Wimbo wa Mahadhi ya Kufoka Upendwao na Vijana nchini Tunisia

Manao tarehe 14 Septemba, wasanii wa Tunisia Hamzaoui Med Amine na Kafon walitoa wimbo wao mpya ujulikanao kama ‘Houmani’. hadi sasa ukiwa na watazamaji zaidi ya milioni 3.4 katika mtandao wa Youtube, wimbo huu umekuwa kama wimbo wa Taifa miongoni mwa vijana nchini Tunisia.

Kipande cha video kilichogharimu takribani kiasi cha dinari 250 za Tunisia, karibu kiasi cha dola 250 za Marekani, inawachora watu wa daraja la chini kabisa nchini Tunisia na namna wanavyoendesha maisha yao.

Kwa lahaja ya watu wa Tunisia,msemo Houmani unatokana na neno Houma, ambalo lingeweza kutafsiriwa kama ‘mtaa wa wachapakazi’.

Ahd Kadhem kutoka Iraq afafanua maana ya neno Houmani [ar]:

حوماني: يعني يسكن بمنطقة شعبية والمنطقة الشعبية في تونس يسموها حومة . . . والرآب يتكلم على المناطق الشعبية إلي تجمع الطبقة الفقيرة من الشعب إلي نادر ما يذكرهم مسؤول أو شخصية مشهورة

Houmani lina maana ya mtu anayeishi katika eneo la wachapa kazi. eneo la tabaka la wachapa kazi nchini Tunisia hukulikana kama Houma… Na mziki huu wa kufoka unazungumzia mitaa hii ambayo huishi watu wa tabaka la chini na ambalo ni nadra sana kuongelewa na viongozi wa serikali na hata watu maarufu.

An Alien listening to Houmani. Carticature by

Zombi akisikiliza Houmani. Kikaragosi kimeandaliwa na ZOOart

katika wimbo huo, Hamzaoui na Kafon wanaelezea hali halisi ya maisha wanayokabiliana nayo vijana wanaoishi kwenye mitaa inayojulikana kama ya wachapakazi nchini Tunisia. Mashairi katika wimbo huu ni:

Tunaishi kama takataka kwenye pipa la taka…[Maisha] ni ya kubangaiza hapa

Mwanablogu Mehdi Lamloum anafafanua namna ambavyoHoumani ilivyokwishafanikiwa[fr]:

7oumani, une chanson simple, avec un titre étrange et un clip produit a peu de frais a créé des débats énormes ces dernières semaines…Et c’est ce qui est intéressant dans cette oeuvre. Elle est entrée rapidement dans la culture populaire en générant des conversations et débats sur plusieurs sujets…La question des quartiers populaires vs quartiers riches, même si elle n’est pas directement abordées dans la chanson, y est très présente. Une question a émergé a ce propos sur … qui a le droit d'écouter 7oumani?
Est-ce que les habitants des “quartiers riches”… ont le droit de s’identifier au quotidien que relate 7oumani?

Houmani, wimbo wa kawaida lakini wenye jina la ajabu na kiapnde cha video ambacho hakikuchukua gharama kubwa kuandaliwa, kimezua mjadala mkubwa katika wiki za hivi karibuni. Kwa haraka, wimbo huu umeshajikita katika utamaduni uliozoeleka kiasi cha kuzua majibizano na mijadala kadhaa…. suala la tabaka la wafanyakazi dhidi ya lile la watu matajiri, pamoja na kuwa halijazungumzwa sana katika wimbo huu, ni miongoni mwa mijadala inayoendelea kwa kiasi kikubwa. Kuhusiana na hili, kuna swali liliulizwa: ni nani mwenye haki ya kusikiliza Houmani? watu wa ‘tabaka la matajiri’ wana haki ya kujilinganisha na hali halisi ya maisha inayozungumzwa kwenye Houmani?

Anaongeza:

Ceux qui critique la chanson sur un point de vue musical ont parfaitement raison…
Mais ils devraient voir ce qu’il y a au-delà du morceau lui-même : une oeuvre qui a réussi a transcrire une partie de ce que ressentent les tunisiens, qu’ils viennent des quartiers populaires ou pas, qu’ils vivent le quotidien décrit ou pas…

Wale wanaoukosoa wimbo huu kwa mtazamo wa kimuziki wapo sahihi kabisa. lakini wanatakiwa kupata tafsiri sahihi ya wimbo huu: wimbo huu umefanikiwa kuwakilisha angalao hisia za watu wa Tunisia, bila kujali kama wanatokea mitaa ya watu masikini au wanaishi maisha yanayozungumzwa katika wimbo huu au vinginevyo…

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.