Kuwa na Shahada Hakukuhakikishii Ajira Nchini China

Chinese graduates at a job exhibition in 2007. Photo from state news agency Xinhua.

Wahitimu wa shahada wakiwa kwenye Kongamano la Ajira mwaka 2007. Picha kutoka shirika la habari la Taifa Xinhua.

Kwa mara nyingine, zaidi ya wanfunzi milioni 7 nchini China wamehitimu shahada zao kutoka vyuo mbalimbali mwezi wa Mei. Ikiwa utawajumuisha wanafunzi 300, 0000 kutoka vyuo vya nje pamoja na wale waliohitimu miaka iliyopita na ambao bado wanatafuta ajira, hii ina maana kuwa, zaidi ya vijana milioni 15 wanadhaniwa kuwa wanatafuta ajira kwa mwaka huu.

Kama Taifa linaloibuka kwa kasi kiuchumi, China inachukuliwa kuwa na nafasi nyingi za ajira. Kwa kweli, kama utaamua kutafuta kwenye google “tafuta ajira nchini China”, utapata mamilioni ya majibu. Lakini ukweli ni kwamba, wahitimu wengi wa vyuo vikuu wanahangaika kutafuta ajira. Kwa hakika, kuna ule msemo ulioibuka miaka ya hivi karibuni kwamba “kuhitimu ni sawa na kukosa ajira”.

Mwaka 2013, kiwango cha ukosekanaji wa ajira kwa wahitimu wa vyuo vya kati na vyuo vikuu miezi miwili baada ya kuhitimu ilikuwa asilimia 17.6, hii ni kwa mujibu wa Times Higher Education; kwa wale wa vijijini, kiwangocha ukosekanaji wa ajira kilikuwa ni asilimia 30.5. Kiasi hiki ni kikubwa kuliko kiwango cha ujumla cha kukosekana kwa ajira, (au angalao kile kinachofikiriwa kuwa kiwango cha ukosekanaji wa ajira, kwani taarifa kutoka nje ya China hazina uhakika). Kwa kuwa uchumi wa China umekuwa ukishuka kwa miaka miwili iliyopita, hali ya kukosekana kwa ajira miongoni mwa wahitimu imezidi kuwa mbaya.

Mihemko ya kizazi cha vijana nchini China imeonekana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kupitia ujumbe mfupi wa simu za mkononi, kama inavyoonekana hapa:

当我们出生的时候,奶粉里都有毒了,当我们长身体的时候,只能吃垃圾食品了,当我们要上幼儿园的时候,开始乱收费了,当我们大学毕业的时候,毕业就是失业了,当我想努力赚钱的时候股市倒了,当我想努力谈恋爱的时候帅哥都成GAY了,当我想追求一切流行的时候,又开始非主流了!

Wakati tunazaliwa, mlo wa mtoto machanga ulikuwa na sumu, wakati miili yetu ikiwa inaendelea kukua, tulikuwa tunatumia mlo usio kamili; tulipoanza shule ya awali, ada ilikuwa kubwa isivyomithilika, tulipohitimu vyuo vikuu, hatukuajiriwa, tulipojaribu kujikimu kupitia soko la ndani, lilianguka, tulipojaribu kuingia kwenye mapenzi, tuligundua kuwa kila kijana mzuri alikuwa ni shoga; tulipojaribu kufuata miiko [Tamaduni na maadili], wala haikuwepo tena ile miiko.

所谓大学:管理监狱化,素质流氓化,Kiss公开化,消费白领化,上课梦境化,逃课普遍化,寝室网吧化,补考专业化,学费贵族化,论文百度化,近视全面化,食堂饲料化,求职梦想化,毕业失业化,就业民工化。

Nini maana ya chuo kikuu: utawala ni kama jela, ubora ni kwa ajili ya wahuni. [Wanafunzi] wanajifunza namna ya kubusiana hadharani, matumizi yao ni kama mfanyakazi wa kigeni na ndoto za alinacha darasani. Kutokuhudhuria masomo ni jambo la kawaida, mambweni ni kama sehemu za huduma za intaneti. Kufanya mitihani kumekuwa ni utaalam, wanaomudu ada ya shule ni wale walio na uwezo tu. Andiko la utafiti linaonekana kama matokeo ya utafutaji kupitia Baidu. Kila mtu anajengewa matarajio yasiyo na tija. Chakula kwenye migahawa ya shule ni ya kulishia wanyama. Kupata kazi ni kama ndoto. Kuhitimu masomo ni sawa na kukosa kazi. Ajira zilizopo ni kwa wahamiaji kutoka vijijini kuja mjini.

