· Oktoba, 2012

Habari kuhusu Marekani ya Kaskazini kutoka Oktoba, 2012

Je, Una Swali Lolote kwa Jimmy Carter?

  10 Oktoba 2012

Rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter anapokea maswali kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na Twita (#CarterQA) kama sehemu ya kuadhimisha miaka 30 ya Kituo cha Carter (Carter Center)...

Uarabuni: Sera ya Romney kwa Mashariki ya Kati Yaibua Mjadala

Hotuba ya Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Republican Bw. Mitt Romney iliyoelezea sera yake ya nje imeibua mjadala mzito miongoni mwa raia wa mtandaoni leo hasa wale watokao katika nchi za ki-Arabuni. Twiti zinazohoji sera ya mambo ya nje ya Marekani kwa Mashariki ya Kati ziliendelea wakati ambao Romney, anayepeperusha bendera ya chama cha Republican, alipozungumza katika Chuo cha Jeshi cha Virginia. Endapo atachaguliwa, Romney ameahidi kuwa na sera rafiki za mambo ya nje, tofauti na mwelekeo usiotabirika wa sera za Obama wakati huu ambapo mabadiliko ya kisiasa yanaendelea kulikumba eneo la Mashariki ya Kati.