Bodi ya Shule ya Msingi Fatumeta katika kitongoji cha Dili imeamua kuweka sheria zitakazo wabana wanafunzi watakaoongea lugha nyingine tofauti na Kireno ikiwemo Kitetumi wawapo katika mazingira ya shuleni.
Kutoka kwa gazeti la Timor Post, mkurugenzi wa shule hiyo Fernanda Belo, anasema kuwa wanafunzi ni lazima waongee Kireno pekee wawapo shuleni. Wanafunzi mbao “hawataweza kuongea lugha hiyo” watalazimika kukaa kimya. Kwa mujibu wa gazeti hilo, mwanafunzi akikamatwa akizungumza lugha tofauti na Kireno “atapigwa faini”. Ikiwa imeandikwa Kitetumi, gazeti la Timor Post limemnukuu Belo akisema kuwa:
Ami ko’alia ona ho inan-aman katak alunus sira tama iha resintu eskola ne’e labele ko’alia tetun, hotu-hotu ko’alia lian português, sé maka ko’alia tetun sei multa dollar 1
Tumeeleza hii sheria kwa wazazi na tumeweka msimamo kuwa wanafunzi hawataongea Kitetumi, kila mmoja lazima aongee Kireno. Kama mwanafunzi ataongea Kitetumi atapigwa faini ya dola moja.
Mkurugenzi wa shule hiyo anasisitiza kuwa “wazazi wamekubaliana na sheria hiyo” na kuafiki kupitisha faini hiyo ili kuwasaidia wanafunzi waweze kuongea Kireno zaidi.
Baada ya kupata Uhuru wake kutoka kwa Indonesia mwaka 2002, Timor-Leste iliamua kutumia Kireno na Kitetumi kama lugha rasmi ya Taifa. Muongo mmoja baadaye, tafiti zinaonesha kuwa ni asilimia 15% pekee ya watundio wanaoongea Kireno:
Apesar de fazer parte da CPLP, Timor-Leste é um dos países com menor penetração da Língua portuguesa. Por todo o território falam-se cerca de 20 línguas e dialetos para além do Indonésio. Apenas 15% da população fala Português.
Pamoja na kuwa sehemu ya CPLP, Timor-Leste ni moja ya nchi ambazo Kireno kinapenya kwa kiwango cha chini kabisa. Kwa nchi nzima kuna karibu lugha 20 tofauti zinazozungumzwa ukijumuisha na Kiindonesia. Asilimia 15% tu ya watu ndio wanaozungumza Kireno.
Pamoja na hayo, inaonesha kuwa sheria za shule ya Msingi ya Fatumeta zinavunja sheria za nchi katika ufundishaji. Raisi wa Alola Foundation na balozi wa matumaini mema kwa ajili ya masuala ya elimu Kirsty Sword Gusmao,ameiambia Global Voices kuwa taratibu za kuwapiga faini wanafunzi wanaoongea Kitetumi zimepitiwa:
Ha'u sei refere asuntu ida ne'e ba Sra Vice-Ministra Ensinu Báziku tanba regra/sansaun hanesan ne'e la han malu ho Dekreto Lei kona-ba Kurrikulu Foun Ensinu Baziku nian.
Nitalipeleka jambo hilo kwa Naibu Waziri wa Elimu ya Msingi kwa sababu sheria hii haiendani na sheria za Mtaala wa Elimu ya Msingi [wa Timor-Leste].
Gusmão anaelezea kuwa:
Sra Diretora Eskola Fatumeta ne'e mak tenke simu multa tanba viola Dekretu Lei 4/2015 Kurrikulu Ensinu Báziku ne'ebé determina: a) prosesu hanorin lian tenke hahú ho oralidade no depois mak hakat ba lee no hakerek (art. 11-1) b) progresaun husi Tetun ba Portugés (hahú hanorin literásia Tetun) (art. 11-2) c) karga oráriu literasia Tetun no Portugés iha siklu 1 la hanesan (Tetun mak barak liu) no iha siklu 2 hanesan d) objetivu final aprendizajen komponente literásia atu iha báze mak’as lian ofisiál rua (art 11-2) (la iha objetivu atu hanorin lian inan/nasionál seluk) e) uza lian instrusaun sei lalenok progresaun (hahú lian instrusaun ne’ebé uza mak Tetun no depois mak hahú móis hanorin komponente kurrikular seluk ho lian Portugés (art. 14-2 no 3) Viva lian-Tetun!
