Madagaska: Zaidi ya 25 Wauwawa Katika Maandamano Kuelekea Ikulu

Angalia ukurasa wa habari maalum kuhusu Mapambano ya kugombea nguvu za kiasiasa Madagaska.

Watu wapatao 25 walipigwa risasi na kuuwawa leo katika mji mkuu wa Madagaska, Antananarivo, wakati wa maandamano ya kuelekea ikulu ya nchi hiyo yaliyoitishwa na meya wa jiji Andry Rajoelina baada ya kujitangaza kama kiongozi wa serikali mpya ya mpito katika mkutano wa hadhara wa kisiasa. Katika majuma yaliyopita, ugombeaji wa nguvu za kisiasa kati ya Meya na Rais Marc Ravolamanana kumesababisha ghasia na uporaji.

Mkutano huo wa kisiasa ulifanyika katikati ya Mji wa Antananarivo majira ya mchana, saa za Madagaska. Rajoelina alitangaza kuundwa kwa serikali ya mpito, na yeye mwenyewe akiwa kiongozi wa serikali, bila kujali ukweli kwamba serikali iliyopo sasa bado inashikilia nafasi hiyo. Aliwataka watu wanaomuunga mkono waandamane kuelekea ikulu iliyopo Ambohitsorohitra.

Wakati umati mkubwa ulipowasili ikulu, wajumbe waliingia kwenye kasri majira ya saa 8:46. Ni wakati huu ambapo risasi zilirushwa. Watumaiaji wa twita waliokuwapo na wanablogu wengine waliripoti:

Habari za mwanzo zinaashiria kuwa dazeni za miili ilikuwa imenguka mitaani. Mooja wa majeruhi, inasemekana ni mpiga mpiga wa idhaa ya televisheni ya RTA (uthibitisho rasmi bado unasubiriwa).

Hadi majira ya saa 9:40 alasiri, risasi bado zilikuwa zinapigwa. Rajoelina, alilitaka jeshi la EMMONAT, linaloungwa mkono na pande zote ambalo liliundwa wakati wa mgogoro huu, kuingilia kati na kuulinda umma.

Habari rasmi (kwa mujibu wa Reuters, Al Jazeera) zinaeleza kuwa vifo vinafikia 25 kwa kadiri ya picha zinavyozidi kumiminika kwenye Televisheni ya taifa. BBC na AFP viliripoti vifo 5 tu. Habari kama zinavyotokea (katika wakati halisi) mtandaoni zinapatikana kwa lugha ya Kifaransa hapa.

Kuna kurasa za kutafiti za twita “#madagascar”, ambalo ndio neno-kiini ambalo watu wamekuwa wakilitumia wakati wote katika majuma yaliyopita ambayo yalijaa fukuto la kisiasa na ghasia za hapa na pale.


Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.