Baada ya Tishio la Ebola Kuondoka, Marekani Yalitaka Kundi La Wahamiaji Kutoka Afrika Magharibi Kurejea Makwao

Mkazi mmoja akitembea kati ya maeneo yaliyokumbwa na Ebola, pembeni ni ukuta uliochorwa picha zinazoashiri baadhi ya athari za virusi wa Ebola Tubman Boulevard mjini Monrovia, Liberia, mnamo September 18, 2014: Picha na: Morgana Wingard/UNDP. CC BY-NC-ND 2.0

Simulizi hili lililoandikwa na Maria Murriel hapo awali ilionekana katika ukurasa wa PRI.org mnamo tarehe 2 Juni, 2017. Imechapwa tena hapa kama sehemu ya ushirikiano baina ya PRI na Global Voices.

Mwishoni mwa mwezi Mei, Wahamiaji kutoka Afrika ya Magharibi takribani 4,000 waliokuwa wakiishi na kufanya kazi kihalali nchini Marekani  walipoteza haki zao za uhamiaji.

Awali walikuwa wakipewa hadhi ya uhamiaji kama sehemu ya kutimiza malengo mpango wa Marekani kuwasaidia watu kutoka nchi zenye migogoro, au TPS. Mwaka 2014, TPS ilipewa dhamana juu ya watu kutoka nchi za Liberia, Sierra Leone pamoja na Guinea kutokana mlipuko wa ugonjwa wa ebola.

Shirika la Afya Duniani limetangaza kwamba ugonjwa huo wa Ebola kwa sasa haupo. Sambamba na hilo mnamo tarehe 20  Mei, TPS imetoa tamko la muda wa mwisho kwa watu wa mataifa hayo, ikiwemo mwandishi wa riwaya kutoka Liberia kwa jina Paul, ambaye aliomba uhamiaji kwa jina moja tu ili kulinda umarufu wake.

Muda wake ukiwa umekwisha, Paul anaishi nchini marekani bila ruhusa  — lakini anasema n vigumu kwake na kwa watu w namna yake kurejea nchini Liberia.

“Ni vigumu kurudi kwa sababu hata fedha ya kulipia tiketi ya ndege hakuna,” anasema.

Miezi sitiliyopita, Idara ya Nchi Na Usalama nchini Marekani  (DHS) iliwajulisha wamiliki wa TPS kutoka nchi hizo tatu za Afrika Magharibi kwamba muda wao umefika ukingoni. Ilitarajiwa kwa muda uliobaki wangeutumia kujipanga kurudi makwao, kuepuka kuishi nchini hapo kiharamu pale muda utakapokoma.

Afrika Magharibi. Picha kutoka  Umoja Wa Mataifa.

 

Ingawa Paul anasema kuwa kuishi kwake Marekani kumemnyima uhuru wa kufanya kazi zake,kwa hivyo ameshindwa hata kujiwekea akiba ya nauli kwa safari ya kurejea nchini kwake sababu kubwa ni kupoteza umaarufu wake, ukitaka kutafuta kazi, waajiri wengi hawataki kukupa kazi ya kufanya wakati wote,” Paul anasema, “kwa sababu wanaona wewe ni mtu wa kupita tu, kwa mujibu huo hawataki kukupatia kazi  ya kudumu. Aa hii ni kati ya  vitu vinavyonitesa sana.”

Paul anasema alifanya kila kazi aliyoipata hata zisizo za kawaida, n baada ya miaka mimwili au mitatu, ameweza kutengeneza makazi yake hapo nchini amarekani. Anaishi Sacramento, California, pamoja na mke wake, ambae walikutana Marekani.

Ana watoto pia Liberia, lakini amekiri kwamba kuhamia kwake Marekani kulimgharimu awe na mahusiano mengine.

“Nilikuja, sio kwa ajili ya kukaa, haukua mpango wangu, lakini nikakaa kwa sababu ya migogoro, kwa hiyo nikapoteza mawasiliano,” akisema. “nikapoteza watu wangu.”

Paulo anasema hii ni moja kati ya dosari za TPS — kwamba serikali haikuzingatia je,wahamiaji watachangamana vipi na watu wa Marekani, hata kama watakaa nchini hapo kwa muda tu.

Jessica Vaughan, mpinzani wa TPS aliyejikita kwenye masomo ya Uhamiaji, mwenye mawazo ya msingi akiilenga  Washington, DC, anafikiri huu mpango wa TPS una dosari unawaruhusu watu kama Paul kuishi Marekani kwa kipindi kirefu kupita maelezo — ukipelekea watu hao kujifunga na kujenga mahusiano.

