Mwanzo Mpya Kwa Malaysia Baada ya Wapiga Kura Kuuangusha Utawala wa Miongo Sita wa Chama Tawala

Kundi la waMalaysia la Bersih wakati wa moja ya kampeni zake za kutaka shughuli za  Uchaguzi ziwe huru na za Haki.  Chanzo:  Facebook

Baada ya miaka sita ya chama tawala cha Malaysia, Barisan Nasional (BN) kimeshindwa  katika uchaguzi Mkuu wa kumi na nne (GE14) hapo Mei 9, 2018.

Serikali ya BN iliongozwa na Najib Razak aliyehusishwa na kashfa za rushwa. Umaarufu wa Razak ulizidi kupungua pale alipojaribu kukandamiza madai ya uwazi na ukweli kuhusu tuhuma na kashfa za rushwa zilizomkabili.

Sasa Malaysia itaongozwa na  mzee wa miaka 92, Dr. Mahathir Mohamad aliyewahi kuhudumu kama waziri Mkuu kwa muda wa miaka 22 mpaka alipostaafu mwaka 2003. Alianza tena masuala ya siasa ili kukiongoza Pakatan Harapan (PH) Chama cha Upinzani katika kumkabili Razak na Muungano wa utawala ambao alishawahi kuuongoza.

Matokeo ya mwisho ya Uchaguzi Mkuu yanaonesha Wamalysia wengi kutokuridhishwa na utendaji wa serikali ya Razak. Wanamitandao wengi wa Malaysia walisherehekea habari za matokeo  ya kihistoria ya kura:

Katika siku yake ya kwanza ofisini, Rais mpya aliandika:

Alihapa kuchunguza vitengo vilivyohusika katika rushwa. Pia alilikubali ombi la wapinzani kuondoa sheria, kodi na mipango kandamizi.

Malaysiakini, tovuti huru ya habari, ilionesha umuhimu wa ushindi wa upinzani:

Hii ndio siku waMalaysia wanaona nguvu ya sanduku la kura.

Hasira dhidi ya uongozi wa sasa imewafanya watoke kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi wa 14 na wa kihistoria.

Hii ni mara ya kwanza nchi inashuhudia kubadilika kwa serikali tangu kupata uhuru toka kwa Waingereza hapo 1957.

Gazeti limechukua hatua ya kuikumbusha serikali mpya kuhusu mabadiliko ya msingi na ya haraka ili ‘kuiponya’ nchi:

Sasa uchapakazi umeanza. Hakuna anayepaswa kuwa chini ya udanganyifu kuwa serikali mpya itaweza kufuta uozo ambao umeota mizizi kwa miongo mingi.

Kwa nchi ambayo imegawanyika hivi, itachukua muda kupona majeraha na kwa waMalaysia kujenga imani baina yao na kwa taasisi zilizowakwaza.

Aliran, kikundi cha kijamii, pia  ilisherehekea  matokeo ya uchaguzi mkuu GE14 wakati ikiorodhesha baadhi ya changamoto  ambazo serikali mpya itakumbana nazo:

Aliran inawashukuru watu wa Malaysia walioinuka, wakashinda magumu yaliyokuwa mbele yao na kutumia kura na kufanya hili litokee. Tunawapongeza pia wanawake na wanaume ambao wamefanya kazi (wengi wao kwa miongo mingi) ili kuleta muamko ambao ulihitajika sana kwa mabadiliko haya.

Matokeo ya uchaguzi mkuu ni agano la nguvu ya watu katika kuleta mabadiliko. Ulimwenguni kote, Malaysia imeweka mfano bora- kwa Nguvu ya Umma na serikali kubadilishana madaraka kwa amani.

Serikali ya PH lazima ifanye kazi ya kubomoa taasisi nyingi ambazo ziliwaweka wala rushwa madarakani.  Hili pamoja na mengine, pia linahusisha kudhibiti nguvu ya serikali kuu na kuhuisha mamlaka nyingine ambazo ziliharibiwa kwa kuingiliwa vibaya na siasa.

Bandiko hiki la twita linajumuhisha hisia za wengi siku moja baada ya uchaguzi wa kihistoria GE14:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.