Hofu ya Mkono wa Sheria? Kujitafutia Uhuru? Raia wa Gambia Wahoji Nchi yao Kujiondoa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai

Gambian President Yahya Jammeh who has been in power since 1994 is widely accused of human rights violations. Public Domain photo by the White House uploaded online by Wikipedia user Alifazal.

Rais wa Gambia Yahya Jammeh ambaye yopo madarakani tangu mwaka 1994 anatuhumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Pich akwa hisani ya Ikulu iliyopakiwa na mtumiaji wa Wikipedia Alifazal.

Kufuatia tangazo la kusitisha uanachama katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai(ICC), Raia wa Gambia waonesha kutokukubaliana na sababau za serikali yao za kujiondoa. Wanaharakati na raia wa kawaida waishio ndani na nje ya nchi wanajadili yale wanayodhani ndio sababu “kuu” zilizopelekea serikali yao kuamua kusitisha uanachama wa ICC.

Serikali imeishututumu ICC kwa kuonesha upendeleo kwa kuwalenga zaidi viongozi wa Afrika kuliko wale wa mataifa ya Magharibi. Alipokuwa akitoa taarifa ya kuachana na mahakama hii, Waziri wa Mawasilianmo wa nchini Gambia Sheriff Bojang alisema kwamba ICC ni “Mahakama ya wazungu iliyo na lengo la kuonea na kudhalilisha watu wa rangi nyingine na hususani Waafrika.”

Uamuzi huu umekuja mara baada ya nchi za Afrika Kusini na Burundi kusitisha uanachama wa ICC.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, ICC imeshafungua mashitaka yanayohusisha nchi nane – ambazo zote ni za mataifa ya Afrika isipokuwa nchi moja tu. Mapema mwaka huu, wanachama wa Umoja wa Afrika waliunga mkono pendekezo la Kenya la kutaka kusitisha uanachama wa ICC.

Mgombea binafsi wa kiti cha Urais Dr. Isatou Touray katika mkutano na waandishi wa habari alishutumu kitendo cha serikali ya Gambia kusikitisha uanachama wa ICC na kusema kuwa uamuzi huo uliwakilisha aina ya uongozi wa Rais wa sasa Yahya Jammeh:

Ndugu zangu raia wa Gambia kushitishwa kwa uanachama wa Gambia kwenye ICC, kama ilivyokuwa kusitisha uanachama wa Jumuia ya Madola mwaka 2013, ni jambo lisilo la kikatiba linalo na kwa mara nyingine linaonesha ni kwa kiasi gani uongozi wa Rais Jammeh umeshindwa kuheshimu katiba na sharia za nchini Gambia.

Dr. Touray, mwanaharakati wa haki za binadamu ndiye mwanamke wa kwanza nchini Gambia kuonesha nia ya kugombea kiti cha Urais. Uchaguzi wa Rais utafanyika nchini Gambia tarehe 1 Disemba, 2016. Mwezi Oktoba 2013, nchi ya Gambia ilijiondoaleft kwenye Jumuiya ya Madola, kwa kile ilichokiita “kuendelea kusujudu ukoloni”.

Hata hivyo, kwa Mama Linguere Sarr, mwandishi wa habari na mwanaharakati aishiye huko Swedenyeye anaona kuwa Gambia imejiondoa ICC kwa kuogopa mkono wa sharia. Mwezi Septemba 2016, Rais Jammeh alimuachisha kazi waziri wake wa mambo ya ndani na rafiki yake kipenzi wa muda mrefu Ousman Sonko. Muda mchache mara baada ya kuachishwa kazi, Ousman Sonko, anayesemekana kutaka kuuawa na maafisa usalama wa serikali na hivyo kulazimika kutokomea na kutafuta hifadhi nchini Sweden.

Hata hivyo, baadhi ya watu wanakubaliana na uamuzi wa serikali wa kujiondoa ICC wakisema kuwa huu ni mpango wa kujitafua uhuru kamili. Katika ukurasa wake wa Facebook Benjamin Mpofu aliandika:

Huu ni mfumo mahakama wa kizungu ulioandaliwa kwa lengo la kuendeleza mfumo dhalimu wa mahakama na wa kibaguzi na kwamba hali hii inanikumbusha miaka ya 50 na 60 pale makoloni ya enzi hizo yalipokabiliana vikali na wakoloni, angalao ilikuwa fadhali kwa wakoloni kufifishwa nguvu kulikosababishwa na vita vya duania. Hali ya sasa ya kutizama upya uhusiano wa kisiasa kati ya mataifa mbalimbali ni wakati muafaka kwa Afrika kuzingatia vipaumbele vyake. Mpango wa kutafuta uhuru kwa ujumla wake hauna budi kuanza na kwa kuanziaICC iwe mfano

Lakini kwa mwanasheria Malick Jallow, maamuzi ya nchi za Kiafrika kujiondoa ICC hayana sababu za msingi. Aliandika:

Nimefuatilia mijadala ya hivi karibuni kuhusu matamko ya kujiondoa ICC kwa baadhi ya nchi za Kiafrika, ikiwa ni pamoja na Gambia. Matamko mengi yanathibitisha mtazamo wa muda mrefu sana kuwa ICC pamoja na Haki za Kimataifa za Makosa ya Jinai pengine ni mambo yasiyofahamika kabisa barani Afrika.

Mwendesha mashitaka wa ICC, Fatou Bensouda, ambaye ni raia wa Gambia, aliwahi kuzungumzia suala la nchi za Afrika kujiondoa ICC. “Hatuna budi kuwa imara,” Bensouda aliwaambia waandishi wa habari wiki iliyopita akiwa Hague. Kabla ya kupata wadhifa kama mwendesha mashtaka wa ICC, Bensouda aliwahi kufanya kazi kwenye serikali ya Rais Jammeh kama waziri wa sharia mwaka 1998, alitumikia pia serikali akiwa kama mshauri mkuu wa serikali kwenye masuala ya sharia. Hata hivyo, aliondolewa miaka miwili baadae.

Nnchi ya Gambia bado haiwasilisha nyaraka kwa ajili ya kuanza mchakato rasmi wa kujiondoa ICC, hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa msimo huu utaendelea kuwa hivi kwa taifa change hili la Afrika Magharibi. Kwa miaka kadhaa, Gambia imeendelea kuhamisha mtazamo wake kutoka ule wa kimagharibi kwenda mrengo wa kimashariki. Mwaka 2016, nchi hii ilifungua ubalozi wake huko Urusi pamoja na kurejesha tena uhusiano wake na nchi ya China (nchi zote hizi si wanachama wa ICC)

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.