“Wengi wa namna hii wamekua wakiishi hapa na serikali imewaruhusu bila kuzingatia kwamba kwamba muda wao umekwisha,” Vaughan anasema. “[TPS inataka kufanana na] mlango wa nyuma wa kuhalisha watu kutoka mataifa mengine au mpango wa kuwasamehe kwa sababu ni wachache sana kati yao ambao walirejea makwao baada ya kupewa hifadhi ya halali kwa muda.”TPS ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 1990s, na baada ya hapo serikali ya   Marekani imekuwa ikiurejeza mpango huu kila mara baada ya miezi 18 wakizingatia misingi ya nchi baada ya nchi. Katika baadhi ya matukio, serikali imetoa mrejesho wa kila baada ya miezi sita — kama ilivyofanyika kwa Haitians hivi karibuni.

Corina Bogaciu akishirikiana na kamati ya kuhudumia Waafrika iliyopo  New York wamesema TPS imewachoka Afrika Magharibi mapema sana.

” Kiungwana kabisa,TPS imewapa muda mfupi mno,” anasema “Nchi nyingi huwa zilipewa muda wa vipindi vya miezi 18 viwili mfululizo ya nyadhifa za kukaa hapa Marekani, na baada ya hapo hurejea makwao.”

Liberia, Sierra Leone and Guinea walipewa muda upatao  miezi 18 tu, ikifuatiwa na vipindi viwili vya miezi sita ya nyongeza. Kwa sasa ambapo nyadhifa zao na TPS zimekwisha  muda wake  Bogaciu haina uhakika nini haswa kitafuata baada ya haya. Anasema ipo iddi kubwa ya watu kama Paul ambao hawajiwezi hata kugharamikia hata tiketi zao kurudi Afrika .

“Unapotakiwa kuondoka, serikali inapaswa kugharamikia safari yako,” alisema. “Lkini unapotarajiwa tu kuondoka, Lahasha! ni wajibu wako kujikusanya na kuondoka kwa wakati na ukienda kinyume, utakuwa unaishi hapa kinyume cha sheria na hatutakutambua.”

DHS ilisitisha maombi ya mahojiano, badala yake wakahamisha kwa  PRI's Tovuti ya dunia.

Bogaciu nasema baadhi ya watu anowahudumia waliopoteza nyadhifa  TPS wametandwa na hofu kubwa kwamba pengine serikali utekelezaji wa wao kuhamishwa nchini humo.Huku miongoni mwao wakitafuta nmna mpya ya kujilinda kwa fomo za matibabu.

Mit Philip, mchambuzi wa sera kutoka kundi la madaktari wasio na mipaka , ingwa kwa sasa ugonjwa wa Ebola haupo tena Afrika Ya Magharibi, bado umeacha athari kubwa itakayoendelea kuleta hali tete kwenye mfumo mzima wa nchi hizo.

“Ndani ya kipindi cha miaka miwili ya Ebola, huduma za kiafya zilidorora, bila pingamizi,” Philips anasema. “Sambamba na hilo watu walijawa na hofu kubwa kusogelea vituo vya afya kwani palionekana kama ni mahali ambapo unaweza kujipata maaambukizi ya ugonjwa huo wa Ebola.”

Hofu iliyotnda imepelekea watu kutopata chanjo, na imenukuliwa mwanzoni kabisa mwa mwaka huu Guinea, ilikubwa na mlipuko wa ugonjwa wa surua. Philips alisema kwa sasa Liberia inasumbuliwa na homa ya uti wa mgongo .

“Ingawa janga la Ebola limefikia tamati … kama ilivyotangazwa,” Philips anasema, “bila shaka sio Ebola tu katika sekta ya afya [ambapo TPS hawani budi kukabiliana nayo ]. … vilevile itategemea sana jinsi gani wataweza kuepuk bila kuenea zaidi kwa maambukizi na kulinda hali ya usalama katika sekta hiyo kitaifa kwenye nchi husika .”

Baadhi ya ndugu wa Paul walikuwepo miongoni mwa waathirika wa ugonjwa wa Ebola mwaka  2014, lakini hofu yake kubwa kurudi nchini Liberia haitokani na hali ya usalama kiafya bali. mustakabali wa ajira yake.

Ingawa sio rahisi kupata kazi ya kudumu Marekani, walau anaweza kupata kibarua cha muda, anasema.

“Sio kitu rahisi kupata jira nikiwa Liberia,” anaeleza” Sio kama Marekani ambapo ninaweza kupata ajira ya muda. [Hapa] tuna mawakala wanaoweza kukusaidia katika swala zima la ajira. Utaratibu ambao haupo Afrika, mahususi kwenye nchi yangu.”

Mke wa Paulo ni mzaliwa wa Marekani. Walikubaliana kukaa wote mwaka 2006, lakini makubaliano yao yalikataliwa. Hadi watume maombi kwa awamu nyingine, Paulo hana nyaraka zinazohitajika. Hawezi kupata kazi halali ya kudumu, na hawezi kurudi Liberia

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.