Habari kuhusu Kiarabu
Misri: Kupandishwa cheo kwa Sissi ni ya Hutua ya Kuelekea URais?
Kupandishwa cheo kwa Abdel Fattah El Sissi hadi kuwa Jemadari Mkuu kumezua mjadala mkubwa katika mitandao ya intaneti, ambapo watu wengi wanawaza kuwa kama ndio njia yake ya kugombea Urais.
Misri: Kampeni kwa Ajili ya Haki za Watu Wenye Mahitaji Maalum
Wamisri pembezoni wenye mahitaji maalum wamekuwa wakifanya maandamano kwa haki zao kabla na tangu mapinduzi ya #Jan25. Hata hivyo, malalamiko yao bado hayajatatuliwa. Wakati Kamati ya watu 50 wanapiga kura juu ya rasimu ya hivi karibuni zaidi ya Katiba ya Misri, kampeni ya Zayee Zayak, ambayo hutafsiriwa kuwa “Mimi ni...
Mwanaharakati wa Misri Alaa Abd El Fattah Akamatwa — Tena
Mwanablogu mashuhuri na mwanaharakati Alaa Abd El Fattah alikamatwa jana jijini Cairo usiku wa Alhamisi. Wanaomwuunga mkono wanahisi amekamatwa kwa kutumia sheria mpya ya kuzuia maandamano.
Udadisi wa Sami Anan
Mwanablogu wa Misri Zeinobia anatoa maoni yake machache kuhusu kuibuka tena kwa Sami Anan, Mnadhimu mkuu wa zamani wa Majeshi ya Misri. Je, ana mpango wa kugombea urais? Mwanahabari wa Sauti za Dunia Mtandaoni Victor Salama anasimulia zaidi.
Misri: “Morsi Hatarudi Madarakani”
Aliyekuwa rais wa Misri Mohamed Morsi hatarudi madarakani, anasema mwanablogu wa Misri Alya Gadi, kwenye mtandao wa Twita. Kuufanya ujumbe wake wazi, ametafsiri kwa lugha mbalimbali: مرسي لن يعود – Morsi is not coming back – Morsi no va a volver – Morsi ne reviendra pas – Morsi kommt nicht zurück...
Wimbo wa Mahadhi ya Kufoka Upendwao na Vijana nchini Tunisia
Ukiwa umetazamwa zaidi ya mara milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube, wimbo wa Houmani umegeuka kuwa wimbo wa taifa kwa vijana wa Tunisia. Afef Abrougui anaeleza kwa nini,
Yemeni: Bundi Atua Nje ya Dirisha Langu
Mwanablogu wa Yemeni, Abdulkader Alguneid amkuta bundi nje ya dirisha lake: Kupitia mtandao wa Twita, anaelezea tukio hilo ambalo ni nadra sana kutokea: بومة كبيرة خلف زجاج نافذتي، 1.30 بعد منتصف الليل. Alikuwa Bundi mkubwa, nyuma ya dirisha langu la kioo, majira ya saa 7.30 usiku, tarehe pic.twitter.com/19WjfUelQ0 — abdulkader...
VIDEO: Shairi la Filamu “Maombi ya Woga” Latia Fora Misri
Mkusanyiko wa kiraia la Misri Mosireen umekuwa, bila kuchoka, ukiweka kumbukumbuza Mapinduzi ya Januari 25 na matukio yaliyofuata baadae kwa kutumia picha na dokumentari. Moja ya ubunifu wake wa mwisho mwisho ni “Maombi ya Woga”, shairi la filamu iliyotengenezwa na Mahmoud Ezzat na kusimuliwa na mwanachama wa Mosireen Salma Said....
Blogu na Uhuru wa Saudi Arabia
Saudi Arabia inasherekea Siku ya Uhuru tarehe Septemba 23. Wanablogu wanaeleza matumaini yao kwa taifa ambalo linaheshimu na kuthamini watu wake na matarajio yao.
Kubusiana Kwenye Mitaa ya Misri
Picha inayosambazwa katika mtandao wa Facebook inayowaonyesha vijana wawili raia wa Misri wakibusiana barabarani iliibua hasira na wengine kuipenda. Ilitolewa na Ahmed ElGohary, mtangazaji aliyepingwa kwa ‘kukosa utu uzima’ kwa sababu ya kuweka picha ya jinsi hiyo. Wengine walisifu uzuri wa picha hiyo na tafsiri yake kwa mapinduzi ya kiutamaduni. Kuonyesha mapenzi hadharanini si jambo linalokubalika nchini...