Watu wengi wanaamini kwamba moja ya mambo yanayochangia tatizo la ukosefu wa ajira miongoni mwa wahitimu wa vyuo vikuu wa hivi karibuni ni sera ya mwaka 1999 ya kuongeza udahili vyuo vikuu. Kabla ya hapo takribani asilimia 35 tu ya wahitimu wa shule za upili ndio waliopata nafasi ya kusoma kwenye vyuo vya kati, vyuo vya ufundi ana vyuo vikuu. Lakini, kwa mwaka 2015, asilimia hii ilikuwa ni zaidi ya asilimia 80, na pia takribani asilimia 40 walijiunga na shahada ya kwanza kwenye vyuo vikuu. Kwa majiji makubwa kama vile Beijing, kiasi cha wanfunzi waliojiunga na vyuo vikuu kilikuwa zaidi ya asilimia 70.

Baadhi ya watu wanaona kuwa, hakuna ajira za kutosha kwa idadi iliyopo ya vijana wengi wanaohitimu elimu ya chuo kikuu. Kwenye mtandao maarufu wa kijamii wa Weibo, Lydia alitoa maoni kuhusu vyuo kutoa idadi kubwa sana ya wahitimu:

以后大学生越来越不值钱了,一抓一大把,有什么区别?

Wahitimu wapo kila mahali, na pia wahitimu wa vyuo vya kati kwa sasa hawathaminiwi kabisa. Unawezaje kuleleza tofauti?

Mtumiaji mwingine wa Weibo, “Nomadic hero”,  aliandika kwamba moja ya madahara ya kuongeza wigo wa udahili ni kushuka kwa ubora wa wahitimu kwa ujumla:

国家维护学习公平尽力让大多数人享有受教育固然是好事,可整体学生质量一蟹不如一蟹。不是大学生不值钱了,而是大学贬值了

Vita dhidi ya upatikanaji wa usawa ili kila mmoja apate fursa ya kwenda shule ni jambo jema. Hata hivyo, ni ukweli mtupu kwamba ubora wa wanafunzi unazidi kupotea. Ni chuo kinachopoteza thamani kuliko hata wanafunzi.

“Ling Yan San Chi” alitoa lawama:

毕业两年啦!!!!我竟然还在想着如何找工作,,,为何活的如此悲催。。。

Nimehitimu miaka miwili iliyopita, lakini bado ninafanya kazi ya kutafuta ajira!!, kwa nini maisha yangu yananiendea kombo namna hii?

Pamoja na kuwa bado ni vigumu kupata kazi, watu wengi wanamtazamo kuwa, kwenda chuo kikuu bado ni njia muafaka ya kupata utaalam na kujikwamua kimaisha — na hivyo, hawajutii maamuzi yao. “HaiDe XiaTian” kwa mfano, anafikiria kuendelea na masomo ya uzamili:

后悔啊,可是后悔又能怎样 只能硬着头皮走下去,考研是通往理想大学的最后也是唯一的机会

Ninajisikia kukata tamaa [ kusoma masomo ya elimu ya juu], lakini hakuna namna nyingine, na ninapaswa kuendelea na njia hii hii. Kujiunga na masomo ya uzamili kutanipa fursa ya kupata chuo kikuu halisi.

Sherehe ya kuhitimu huitwa kuanza, ikiwa na maana ya mwanzo mpya kwa wahitimu, lakini wengi wanachukulia hali hii kama juhudi za mtu binafsi, kama ilivyo kwa mtumiaji wa Weibo UsedToBe5:

找工作是一件考验人心的事情,不断地失败再爬起,当然这都是我自己选择的地狱模式…

“Kupata ajira ni kazi ngumu sana kwa kuwa yakupasa kuanguka na kuinuka tena mara nyingi iwezekanavyo.”. Kwa kweli, sina yeyote wa kumlaumu kwani haya yalikuwa ni maamuzi yangu mwenyewe.

Hata hivyo, siyo kila mmoja amepoteza imani na hali hii. Kiungo habari kwenye Weibo kinachojulikana kama #kuhitimu hakumaanishi kukosa ajira# kinaupa mjadala huu sura tofauti, na pia jumbe zinajaribu kutoa hamasa, ushauri na uzoefu binafsi.

Chapisho la mwisho kuhusiana na kiungo habari hapo juu lilichapishwa  Julai 12 kwenye Weibo na mtumiaji”WanAn Xin XinYu,” ambaye alikuwa miongoni mwa wahitimu wapya milioni 7 wa mwaka 2016:

今天又要去面试工作了,希望明天能开始工作 #毕业不等于失业#加油!虽然已经失业快一个月了

Leo nitahudhuria usaili mwingine, na pia ninatamani kuanza kazi hata kesho. #kuhitimu hakumaanishi kukosa ajira# Add oil [ ni maneno ya kutia hamasa ]! Pamoja na kuwa ni mwezi sasa umepita sijapata ajira.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.