Msumbiji: 2038?

Msumbiji itakuwaje katika miaka 30 ijayo? Mwana sosiolojia Carlos Serra [pt] anatoa mitizamamo tisa ya falme zilizokufa za Kirumi yaani (Byzantine) na anawakaribisha wasomaji wake kurekebisha mitizamo hivyo kwa kadri ya wanavyoona ni sawa:

1. Lugha ya kireno itakuwa ni mabaki, itazidiwa na lugha ya kiingereza, itakayokuwa ikitumika kiufasaha katika maeneo ya mijini. Kireno kitakuwa lugha ya kisomi, itakayozungumzwa katika makundi mahususi, huku ikiungwa mkono na mchanganyiko mtamu wa lugha za kiholela katika sehemu za nyika.
2. Madini ya chuma yataendeshwa na Wachina, Warusi, Brazil, na hatimaye Wahindi. Bonde la Mto Zambezi litakuwa na migodi ya Wachina na Wa-Brazil.
3. Kama tukibahatika, patakuwa na mafuta, ambayo Wamarekani na Wakanada watakuwa wakiyavuna.
4. Misitu, kama itabaki, itamilikiwa na Wachina.
5. Itakuwa ni nchi ya nishati-mimea, itakayoendeshwa kwa biashara ya ubia wa namna mbalimbali, ikikumbatiwa na kilimo kidogo cha kuhamahama, kinachosaidiwa na maghala maalum ya nafaka yanayolindwa kwa ajili ya kusafirishwa nje (kwenda Uchina na India).
6. Biashara, ya jumla na ya rejareja, itatawaliwa na Wachina na Wahindi, kama-katika-urembo na mapambo.
7. Ulaya itamiliki fukwe za bahari za kitalii, zilizo na Wazungu-wa-Kimarekani watakaokuwa wanalilia na kukumbatia kumbukumbu za Ulaya inayokaribia kukata roho na Marekani isiyo-ubeberu.
8. Simu za mikononi zitakuwa zikitengenezwa ndani (Msumbiji), zikiwa na makasha ya Nokia na roho za Kichina, magari yatakuwa ya Kichina na Kikorea, yenye maumbo ya Kimarekani.
9. Wizara yetu itakayovutia zaidi, wizara-kabambe, itakuwa ni ile ya Biashara na Mambo ya Nje (Hebu angalia ukubwa wao wa sasa hapahapa jijini Maputo uweze kupata taswira ya itakavyokuwa huko mbeleni).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.