Shindano lililoanzishwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, #UhuruDabChallenge, kuwahamasisha vijana kujiandikisha kupiga kura limekwama baada ya watumiaji wa mitandao ya kijamii kulitafsiri kama ishara ya kukosa kipaumbele kwenye utawala wake.
Shindano hilo linawahitaji vijana ‘kucheza dab’ —miondoko ya dansi inayofanana na kupiga chafya kwenye kiganja chako —kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura na kuweka picha zao wenyewe kwenye mitandao ya kijamii. Wa-Kenya watapiga kura Agosti 8, 2017.
Twiti iliyokuwa kwenye akaunti rasmi ya Uhuru Kenyatta kuhusu kampeni hiyo ilisema:
The winner of the Dab challenge, whether it is a group or individual with the most retweets at the end of the remaining five days of voter registration, will be rewarded for their patriotism, including visiting with me at State House.
Mshindi wa shindano la Dab, iwe ni kikundi au mtu mmoja moja atakayekuwa na twiti itakayosambazwa mara nyingi zaidi mwishoni mwa siku tano zitakazobaki za zoezi la kuandikisha wapiga kura, atatuzwa kwa uzalendo wake, ikiwa ni pamoja na kunitembelea hapa Ikulu [ya Nairobi].
Na kama sehemu ya kampeni hiyo, Kenyatta alirekodi video ya miondoko ya dab akiwa Ikulu na wacheza dansi maarufu nchini humo wanaoitwa FBI.
Hata hivyo, watumiaji wa mtandao wa Twita waliohamasishwa na alama habari hiyo walianza kutuma maoni ya kukosoa kwa kutumia alama habari ya #DabOfShame. Wa-Kenya walishangazwa inakuwaje rais aliweza kupata muda wa kurekodi video ya muziki wakati nchi ikikabiliwa na matatizo makubwa ya kijamii na kisiasa kama vile njaa, ukame, kufa kwa mifugo na migomo ya kitaifa inayofanywa na wahadhiri wa vyuo vikuu na madaktari.
Kufuatia zoezi hilo la kupinga kampeni hiyo, twiti na picha zote zinazofanana na alama ishara ya kampeni hiyo (ikiwa ni pamoja na ile iliyotajwa hapo juu) zilifutwa kwenye akaunti ya twita ya Rais Kenyata.
Pamoja na kufuta twiti hizo, baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Twita kama vile Dikembe walichapisha picha za twiti hizo na kuzisambaza mtandaoni kwa kejeli.
President Uhuru DELETED these tweets! Should we have a law prohibiting deletion of presidential archive? #DabOfShame #UhurudabChallange pic.twitter.com/kPEp4eiajn
— Dikembe (@Disembe) February 11, 2017
Rais Uhuru FUTA twiti hizi! Jamani, hatuwezi kuwa na sheria ya kuzuia kitendo chochote cha kufuta kitu kwenye kumbukumbu za rais?
Akionesha kupinga shindano hilo, Master Chengo alichapisha picha mbili zinazoonesha tofauti kati ya mwondoko wa dab wa rais na mwondoko wa dab wa wananchi wa kawaida:
Let 2017 be the Year Of Redemption.
Presidential Dab v/s Common Mwananchi Dab. #TheyarebothDabbing #TheDifferenceIsNotTheSame#DabOfShame pic.twitter.com/fbcLBT8aGn— Master Chengo (@MOGULinfluencer) February 11, 2017
Mwaka huu 2017 uwe wa Ukombozi.
Linganisha mwondoko wa Dab wa Rais na Mwondoko wa Dab wa Mwananchi wa kawaida
Video ifuatayo iliyochukuliwa kwenye kituo cha televisheni cha Kenya NTV inamwonesha rais Kenyatta akicheza na kikundi cha dansi cha FBI:
Elia Muriuki alibainisha:
#UhuruDabChallenge in for a rude shock after being turned down by pissed Kenyans. It turned into #DabOfShame Tia bidii #Sir_presidente
— Elias_Muriuki (@iam_muriuki) February 12, 2017
Shindano la Dab la Uhuru limekumbwa na dhoruba baada ya kukataliwa na wa-Kenya wenye hasira. Limegeuzwa kuwa Dab ya Aibu. Tia bidii mhe Rais
Mark Wuon Odhis alilalamika:
Kenyans are suffering with this drought and all we are asked to do is dab #DabOfShame
— Mark Wuon Odhis (@makoth) February 11, 2017
Wa-Kenya wanakabiliana na ukame mbaya, ambao rais ameutangaza kuwa janga ;a taifa.
Silas Okumu alitania:
#DabOfShame after dubbing next is twerking… we shall do it now that drought is a national disaster.
— Silas Okumu (@sokumu58) February 11, 2017
Dab ya aibu baada ya kucheza dansi la dab, kinachofuata ni mwondoko wa twiki…tutafanya hivyo sasa ambapo ukame ni janga la taifa
Twiki ni aina ya dansi ambayo mtu hucheza muziki kwa namna ya kimapenzi.
Wakati Kibii Eliud alimwuuliza rais:
Mr President, how about dabbing off clashes in Kerio Valley and Laikipia? https://t.co/MAOiwIUkWT via @TheStarKenya #DabOfShame
— Kibii Eliud (@eliudkibii) February 11, 2017
Mhe Rais, unaonaje tutumie miondoko ya dab kumaliza mapigano kwenye eneo la Kerio Valley na Laikipia?
Kumekuwa na mfululizo wa mapigano kwenye eneo la Kerio Valley yanayohusishwa na ujambazi wa kutumia silaha na wizi wa ng'ombe na hivyo kusababisha vifo vya watu kadhaa.
Akaunti ya Twita inayotumiwa na mtu anayejiita mtoto wa Kenyatta ilitania:
Stop exaggerating what My Dad did, as a President he has to use Entertainment Allowance well. #UhuruDabChallenge pic.twitter.com/j1qtJHEKzH
— Uhuru Kenyatta Jnr (@UkenyattaJr) February 12, 2017
Msikuze sana yale yaliyofanywa na Baba Yangu, kama Rais lazima atumie vizuri Posho ya Burudani
Hata hivyo, kuna wa-Kenya kama vile Yobra Silver aliyekuwa anaunga mkono kampeni hiyo. Aliandika:
#DabOfShame
Good president
It is good to know he also appreciates the youth— yobra_silver (@yobra50100) February 11, 2017
Rais mzuri. Inapendeza kujua kuwa na yeye anawakubali vijana
Mtumiaji mwingine wa Twita aliandika:
#UhuruDabChallenge wow! HE Uhuru me and my hommies are dabbing????
— saidamilan (@saidamilan) February 10, 2017
Wera! MHE Uhuru mimi na familia yangu tunacheza dansi la Dab
Na Annie alikuwa na maoni yafuatayo:
Its only in Kenya that a president is not supposed to dab, laugh or have some good time~smh #UhuruDabChallenge
— Annie (@matrevor) February 10, 2017
Ni Kenya pekee ambapo rais hatakiwi kucheza dab, kucheka au kufurahia maisha