Habari kuhusu Kiarabu kutoka Januari, 2011
Misri: Habari Za Maandamano Ya Upinzani Moja Kwa Moja Kwenye Facebook
Habari za maandamano ya upinzani ya Januari 25 ya vuguvugu la la Vijana wa Aprili 6 zinapatikana kwenye ukurasa huu wa Facebook (Ar). Taarifa zimeibuka leo kuwa Facebook ilikuwa imezuiliwa isipatikane nchini Misri.
Dunia ya Uarabu: “Acheni Kulia Juu Sudani”
Kura ya maoni kwa ajili ya uhuru wa Sudani ya Kusini leo imeiweka nchi hiyo kwenye uangalizi wa karibu miongoni mwa watumiaji wa twita wa Kiarabu. Kuanzia Saudi Arabia mpaka Palestina, watumiaji Twita wa Kiarabu wanajadiliana kuhusu mshikamano, kugawanyika na rasili mali za Sudani.
Syria: Propaganda ya Vyombo vya Habari vya Serikali Kuhusu Maandamano ya Tunisia na Misri
Mwanablogu wa ki-Syria Maurice Aaek amegundua[ar] kwamba vyombo vya habari vinavyoendeshwa na serikali nchini Syria vinachapisha habari za uongo na nusu-kweli kuhusu maandamano ya upinzani nchini Tunisia na Misri. Amegundua kwamba gazeti la Tishreen daily halikuweka sababu ambazo zilimfanya Ben Ali aondoke na kuwaachia watu wajitafsirie wenyewe, na kuwa gazeti...