Picha ya Rais wa Uganda Akipiga Simu Pembeni mwa Barabara Yazua Gumzo Twita

A photo posted on Facebook by Presidential Press Secretary showing Ugandan President Yoweri Museveni speaking on the phone by the roadside.

Picha iliyowekwa kwenye mtandao wa facebook na Mwandishi wa Habari wa Rais Don Wanyama ikimwonesha Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiongea na simu pembeni mwa barabara.

Watumiaji wa mtandao wa Twita walitumiana picha za kuchekeshana baada ya kuonekana kwa picha inayomwonesha Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiwa amekaa kwenye kiti chake pembeni mwa barabara akiongea na simu. Msafara wake, ambao ulikuwa ukielekea kwenye shughuli ya kikazi, ulisimama kwa takribani dakika 30 kumsubiri apige simu.

Mwandishi wa Habari wa Rais Don Wanyama aliweka picha hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook ikiwa na maelezo yafuatayo:

Njiani kutoka Wilaya ya Isingiro jana ambapo alishiriki maadhimisho ya Siku ya Idadi ya Watu Duniani, Rais Museveni alisimama kwenye kijiji cha Kyeirumba ili aweze kupiga simu. Wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakijiuliza nini kinaendelea walikusanyika kumwona Rais, ambaye baada ya dakika 30 za kuzungumza na simu, alijichanganya nao kwa muda mfupi. Waliishukuru serikali kwa kuweka lami barabara iyo inayounganisha Uganda na Tanzania kupitia Isingiro.

Baadhi ya watu walikuwa na wasiwasi kuwa huenda picha hiyo ilikuwa sehemu ya mpango wa kuwafanya watu wasijadili habari za kuachiliwa huru kwa mwanasiasa wa upinzani Kizza Besigye, aliyekuwa kizuizini kwa muda wa miezi miwili akikabiliwa na mashtaka ya uhaini.

Picha na mjadala huu kumhusu Museveni ni mkakati wa kufunika tukio la kuachiliwa huru kwa Besigye lisijadiliwe kwa uzito mtandaoni

ALama ishara ya#ShindanolaM7 imetumiwa kuonesha picha za wa-Ganda na watu wengine duniani kote wakizungumza na simu zao pembeni mwa barabara. Rais Museveni anajulikana kwa jina la utani la M7 kwa sababu ya matamshi ya jina lake. Watumiaji wengine wa mtandao wa Twita wamekuwa wakiweka picha zilizohaririwa kumdhihaki rais huyo.

Haifahamiki Museveni alikuwa akizungumza na nani hasa wala kiini cha mazungumzo hayo.

Mtumiaji wa Mtandao wa twita aliamini kwamba Museveni alikuwa akizungumza na viongozi nchini Sudani Kusini, ambako mapigano yamelipuka:

Inawezekana M7 alikuwa na majadiliano ya “waachieni watu wangu waende zao” na viongozi wa Sudani Kusini

Museveni ameamuru jeshi la Uganda kuwaondoa wa-Ganda wanaoishi Sudani Kusini kufuatia mapigano yanayoendelea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Juba.

Rosebell Kagumire aliwaonya washiriki wa #ShindanolaM7 kutokujaribu kufanya kitu kama hiki:

Usijaribu hili nyumbani. Wasiliana kwanza na timu ya ubunifu ya #ShindanolaM7

Fredrick Tumusiime aliweka linalodaiwa kuwa tangazo la kituo kimoja cha televisheni nchini Uganda:

Kabla @ntvunga hayaifuta twiti yake

Watumiaji wengine wa Twita walitoa nje viti vyao vya ofisini ili kupiga simu:

Mathias Wandera alijaribu kumwonesha Museveni akipiga simu akiwa mwezini:

Sevo uko juu. Wasiompenda watasema picha hii ya kutengeneza

Shidnano hilo, kama anavyolitazama AutoblogKE, ni kuwakumbusha madereva:

Ha ha jamani nani anaweza kushinda shindano hili? Nadhani ni namna nzuri a kusema TUSIENDESHE HUKU TUKIANDIKA SMS/KUPIGA SIMU

Omara Ronnie alituma picha yake ya #ShindanolaM7 akiwa kwenye kijinjia kidogo kuonesha heshima aliyonao kwa watumiaji wote wa barabara:

Zote ni barabara…heshima kwa watumiaji wote wa barabara

iAfrikan alionesha picha ya timu ya taifa ya Ureno ikishangilia ushindi wa kombe la Ulaya wakati Museveni akiendelea kuongea na simu:

“Wasio mpenda rais watasema picha hii ni ya kutenegeneza”

Mathias Wandera aliweka picha ya Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe akiwa amepiga magoti mbele ya Museveni:

Picha za Museveni bado zinazunguka? Hehehe. Ngoja nijaribu hii.

Ory Okolloh Mwangi aliweka picha hii ikiwa na muhusika wa filamu ya Game of Thrones

Picha ya Mshindi wa Pili

Watoto hawakuachwa nyuma:

Shindano limechukua sura mpya

Wakati huo huo, Michael Kwambo anasubiri zamu yake ya kushiriki shindano hilo:

Jamani…tafadhali nijulisheni lini zamu yangu itafika nishiriki shindano…naomba nilisubiri kwa hamu

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.