa mapema. Shule zilisitisha madarasa. Na wakati kulikuwa na maandamano madogo madogo katika sehemu kadhaa za mji, ilikuwa tu kama siku nyingine yoyote katikati ya Bangkok.

Mashati Mekundu wakiandamana

Mashati Mekundu wakiandamana

Biashara na Uanaharakati

Biashara na Uanaharakati

Mitundiko ya Twita kuhusu maandamano ya Mashati Mekundu yanaweza kupatikana kupitia alama hizi: #redtweet, #rednews, #redmob, #redmarch, #redbuffalo, #stupidred, #redtail, #redshirt, #redbuff. Mwandishi anapendekeza #redtweet na #redshirt. Na hata Thaksin, ambaye anajificha katika nchi mbalimbali, ana akaunti ya Twita.

Haya ni baadhi ya maoni katika twita juu ya maandamano ya Machi 12

wisekwai Wanajeshi wanazunguka zunguka katikati ya Jiji Bangna. Vitambaa vyekundu, vyeupe na vya buluu kuonyesha utii wao. Si vya njano kama ilivyokuwa ’06. #redshirt
bangkokpastor Labda mimi ni mtu ninayeshuku mabaya. Sijashangazwa na vid kwenye wavuti wa taifa unaoonyesha wekundu wakigawa pesa. Wa manjano walifanya hivyo hivvyo. Nani anajali? #redshirt
tulsathit: “Walitegemea maelfu katika kila eneo la kukusanyikia, lakini viongozi wa maandamano waliweza kukusanya mamia katika kila kituo,” chanzo kilisema
Richard Barrow @michael_sp34 sikuhisi hofu wakati wowote leo. Kwa kweli walikuwa wakarimu na walikuwa na hamu ya kupigwa picha.
Richard Barrow: Wanasema kuwa kuwa magari ya mizigo na mabasi mengi ya #mashatimekundu yamekuwa yakisimamishwa na kukaguliwa katika vizingiti vya polisi jambo ambalo linawachelewesha

Mamia ya picha za Mashati Mekundu zinapatikana kwenye mtandao kwa hisani ya Richard Barrow.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.