Masikini Nchini Jordan Wanaweza Kukosa Maji Juma Zima, Ilihali Matajiri Wanapata Maji muda Wote

Chumba cha Wadi, Jordan. Picha imepigwa na Treksjo. Imetumiwa kwa ridhaa.

Makala haya yametafsiriwa na mwandishi wetu mpya kabisa ndugu Matteo E. Mwita. Tunamkaribisha sana kwenye familia yetu ya Global Voices.

Jordan ni nchi ya pili kwa uhaba wa maji duniani . Mto Jordan ni moja ya vyanzo vyake vikuu vya maji ya juu ya ardhi, na ambao unatumiwa pia na nchi ya Israel. Chanzo kingine cha maji ni Mto Yarmouk,ambao pia unatumiwa na nchi ya Syria,hali inayopelekea nchi ya Jordan kuwa na mgao wa maji wa chini ya kiwango kinachohitajika

Linapokuja swala la vyanzo 12 vya maji vilivyoanishwa chini ya aridhi nchi nzima, uhimilivu wa vyanzo hivyo ni swala la kuzingatiwa kwakuwa kuna baadhi vinatumiwa kwa kiwango kikubwa na vingine vinatumiwa kupita kiasi, hali inayohatarisha matumizi ya simu zijazo.

Hali ya uhaba wa maji umezidishwa na uwapo wa watu milioni 1.4 zaidi waliokimbia vita Syria na wanaishi Jordani wakitegemea vyanzo vyake vichache vya maji

Na ukiangalia siku za mbeleni, mabadiliko ya tabia nchi yanafanya hali kuwa ngumu zaidi. Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Stanford wanatabiri kuwa mwishoni mwa karne, Joto nchini Jordani litapanda kufikia nyuzi joto la 4°C, na kutakuwa na upungufu mara tatu wa mvuap. Kwahiyo, Jordani, inatishiwa na ukosefu kabisa wa maji, wakati kiwango cha ukame kinatarajiwa kuwa mara mbili zaidi kati ya mwaka 2071 na 2100.

Japokuwa jitihada za wananchi ziko wazi, ila raia 9,903,877 wa Jordani, hawabebi mzigo sawa. Serikali kushindwa kupeleka maji baadhi ya maeneo mara nyingi kunahusishwa na hali ya kijamii ya eneo husika.
Sara Bader, mkazi wa zamani wa Amman eneo jirani la Al-Yasmine (eneo lenye wakazi wengi kupita kiasi) aliongea na Global Voices kuhusu uzoefu wake alipohamia Abdoun (eneo ambalo ni la watu wa hadhi ya juu):

tulikuwa tunapata maji mara mbili kwa wiki [in Al-Yasmine], wakati mwingine kipindi cha kiangazi yalikuwa hayatufikishi hata mwisho wa juma, kwahiyo tulikuwa tunafua na kutumia maji kwa matumizi mengine siku ambayo maji yalikuwa yanatoka. Tulikuwa makini sana na matumizi ya maji. Hapa [ Abdoun], maji yanatoka kila siku, na mama yangu hatengi tena ni siku gani afue kwa juma.

Inaweza ikaonekana sio sawa kwa baadhi ya maeneo maji kutoka kila siku huku kuna maeneo wanapata maji mara mbili kwa juma, ila ukweli ni kuwa kupata maji mara mbili kwa juma ni kama upendeleo ambao watu wa maeneo duni huutamani.

Kwenye maeneo masikini ya Amman, kwenye vitongoji, na hasahasa vijijini maji yanatoka baada ya siku 20, na kuna wakati hayatoki kabisa.
Kwenye barua iliyotumwa serikalini kulalamikia swala la maji, wananchi waishio katika kitongoji cha Jerash walisema:

Ninawasilisha malalamiko ya mamia ya watu kwako-watu ambao maeneo yao maji hayajatoka kwa siku 30 au 20 au 19.

Akaendelea:

Nina ushahidi kuwa baadhi ya mabomba hayajawahi kutoa maji zaidi ya mwaka kwakuwa mamlaka ya waji haijawahi kupeleka maji kwenye maeneo hayo hata mara moja kwa mwezi.

Maoni ya wananchi wenzake wa Jordani yanaonesha kuwa tatizo linawakumba watu wengi. Wengi walimshauri ahamie kwenye nyumba iliyokaribu na mwakilishi wa serikali au kwenye maeneo wanaoishi watu wenye hadhi ya juu ili aweze kupata huduma bora ya maji, kwakuwa maeneo hayo maji huwa hayakatiki.

Swala kwenye kitongoji hiki nikuwa kaya zina watu wengi, na wakaazi wengi ni wakulima wanaohitaji maji ili wamwagilie mazao yao
Jambo la kushangaza Serikali huwapelekea watu ankara za maji bila kujali kama watu hao walipata maji au la. Kipindi ambacho hawapati maji inawalazimu kununua maji kwenye malori yanayotoa huduma za binafsi za maji. Kwahiyo, wanalazimika kulipa ankara mbili za maji: ile iliyotolewa na serikali na ile ambayo unamlipa mtu binafsi akuletee maji.
Bei elekezi iliyopangwa na serikali kwa wauzaji maji kwa malori ni dinari 4 za Jordani (dola 6 za kimarekani kwa mita), ni kiwango ambacho wananchi wengi hawakimudu, kuna baadhi ya watoa huduma hizo huwapandishia bei wananchi wakati wa uhaba wa maji hadi dinari 5.

Ni sababu gani zinazofanya serikali kuyatelekeza baadhi ya maeneo lipokuja swala la huduma ya maji? Mfanyakazi wa wizara ya maji na umwagiliaji akiongea na GV kwa mashariti ya kutotajwa jina lake alisema:

Uhalisia ni tafauti na watu wengi wanavyofikiria: sio kuwa wizara ina upendeleo katika kugawa maji, ila maeneo duni yana miundo mbinu dhaifu na mabomba hayawezi kuhimili maji kutoka kila siku, mabomba mengi yametoboka na 2/3 ya maji hupotea kabla ya kufika eneo husika. Hiyo ndio sababu inayopelekea maeneo hayo kutopata maji muda wote, kwasababu wizara haiwezi kupoteza maji mengi kiasi hicho kila siku, kwahiyo maji hufunguliwa kila juma au baada ya majuma mawili, na mengi hayawafikii wananchi kwa sababu yanapotea njiani.

Alipoulizwa kwanini wizara haikarabati na kujiziba mabomba yanayovuja au kuyabadilisha kabisa, alisema kwasasa bajeti haiwezi kufanya hilo kipaumbele.
Hats hivyo, serikali imeahidi mgao sawa wa maji mwaka huu na kuwa wakati wote wa majira ya kiangazi majiya uhakika yatapatikana. Tuna matumaini kuwa serikali itatimiza ahadi yake — ukizingatia kuwa maji ni moja kati ya haki za binadamu
.
.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.