Habari kuhusu Kiarabu kutoka Juni, 2012
Misri: Yatambulisha Kipimio cha Morsi
Baada ya miaka 32 ya Hosni Mubarak, Misri imepata rais mpya Mohamed Morsi, na pia kitumizi cha kufuatilia utendaji pamoja na maendeleo ya kutimiza ahadi kuu 64 alizozitoa rais huyo mteule wakati wa kampeni za uchaguzi nchini humo.
Sudani: Kuondoa kizuizi cha Mapinduzi ya Sudani
Tofauti na nchi nyingine katika eneo lake, Sudani mara nyingi huwa haipati nafasi katika vyombo vikuu vya habari, na hili lilikuwa wazi zaidi wakati wa maandamano yalifanyika Ijumaa na Jumamosi. Sababu ni kwamba serikali ya Sudani imevibana mno vyombo vya ndani vya habari na kuwazuia waandishi kuripoti habari zinazohusu masuala ya haki za binadamu na ufisadi.
Sudani: “Polisi Yakanusha Kutumia Risasi; Majeruhi wote ni Wakufikirika
Maafisa wa serikali ya sudani wanarudia ‘uongo’ uliozoeleka ambao watawala wa ki-Arabu wamekuwa wakitumia tangu kuanza kwa yale yanayoitwa Mapinduzi ya Uarabuni yaliyoanza mwezi Desemba 2010. Imekuwa kawaida kusikia kauli kama, ‘waandamanaji wamedhibitiwa wakati wakiwashambulia polisi, ambao nao walijihami kwa kushambulia' Watumiaji wa mtandao wanaonyesha picha tofauti wakati tetesi zinadai mtandao wa intaneti utakatwa kufuatia kuongezeka kwa maandamano.
Sudani: Watumia Mtandao Wathibitisha Tetesi za Kukatwa kwa Intaneti
Raia wa kwenye mtandao wanaifuatilia kwa karibu Sudani, kufuatia tetesi kuwa serikali ya Sudani inadhamiria kuukata mtandao wa intaneti - hatua inayokumbushia jaribio la Misri kuwanyamazisha wanaharakati na kuthibiti mapinduzi ya Januari 25 pale ilipoondoa uwezekano wa watu kuwasiliana kwa mtandao wa intanenti mnamo Januari 27.
Misri: Maandamano ya Kukomesha Udhalilishaji wa Kijinsia Yavamiwa
Maandamano kudai kukomeshwa kwa udhalilishaji wa kijinsia yaligeuka kuwa shubiri baada ya wanawake waliokuwa wanahusika nayo kuvamiwa na kundi la wanaume wenye hasira kwenye viwanja vya Tahrir leo(June 8, 2012). Watu walioshuhudia tukio hilo walielezea maoni yao kupitia twita.