makala mpya zaidi zilizoandikwa na charahani
Saudi Arabia: Kina Mama Huru
WAKATI kukiwa hakuna shaka kwamba kuna vizuizi kwa wanawake waishio Saudi Arabia, havifanani na taswira iliyojengwa na wageni dhidi ya taifa hilo. Katika makala hii tunao ushauri kwa wakina mama wanaotaka kutembelea jiji la Jeddah wakiwa peke yao, kuna muhtasari wa hoteli za kina mama pekee jijini Riyadh, na wito kwa wageni wote wanajihisi kuzungumza kwa niana ya kina mama wanaokandamizwa wa Saudia.
Angola, Brazil: Mshituko na Utengano wa Kitamaduni
Mahusiano maalum kati ya Angola na Brazili yanamaanisha kwamba biashara kati ya makoloni haya mawili ya zamani ya Ureno inashamiri - kadhalika uhamiaji kutoka pande zote za Atlantiki. Lakini, ni vipi hawa watoto wawili wanavyoishi? Ujumbe huu unatoa mitazamo ya wote, kutoka kwa bloga wa Kiangola na wa Kibrazili waishio Luanda.
Arabeyes: Rais wa Mauritania Aliyepinduliwa Katika mapinduzi ya Kijeshi
MAKAMANDA wa jeshi wamemuondoa madarakani Rais Sidi Ould Cheikh Abdallahi, rais wa kwanza kuchaguliwa katika uchaguzi huru katika miongo miwili, katika mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa Jumatano iliyopita baada ya mtafaruku...
Msumbiji: 2038?
Msumbiji itakuwaje katika miaka 30 ijayo? Mwana sosiolojia Carlos Serra [pt] anatoa mitizamamo tisa ya falme zilizokufa za Kirumi yaani (Byzantine) na anawakaribisha wasomaji wake kurekebisha mitizamo hivyo kwa kadri...