Mkurugenzi wa shule ya Msingi Fatumeta ndie anayetakiwa kupigwa faini kwa kuvunja sheria iliyopitishwa 4/2015 ya Mitaala ya Elimu Msingi iliyohitaji yafuatayo (a) Hatua za kujifunza zitaanza kwa kuongea na kisha kusoma na kuandika kutafuata (b) Muendelezo wa kutoka Kitetumi kwenda Kireno ( utaanza kwa kutoa elimu ya Kitetumi) kifungu cha 11-2); (c) Masaa ya kujifunza Kitetumi na Kireno kwa mzunguko wa kwanza hayalingani ( ya Kitetumi yatakuwa juu kidogo) na katika mzunguko wa pili masaa yatalingana (d) ili kumalizia muundo wa mafunzo itahitaji kwanza kuwekwa kwa msingi wa lugha hizi mbili rasmi (kifungu 11-2) (hakuna haja ya kufundisha lugha mama au lugha nyingine ya Taifa). Iishi milele lugha ya Kitetumi!
Pia Global Voices tulizungumza na João Paulo Esperança, mtaalamu wa lugha ya Kireno ambaye ameishi Dili kwa miaka mingi. Esperança anasema kuwa hali katika shule inahitaji kuthibitishwa na kisha mrejesho unaweza kuhitajika au usihitajike inategemea kama kuna umuhimu:
Penso que primeiro há que confirmar qual é a situação real nesta escola, mas eu, pessoalmente, não concordo com políticas escolares que proíbam os alunos de falarem a língua que quiserem no recinto escolar, fora da aula. E pode haver também famílias sem possibilidades económicas de pagar estas multas. Mas creio que não é com má intenção que alguns diretores e professores tentam implementar medidas destas. Antigamente as escolas em Timor usavam muito os castigos corporais, a língua de ensino era o português e, depois da invasão, o indonésio, e os alunos eram punidos fisicamente por falarem outras línguas; era essa a experiência pessoal da maior parte das pessoas, mas a pedagogia moderna recusa que se possa bater aos alunos, por isso alguns professores tentam usar essas multas como um castigo alternativo. Quanto à tentativa de criar uma escola de imersão em língua portuguesa, isso terá provavelmente a ver com o facto de as escolas vistas como modelo em Timor também o serem, e isto inclui, por exemplo, a Escola Portuguesa, as Escolas de Referência e o mítico Externato de São José. Aliás, ultimamente tem surgido uma tendência que nos devia fazer pensar: muitos pais da classe média-alta que não conseguem vaga nessas escolas de imersão em língua portuguesa aqui em Díli estão a colocar os filhos em escolas filipinas de imersão em língua inglesa.
Kwanza kabisa tunatakiwa tuthibitishe hali halisi katika shule hii, lakini mimi binafsi sihafikiani na taratibu za shule zinazozuia wanafunzi kuzungumza lugha wanayotaka kuitumia katika mazingira ya shule, nje ya darasa. Na zinaweza kuwepo familia ambazo hazina namna ya kulipia faini hizo. Lakini nadhani sio kwa nia mbaya Mkuu wa Shule na waalimu wanapojaribu kutekeleza sheria hiyo. Hapo nyuma shule za Timori zilitumia adhabu kali, na lugha ya kufundishia ilikuwa ni Kireno ( na baada ya uvamizi wa Indonesia, ilikuwa ni Kiindonesia)na wanafunzi waliadhibiwa vikali kwa kuongea lugha nyingine. Hii ilikuwa kitu wengi walipitia lakini Mtaala wa kisasa unakataa hatua hizo za kizamani hivyo baadhi ya waalim wanajaribu kutumia hizo faini kama njia mbadala ya kuadhibu. Kwa kuangalia jaribio hili la kuanzisha shule maalum zinazotumia Kireno kisichotumiwa kabisa na wenyeji, labda sababu ni kwamba shule, kama ile inayoonekana kuwa mfano bora kule Timor inayoendeshwa sawa sawa na shule za Kireno, Shule zenye Ubora ambao hata hivyo haupo kama vile Externato S. José zinambana kila mtoto aongee Kireno anapokuwa darasani [bila faini]. Na hili, katika siku za karibuni, limesababisha mtindo mpya unaotufanya tutafakari kulikoni. Matokeo yake wazazi wengi wenye kipato cha juu kidogo kwenye kitongoji cha Dili, ambao watoto wao hawawezi kupokelewa kwenye shule hizi zinazofundisha kwa lugha ya kigeni ya Kireno, wanaamua kuwapeleka kwenye shule zinazofundisha ki-Filipino.
