Duterte ni Nani? Mjadala wa Kina

Alimwita Papa Mtakatifu mtoto wa kahaba. Alimwita Rais wa Marekani Obama mtoto wa kahaba. Amefananishwa na Trump. Amefanya utani kuhusu ubakaji na hafichi tabia yake ya kupenda wanawake. Ndani ya miezi minne, vita yake dhidi ya madawa ya kulevya imeua maelfu ya watu wanaotuhumiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya na kuwa na uraibu wa madawa hayo.

Lakini hayo yote ni upende mmoja tunapomzungumzia Rais wa u-Filipino Rodrigo Duterte.

Kwenye kipindi cha wiki hii cha Kwa Kina , kipindi kipya cha Global Voices kinachochimba suala moja ambalo halipewi uzito na vyombo vikuu vya habari, waandishi wa Global Voices Mong Palatino na Karlo Mongaya wanatusaidia kuelewa upande mwingine wa Duterte.

Katika kipindi hiki, tunasindikizwa na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music, ikiwa ni pamoja na nyimbo za Blue Dot Sessions zinazoitwa Ray Gun – FasterFasterBrighter na Under Suspicion wa Lee Rosevere.

Picha kuu kwenye habari hii imepigwa kwenye mchezo maarufu wa simu za kiganjani unaoitwa Fighting Crime [Fambana na Uhalifu]. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.