Estanislau Saldanha, Rais wa kamati ya kudumu ya bodi ya wakurugenzi wa DIT – Chuo cha Teknolojia cha Dili , anaamini kuwa sio halali kuwa na sheria kali katika matumizi ya lugha:
Desizaun nee viola konstituisaun RDTL konaba lian ofisial no viola lei base edukasaun konaba lian instrusaun iha eskola. Nunee viola direitu estudante nian hodi expresa no aprende iha lian nb fasil no tulun sira atu aprende kontiudu siensia nb lais.
Uamuzi huu unavunja katiba ya RDTL kuhusiana na masuala ya lugha rasmi na pia inavunja sheria ya msingi ya elimu ikizingatia lugha ya kufundishia shuleni. Kwa hiyo, inavunja haki ya wanafunzi ya kujieleza na kujifunza kwa urahisi lugha inayowasaidia kujifunza masuala ya kisayansi kwa njia iliyo rahisi.
Nae Rais wa Baraza la Habari la Timor-Lestè ndugu Virgilio da Silva Guterres anasema kuwa mapendekezo ya kufundisha sayansi lazima yajitokeze:
Eskola Fatumeta nee keta eskola lian portugues karik? Eskola nia objetivu nee atu aprende siensia. Lian, portugues ka ingles, nudar meiu ka instrumentu atu aprende., la'os objetivu. Ita labele uza labarik sira nudar objetu retaliasaun ba regra sira nebe uluk aplika ba ita. Eskola Soibada, Colégio Maliana, no Ossu nia regra vale no aplicável iha sira nia tempu. La'os ba tempu hotu-hotu. Husu Diretora eskola revoga regra nee.
Je, shule ya Fatumeta ilikusudiwa kuwa shule ya lugha ya Kireno? Lengo la shule hiyo ni kufundisha sayansi. Matumizi ya lugha ya Kiingereza au Kireno kama njia au zana ya kujifunzia, lengo sio lugha yenyewe. Hatuwezi kuwatumia au kuwahusisha watoto na taratibu ambazo zilishatumika kabla. Sheria za shule ya Soibada, Maliana na chuo cha Ossu zilikuwa sahihi na zinazotekelezeka kwa wakati huu (lakini) sio kwa kipindi chote (kwa leo). Nimemwagiza mkuu wa shule kuiondoa sheria hii. ( Wakati wa utawala wa kikoloni wa Ureno, shule hizi zilikuwa zinatumia sheria za elimu chini ya mamlaka ya kipindi cha udikteta )
Kashogy Junior, ambaye mdogo wake wa kiume anasoma shule ya msingi huko Dili aliandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa:
Mana, questão sira nene dala ruma atu leva ba mesa discução mos aluno sira iha duvida, Tauk hetan terminação estuda nian, ka hasai husi escola, tauk sira hetan transferencia ba escola seluk nebe mak sira la du'un gosta, e barak tan. Em tão, buat hotu lakon deit iha anin leten :). Istoria barak, so que ita mos hanoin ru-rua fali atu halo qeicha. Estudante sira ne balun em tão foti ne hansan “Joke” wainhira hetan sanção.
Wakati mwingine wanafunzi wanaogopa kuuliza maswali haya kwa sababu wanaogopa kufukuzwa shuleni. Wanaogopa kuhamishiwa katika shule ambazo hawapendi kwenda pia. Kwa hiyo “moshi nenda juu” ingawa kuna hadithi nyingi. Wanafunzi hufikiria mara mbili kabla hawajalalamika kuhusu jambo lolote. Wanafunzi wengine hulifanyia jambo mzaha likishathibitishwa.
Taarifa hizi za Timor Post zimekuwa za manufaa sana kwa jamii ya wa-Timor. Kuwapiga wanafunzi faini kwa sababu ya kuongea Kitetumi imeleta mshtuko mkubwa miongoni mwa jamii kwa sababu Kitetumi ni moja kati ya lugha rasmi nchini.